Waziri Kigoda alisema,''Alisema,nawazadieni hivi vifaa vya michezo,halafu baadaye, mwende pale mkajiandikishe'' hakusema explicitly wachukue kadi cha Chama,lakini it implies kwamba alikuwa anataka wachukue kadi a Chama.
Lakini sidhani kama ni kosa. Mimi nilikuwa nasoma Kibaha Sec. na Jakaya Kikwete ,alianzisha tawi la TANU pale Shule ya Kibaha. Amelianzisha yeye. Halafu alikuwa anafanya sana activism. Fikiria,Kihaha Sec. ilikuwa Elite School. Hali ya maisha ya wanafunzi ilikuwa nzuri sana. In spite of all that Kikwewte aliandika article kwenye gazeti la ''The Nationalist'' titled ''Is Kibaha Sec a colony of the Nordic Countries?'' Basi akaitwa Wizara ya Elimu,akaambiwa mambo uliyoandika sawa kabisa,lakini hawa watu wanatusaidia,kwa hiyo leave them alone.'' Lakini this incident made him stand out from the crowd pale Kibaha. Akaonekana kwamba huyu mtu moto wa kuotea mbali. Halafu alipokuwa Chuo Kikuu,alikuwa vice president katika student government. Kwa hiyo,very often,hawa politicians,hizi activities wanaanzia shuleni.
Ukitazama maisha ya Bill Clinton,pamoja pia na Hillary Clinton,unaona pia kwamba , politics wameanza shuleni,running for class president.[Indeed,siyo politics tu,na ufuska pia Bill Clinton alianza zamani. Lakini student politics wakati ule ilikuwa siyo masihara,ilikuwepo Vietnam War,na wanafunzi walikuwa wanachomolewa darasani wanapelekwa Vietnam,ingawa Bill Clinton alifanikwa kukwepa draft,ingawa,usimuulize ukionana naye,kwa sababu this is a very sensitive subject,
Mambo mengi unajifunza,ukisoma kuhusu maisha yake,kwamba alikuwa anatumia cocaine,hata alipokuwa Governor wa Arkansas,yaani cocaine,actual cocaine. Lakini unajifunza mengi unapofahamu kuhusu maisha ya Clinton. Alikuwa ana pollster wake anaitwa Billl Morris,ambaye alikuwa hodari sana wa kuchukua polls,kiasi kwamba Bill Clinton kila siku alikuwa anaongea tu mambo ambayo wananchi wanataka kusikia,that is why Bill Clinton always spoke slowly and deliberatetly]
Lyndon Johnson pia politics zake ameanza shuleni. Na huko ndio wanasema zilionekana tabia zake za usiri,kupenda kufanya mambo kwa siri,message yoyote ikishasomwa.lazima iwe destroyed;, tabia za ubabe. In fact ukisoma life history ya Johnson, hutaona vigumu sana kuelewa kwa nini Kennedy Presidency ilikiwisha 'aforetime.[Lakini hii inatupeleka nje ya mada]
Kwa hiyo idea ya kuwafundisha politics wanafunzi siyo mbaya. And yet unaona kwamba Waziri Kigoda hathubutu kutamka waziwazi wanafunzi wachukue kadi ya Chama.