Ni Sahihi Waziri Kuhamasisha Wanafunzi wa Sekondari kuchukua Kadi ya Chama? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni Sahihi Waziri Kuhamasisha Wanafunzi wa Sekondari kuchukua Kadi ya Chama?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Albedo, Feb 27, 2010.

 1. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #1
  Feb 27, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,565
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Jana nilikuwa naangalia Taarifa ya Habari Channel ten, nikamuona Aisha Kigoda akigawa Misaada huko Handeni, Moja kati ya Misaada aliyogawa ni Mpira mmoja wa Miguu na mmoja wa Netball kwa Wanafunzi wa Shule moja ya Sekondari. Baada ya Kugawa Mipira hiyo akaawaambi

  " Mkimaliza Mwende pale Mkajiandishe halafu Mpewe Kadi" Sasa nikajiuliza ni Kadi za Harusi, za Mwaliko au za CCM! Is this correct? Kwa Wazuri kuhamasisha vitoto vya Shule viwe viwanachama vya Chama fulani baada ya Kutoa Hongo ya Mipira
   
 2. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #2
  Feb 27, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,415
  Likes Received: 2,051
  Trophy Points: 280
  Hapa best hatuwezi jua ni kadi za nini manake zipo za aina nyingi mfano kliniki, chakula kwa wanaokula shule, bima kwa wale wanaozitunza kwa mamatroni wao. But all in all kama ni za chama basi haya ni makosa but usiwe na shaka kwani hawa watoto hawapigi kura na kama ni shule ya msingi bado sana labda 2015 na wengi wao watakuwa wamekwisha elewa chama chao na watakihama tu.
   
 3. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #3
  Feb 27, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Sio sahihi hata kidogo.Ndivyo ilivyo hii miviongozi ya CCM hata Pinda huwa anatumia madaraka yake vibaya.
   
 4. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #4
  Feb 27, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  hiyo ni sign ya kukosa wafuasi sasa wanataka kutumia vijana wapate wafuasi maana baba zao na mama zao wameshakosa imani na CCM
   
 5. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #5
  Feb 27, 2010
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,704
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Mhh! sichangii lolote mana sijui sana hizi siasa, haki, kutoa elimu na kuhamasisha watu wachukue haki zao.
   
 6. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #6
  Feb 27, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,699
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  La muhimu ni umri ndugu!!! the rest ni propaganda!
   
 7. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #7
  Feb 27, 2010
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 5,550
  Likes Received: 1,590
  Trophy Points: 280
  kampira kamoja! na hapo hapo unatakiwa ukachukue kadi, mwe!
   
 8. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #8
  Feb 27, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,565
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Acha tu
   
 9. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #9
  Feb 27, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,257
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Kabla ya kuanzisha hii thread ilitakiwa kwanza upate uhakika pasipo shaka kwamba ni kadi gani alizokuwa anazizungumzia vinginevyo mjadala mzima unakuwa hauna basis ya discussion.
   
 10. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #10
  Feb 27, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,565
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu Sidhani kama Unatarajia watu wajiandikishe na Kuchukua Kadi za Kipaimara kwenye Mkutano wa Kisiasa
   
 11. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #11
  Feb 27, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 14,794
  Likes Received: 1,431
  Trophy Points: 280
  Weye bana- great thinker. Umenifurahisha. Alafu mipira miwilu ya kichina ni tsh 20,000/ exchuzi mwah!
   
 12. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #12
  Feb 27, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,257
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Ni wapi kwenye hii thread ulipoonyesha kuwa huo ulikuwa mkutano wa siasa?kama una-data zitoe ili mjadala upate nyama, ila kwa thread ilivyo sasa sioni tutaujadili kwa basis gani.
   
 13. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #13
  Mar 1, 2010
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,013
  Likes Received: 1,216
  Trophy Points: 280
  Waziri Kigoda alisema,''Alisema,nawazadieni hivi vifaa vya michezo,halafu baadaye, mwende pale mkajiandikishe'' hakusema explicitly wachukue kadi cha Chama,lakini it implies kwamba alikuwa anataka wachukue kadi a Chama.
  Lakini sidhani kama ni kosa. Mimi nilikuwa nasoma Kibaha Sec. na Jakaya Kikwete ,alianzisha tawi la TANU pale Shule ya Kibaha. Amelianzisha yeye. Halafu alikuwa anafanya sana activism. Fikiria,Kihaha Sec. ilikuwa Elite School. Hali ya maisha ya wanafunzi ilikuwa nzuri sana. In spite of all that Kikwewte aliandika article kwenye gazeti la ''The Nationalist'' titled ''Is Kibaha Sec a colony of the Nordic Countries?'' Basi akaitwa Wizara ya Elimu,akaambiwa mambo uliyoandika sawa kabisa,lakini hawa watu wanatusaidia,kwa hiyo leave them alone.'' Lakini this incident made him stand out from the crowd pale Kibaha. Akaonekana kwamba huyu mtu moto wa kuotea mbali. Halafu alipokuwa Chuo Kikuu,alikuwa vice president katika student government. Kwa hiyo,very often,hawa politicians,hizi activities wanaanzia shuleni.
  Ukitazama maisha ya Bill Clinton,pamoja pia na Hillary Clinton,unaona pia kwamba , politics wameanza shuleni,running for class president.[Indeed,siyo politics tu,na ufuska pia Bill Clinton alianza zamani. Lakini student politics wakati ule ilikuwa siyo masihara,ilikuwepo Vietnam War,na wanafunzi walikuwa wanachomolewa darasani wanapelekwa Vietnam,ingawa Bill Clinton alifanikwa kukwepa draft,ingawa,usimuulize ukionana naye,kwa sababu this is a very sensitive subject,
  Mambo mengi unajifunza,ukisoma kuhusu maisha yake,kwamba alikuwa anatumia cocaine,hata alipokuwa Governor wa Arkansas,yaani cocaine,actual cocaine. Lakini unajifunza mengi unapofahamu kuhusu maisha ya Clinton. Alikuwa ana pollster wake anaitwa Billl Morris,ambaye alikuwa hodari sana wa kuchukua polls,kiasi kwamba Bill Clinton kila siku alikuwa anaongea tu mambo ambayo wananchi wanataka kusikia,that is why Bill Clinton always spoke slowly and deliberatetly]
  Lyndon Johnson pia politics zake ameanza shuleni. Na huko ndio wanasema zilionekana tabia zake za usiri,kupenda kufanya mambo kwa siri,message yoyote ikishasomwa.lazima iwe destroyed;, tabia za ubabe. In fact ukisoma life history ya Johnson, hutaona vigumu sana kuelewa kwa nini Kennedy Presidency ilikiwisha 'aforetime.[Lakini hii inatupeleka nje ya mada]
  Kwa hiyo idea ya kuwafundisha politics wanafunzi siyo mbaya. And yet unaona kwamba Waziri Kigoda hathubutu kutamka waziwazi wanafunzi wachukue kadi ya Chama.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...