Ni sahihi viongozi kumlazimisha Magufuli aongeze muda madarakani?

Hakuna upumbavu kama huo, yeye amalize tu muda wake atembee salama! Unafikri Mkapa kwa yale aliyoyafanya angeweza kutoka? Tuache upumbavu!!
 
Ni sahihi kwa viongozi mbalimbali kumlazimisha Magufuli kuongeza muda wake madarakani...
Je ameshafikia hata nusu ya Yale aliyoyafanya hayati MWL.Julius Kambarage Nyerere....
Aliyo ahidi atayatekeleza yote anahitaji pongezi au la

Hali ya kisiasa, kijamii, kiuchumi, kitekinolojia, ki mazingira katika ngazi za ndani na nje kwa wakati wa Mwalimu, si sawa na wakati wa Magufuli.

Sioni kama ni haki na ni halali kumtaka Magufuli afanye nusu ya aliyoyafanya Mwalimu kwa miaka mitano wakati Mwalimu aliyafanya kwa miaka 17.5

Kama ni kulinganisha, mlinganishe Mwinyi na Nyerere maana walifuatana, halafu mlinganishe Mkapa kwa Mwinyi, na umlinganishe Kikwete kwa Mkapa, kisha umlinganishe Magufli kwa Kikwete. Mazingira aliyoyakuta Kikwete baada ya Mkapa, siyo aliyoyakuta Magufuli kwa Kikwete. Hali aliyoiacha Mwinyi siyo aliyoikuta kwa Nyerere.

Hapa kuna mawili. Ukikuta mtangulizi wako amevurunda na kuharibu hali aliyoikuta yeye, utaanzia chini kuliko alipoanzia yeye na hivyo marekebisho na magumu kuliko muendelezo.

Kumlinganisha Magufuli na Nyerere ni kumuonea na ni abuse ya juhudi zake.
 
Ni sahihi kwa viongozi mbalimbali kumlazimisha Magufuli kuongeza muda wake madarakani...
Je ameshafikia hata nusu ya Yale aliyoyafanya hayati MWL.Julius Kambarage Nyerere....
Aliyo ahidi atayatekeleza yote anahitaji pongezi au la

Hujui kama nyerere aliongoza miaka zaidi ya ishirini
 
Mmerudi tena na hoja zenu za kuongezewa muda!Wako watu wazuri tu ndani ya ccm hata nje ya ccm wanafaa kuongoza nchi na tukafika mbali.Mazuri unayoyaona leo mengi yalianzishwa awamu zilizopita na isitoshe anakamilisha tu,hao waliopita wangeamua kujiongezea muda angekuwepo leo?Acheni tamaa kwakuwa mnafaidika na uwepo wake!Anamazuri yake na mapungufu yake pia,mwacheni akimaliza muda wake apumzike aje mwingine!
 
Ni sahihi kwa viongozi mbalimbali kumlazimisha Magufuli kuongeza muda wake madarakani...
Je ameshafikia hata nusu ya Yale aliyoyafanya hayati MWL.Julius Kambarage Nyerere....
Aliyo ahidi atayatekeleza yote anahitaji pongezi au la
Hata kama angefanya mazuri zaidi ya malaika, lakini Sheria na Katiba ya nchi lazima hieshimiwe. Ndio maana wakaweka ukomo wa Miaka ya Uraisi.
 
Mmerudi tena na hoja zenu za kuongezewa muda!Wako watu wazuri tu ndani ya ccm hata nje ya ccm wanafaa kuongoza nchi na tukafika mbali.Mazuri unayoyaona leo mengi yalianzishwa awamu zilizopita na isitoshe anakamilisha tu,hao waliopita wangeamua kujiongezea muda angekuwepo leo?Acheni tamaa kwakuwa mnafaidika na uwepo wake!Anamazuri yake na mapungufu yake pia,mwacheni akimaliza muda wake apumzike aje mwingine!
Sisemi Magufuli ni dictator Ila nchi zenye viongozi mfano Kama wake zimeonekana zikipata maendeleo kwa mfano raisi wa kwanza wa China MAO ZEDONG ndiye aliyeifikisha China ilipo..

Kwa uongozi wake China sasa ndio Large Industrial Power na the Economic Giant...

Wengine kama Benito Mussolini wa Italia na Fidel Castro wa Cuba wote wameleta mabadilko kwenye nchi zao
 
Sasa na Kina Nyerere waliofanyaa makubwa kwenye hii nchi ambapo Kuna baadhi ya wananchi waloamini kwamba Nyerere akitoka madarakani nchi itakngia vitani,lakini mambo yamekwenda sawa, akili ni kwake akikaza shingo itavunjika.
 
Ni sahihi kwa viongozi mbalimbali kumlazimisha Magufuli kuongeza muda wake madarakani?

Je ameshafikia hata nusu ya yale aliyoyafanya hayati MWL.Julius Kambarage Nyerere..

Kwa asilimia kubwa atakuwa ametekeleza mengi Kati ya yale aliyoahidi lakini je raisi atakayekuja atakuja kivingine....

Ama ni 10 kwa 10 kisha sepa zako
Watu wanamsifia sana Mkapa baada ya kufariki.

Wakumbuke Mkapa alisema nini kuhusu marais kujiongezea muda madarakani.

Mkapa alipinga sana hii habari.

Kwenye kitabu chake kaandika vizuri alivyompinga Salmin Amour wakati Salmin alivyotaka kujiongezea muda urais wa Zanzibar.

Kama Magufuli anamuheshimu kweli Mkapa kama anavyodai, akatae hizi habari za kuongezewa muda wa urais.

Soma kitabu cha Mkapa uone alivyoandika.

Soma hii makala.

Mkapa on presidential term-limits
 
Role model wake (alye pumzishwa leo nyumba ya milele) alikaa kimya kimtego, maana yake ni kwamba hakukubaliana na kuongezewa muda, binafsi najua JPM mtego huu hataukubali ili a-keep standards...
Mkapa hakukaa kimya kuhusu term limits.

Alipinga vikali sana.

Mpaka kwenye kitabu chake kaandika alivyompinga Salm8n Amour wakati Amour anataka kuongeza muda wake wa urais.

Mkapa kaandika vizuri sana anavyopinga marais kuongeza muda wa urais.

Magufuli akikubali kuongeza muda atakuwa kakataa kabisa falsafa za Mkapa.

Soma kitabu cha Mkapa, soma makala hii.

Mkapa on presidential term-limits
 
Kwa aliyoyafanya Mkapa na Magufuli mwenyewe kakiri basi wa kuongezewa muda alikua ni yeye marehemu Ben Mkapa na si vinginevyo. Lakini si tu kwamba alikataa upuuzi huo unaopigiwa debe na wachumia tumbo wanaojipendekeza kwa mtawala wa wakati husika bali pia alilipinga kwa nguvu zake zote lisitokee Tanzania

No matter how good a dancer you are, you must leave the stage
 
Automatically Magufuli inabidi aongezewe muda tu. Kupitia Magufuli tutafika mbali sana kama nchi na itachukua miaka mingi kumpata mtu mwenye dhamira ya dhati kama Magufuli.
Fikiri kabla ya kutenda ujenzi na nidhamu kazini
 
Back
Top Bottom