Ni sahihi viongozi kumlazimisha Magufuli aongeze muda madarakani?

zagarinojo

JF-Expert Member
Jul 26, 2020
2,622
2,835
Ni sahihi kwa viongozi mbalimbali kumlazimisha Magufuli kuongeza muda wake madarakani?

Je ameshafikia hata nusu ya yale aliyoyafanya hayati MWL.Julius Kambarage Nyerere..

Kwa asilimia kubwa atakuwa ametekeleza mengi Kati ya yale aliyoahidi lakini je raisi atakayekuja atakuja kivingine....

Ama ni 10 kwa 10 kisha sepa zako
 
Kwa maoni yangu binafsi ni sahihi kumuongezea muda sababu kazi anayofanya inajieleza yenyewe,, tubadilishe ili tupate nini zaidi,,?
 
Automatically Magufuli inabidi aongezewe muda tu. Kupitia Magufuli tutafika mbali sana kama nchi na itachukua miaka mingi kumpata mtu mwenye dhamira ya dhati kama Magufuli.
 
Fikeni nyie, binafsi sihitaji kusikia, watu walifanya makubwa Sana lakini hamyasemi
 
Role model wake (alye pumzishwa leo nyumba ya milele) alikaa kimya kimtego, maana yake ni kwamba hakukubaliana na kuongezewa muda, binafsi najua JPM mtego huu hataukubali ili a-keep standards...
 
Role model wake (alye pumzishwa leo nyumba ya milele) alikaa kimya kimtego, maana yake ni kwamba hakukubaliana na kuongezewa muda, binafsi najua JPM mtego huu hataukubali ili a-keep standards...
Iwapo wananchi watamtaka walio wengi anaweza kugeuka na kuyapa mgongo matwaka yake na kuendelea kwani hata Nyerere alituongoza miaka mingapi mazee
 
Ni sahihi kwa viongozi mbalimbali kumlazimisha Magufuli kuongeza muda wake madarakani...
Je ameshafikia hata nusu ya Yale aliyoyafanya hayati MWL.Julius Kambarage Nyerere....
Aliyo ahidi atayatekeleza yote anahitaji pongezi au la
Ngoja waje wenye wagombea mamluki wanaowawakilisha mabeberu wakutolee povu! Vaa barakoa kabisa!
 
Iwapo wananchi watamtaka walio wengi anaweza kugeuka na kuyapa mgongo matwaka yake na kuendelea kwani hata Nyerere alituongoza miaka mingapi mazee
kama JPM ni smart, mchezo wa kuongezewa muda hataukubali come what may... Muda ukifika tutaongea zaidi
 
mimi hata hii mitano nimeona ni mingi. ingekuwa mimi ndo tanzania basi ningeshamtimua kwenye urais toka 2016
 
Kazi kujenga ma barabara bila mpangilio, huku sumbawanga umasikin unaongezeka
Ila wanasema ukifanya jambo ukaona kila mtu anakusifia ujue your not right Ila ukifanya jambo kukawepo na two sides ujue your right move on
 
mimi hata hii mitano nimeona ni mingi. ingekuwa mimi ndo tanzania basi ningeshamtimua kwenye urais toka 2016
Kwa kosa lipi tena Mkuu kwani waliopita walikuwa poa kila idara
Au na yeye mpaka afe ndo tuanze kukubali utumishi wake
 
Kwa uzuri gani Haya aliyoyafanya ni viporo vya marehem mkapa labda ndege tu lakini hana jipya
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom