Ni sahihi mzazi kumnunulia mwanafunzi simu?

Ni sahihi mzazi kumnunulia mwanafunzi simu?

mkuu, maisha ya chini tu, sasa mimi nimepewa hivo wenzangu niliosoma nao walikuwa wameshaanza kuvitumia,watu walikua na psp, ipod na makorokocho mengine mengi

Daa luck you...io la saba hata kugusa laptop nilikua sijawahi,ilikuwepogi tuu computer flan za dell za zaman sana nyumbani ndio nilikua naitumia tumia (kwa kuchezea magemu tuu)
 
Kiukweli watoto wakike wengi wao wanaanza kuwa na simu kabla ya hata wazee wao kuwanunulia. Weng wao huanzia tokea kidato cha kwanza kwa siri, hunuliwa na mabwana wao. Wanaoishia kukamatwa na wazee wao ni wachache mno mana wengi wao huwa wasiri kinoma.
Ukitizama kimazingira mtoto anapofika kidato cha 4 basi tayari anahitajika kuwa na simu kutokana na mazingira yalivo. Lakni kiuhalisia huo umri bado nu mbaya sana mtoto kumilikia simu. Kiufupi tunaishi katika dunia ngumu sana kwa kweli.
 
Wazee wa sasa tujifunze kubadilika, tusiwanunulie watoto wetu ambao ni wanafunzi wa shule za msingi au sekondari simu hata kama tuna uwezo ndio mwanzo wa kuwapoteza, walau mwanafunzi wa chuo ndio wa kununuliwa simu ambapo hapo tayari atakuwa na miaka 20 au zaidi, hapo akili yake tayari itakuwa imeshatulia kiasi. Na sio mtoto tena kulingana na katiba ya nchi.
 
Mimi nilianza kumiliki nikiwa na miaka 19
 
Simu zinaharibu sana watoto wetu/wadogo zetu ...niombe serikali yetu tukufu ipige marufuku utumiaji wa simu kwa wototo wadogo hasa wanafunzi sheria iwe ...lazima uwe na miaka 18 ndio utumie simu..!
 
Back
Top Bottom