Ni sahihi mwanaume kubadili dini yake na kufuata dini ya mchumba wake?

Mzee Chapuuka

Member
Apr 21, 2017
97
243
Mada tajwa yahusika,

Siku hizi kumekua na mtindo wa watu kubadili dini na kufuata zile za wapenzi wao ili hatimaye wafunge ndoa. Siku za nyuma tuliona wanawake ndio hubadili dini na kufuata dini za wapenzi wao. Ila siku hizi wanaume nao hubadili dini na kuwafuata wachumba ( wake zao) wao,Je kiutamaduni wa Kiafrica/Tanzania kufanya hili Jambo ni busara kweli?

Tujadili
 
Yan kubadili dini kw a sababu ya kupenda?!!
Mapenzi yanaishaga jamn..badili dini kwa sababu umeamini na umeona huko unapoenda ni bora zaidi kuliko ulipotoka.
 
Mada tajwa y
Ila siku hizi wanaume nao hubadili dini na kuwafuata wachumba( wake zao) wao
Je kiutamaduni wa kiafrica/Tanzania kufanya hili Jambo ni busara kweli?
Tujadili
Kitu chochote chaweza kuwa sahihi au sio sahihi kutokana na tamaduni za watu husika
 
Back
Top Bottom