Ni sahihi mke wako kushirikiana na mpangaji mwenzake kupika kila siku?

Mtoa mada acha uchoyo na ubinafsi, huijui kesho yako, nasikitika mkeo kapata mwanaume mwenye roho mbaya. Khaaaah.

Hao ndio majirani na watu wako wa karibu, ukumbuke hilo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndo maana nimekuja kuuliza nipate mwanga kama kuna mipaka ya watu kushirikiana mambo fulani yanaohusu wenzi..poa nachukua maoni yako kwamba ni sawa kusaidiana vyakula.asante nathamini mchango wako
 
Mbona zoezi ni dogo sitisha kununua vitu kwa jumla tu.kisha anza kama jamaa kuacha kodi ya kichwa kidogo mnooo na siku nyingine usiache.
Yy ataelewa kwa vitendo kua unamanisha nn mpk hapo.
Asante sana na hili ndilo ninalofikiria kwa sasa..leo ilikuwa nikanunue vya jumla lakini mienendo ya siku za nyuma imeniwazisha nafikiria kurudi tena kwenye vya reja reja.
 
Mimi hapo sioni cha ajabu watu kusaidiana coz huwezi kujua kesho na keshokutwa hiyo familia wanaweza kuja kuwa msaada mkubwa sana kwako. Pili Hakuna mtu aliyefilisika kwa kumsaidia jirani yake chakula . Hebu tuacheni uchoyo na roho mbaya ambayo wengi hmu ndani nimeona imewajaa. Ujamaa ni jadi ya Watz hasa wale wanaotokea kanda ya ziwa watakuw mashahidi
 
Mpige marufuku.
Kama hauwez then fanya reverse psychology. Fuatilia ujue nan anapika. Akipika jirani, siku hyo sifia sana chakula na kula cha kucheba, akipika wife vunga. Wanawake wana wivu, muda si mref utaona anakwambia wamevunja mahusiano
 
Assume una mke mdogomdogo mama wa nyumbani na bado hamjapata mtoto, sasa mnaishi kwenye nyumba moja mko wapangaji wawili tu; yaani mtu na mkewe ambao hawana pia mtoto ila wenyewe hawana kazi ya kipato cha kati, wanaunga unga maisha yaendelee.

Mara nyingi mume wake anatoka asubuhi anarudi usiku leo kapata kidogo kesho kakosa nyakati nyingi hamuachii mkewe hela yoyote ya mezani.

sasa wewe kipato chako sio haba sana unapata salary mpaka ya kuwa na na uwezo wa kununua vitu vya jumla ukaweka ndani mchele, mafuta, unga, gas,nyanya,vitunguu na kadhalika.

Sasa inaibuka tabia ya mkeo kuanza ku share kupika na yule mdada mpangaji..na mke anakutamkia wazi kabisa kwamba wanashirikiana kupika jirani yake huyo ananunua mboga na viungo vya mchana halafu mimi tanunua mboga za usiku.

Anadai kwamba hata kwao kijijini ulimpomtoa huwa wanapika na wifi yake wanakula pamoja na kwamba hajazoea maisha ya choyo. Anadai niwaache waendelee kushirikiana kwa sababu chakula cha kula mwenyewe hakimnogei ikumbukwe me huwa natoka asubuhi na mchana nakula kazini narudi usiku tu.

swali langu wakuu wenye uzoefu mnaonaje je hapo hakuna kuhujumiana kweli maana me nahisi kwa uwezo wangu ndo natoa mchango mkubwa sijawahi kuona wao wanunue vitu kwa jumla.

Je, nimkubalie mke wangu tu alivyozoea kumsaidia jirani yake? Maana kweli kuna siku za kuishiwa pengine jirani yake atamsaidia pia chakula alichonach,o ila sasa roho inauma maana nahisi kama mke wangu hana uchungu na maisha yalivyo magumu; anahisi me napata hela nyingi huku kazini.

Hali hio ni ya kawaida kweli kwa mke kusaidiana kupika na kuosha vyombo na mpangaji mwenzake wa pekee na umri wa mke ni miaka 18.
Uzuri hiyo ni nyumba ya kupanga siyo yako ,kwa hiyo hama haraka sana
 
Back
Top Bottom