Ni sahihi kwa mwanaume kuoshwa miguu?

Ni sahihi kwa mwanaume kuoshwa miguu?

Adimu

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2013
Posts
678
Reaction score
308
Siku hizi kuna biashara ya urembo ambapo wanawake huoshwa miguu na vijana wanaotoa huduma hiyo, unakuta mwanamama kaweka miguu juu anasafishwa sijui kucha sijui ni miguu haya.

Cha ajabu na chakusikitisha kuna wanaume nao wanatumia huduma hii na mpaka naandika uzi huu kuna jamaa mtumzima tu yuko jirani yangu na hapa ni sehemu ya starehe na kuna watu weengi ila bila haibu katenga miguu juu ya mapaja ya kijana wa kiume na anasafishwa miguu.

Kwakweli kwaupande wangu naona si sahihi na inapaswa tuwaachie wanawake mambo haya. vipi kwa upande wenu wadau hii imekaa sawa?
 
Atataka hadi kusuguliwa mgongo na mwanaume mwenzie
huyo sio mwanaume mwenzio
 
Apana Mie Wangu namuosha mwenyewe, massage Ya kichwa mwenyewe staki hashuo..
 
hawa vijana wanasaidia sana hasa kwa wanaume wenye vitambi kutukata kucha na ni mgawanyo wa rizik,utakiwi kushangaa jamaa
 
Sasa kwann usimkabizi jukumu ilo mke wako mpaka mwanaume mwenzio?
 
Kwa nini unakuwa mbaguzi? Ka ni sawa kwa mke wangu kuoshwa miguu na vijihunihuni wakati miye nikiwa sipo, tena wengine siku hizi huingia hadi sebuleni, basi na miye niagize kasichana kanioshe miguu yangu. Si kila muonshwa ni bwabwa. Wengine hawana hata mda wa kuangalia miguu yao, kucha, fangas etc. Kamata mtu mjuzi wa kazi hizo, kwa nini asioshwe? Usiidharau ofisi ya mtu. Sijui ka nimeuelewa
 
Ivi mwanaume anasuguliwa kucha anataka akamringishie nani? Basi tuanze kupakwa na rangi na tuvae skuna ili kucha zionekane! Hii niofisi sawa lakini inawahusu akina mama
 
Kwa nini unakuwa mbaguzi? Ka ni sawa kwa mke wangu kuoshwa miguu na vijihunihuni wakati miye nikiwa sipo, tena wengine siku hizi huingia hadi sebuleni, basi na miye niagize kasichana kanioshe miguu yangu. Si kila muonshwa ni bwabwa. Wengine hawana hata mda wa kuangalia miguu yao, kucha, fangas etc. Kamata mtu mjuzi wa kazi hizo, kwa nini asioshwe? Usiidharau ofisi ya mtu. Sijui ka nimeuelewa

Hiyo lugha tu inaonesha unaoshwa.Wape riziki.
 
Inaitwa pedicure...professionals wanaelewa zaidi. Ila my hubby aligoma...😄
 
Mambo ya kuiga yanatuathiri sana waafrika, tunaacha kufata asili zetu tunapna kila kitu ni fashion.

Ni aibu sana.
 
Inaitwa pedicure...professionals wanaelewa zaidi. Ila my hubby aligoma...í-½í¸„

Lakini inaonekana kama unaruhusu huyo hubby wako aoshwe sio?
 
Back
Top Bottom