Ni sahihi kwa Askari kujitambulisha Bar na kupiga stori za kazi zao mbele ya raia? Ni kutafuta kuogopwa au nikukosa maadili?

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Pombe ina utamu wake lakini waliosoma wakaelimika wanadai Kwenye mvinyo Kuna ukweli. Katika miaka ya karibuni maeneo mengi ninayokwenda kupiga pombe nimeshuhudia Jambo ambalo zamani sikulizoe. Kuna wimbi kubwa sana la viongozi wa vyombo vya kijeshi walevi au wanywaji. Katika miji mikubwa niliyokaa ikiwemo Dsm, Dodoma, Arusha, Morogoro nk nimebaini watu Hawa pamoja na kuwa wanywaji au walevi vifua vyao au makoromeo hayana uwezo wa kutunza Siri.

Pili wengi wao wanapenda sana kujiweka karibu na wahudumu na wadada wanaojiuza bar au wadada walio Iddle may kwa stress. Baadhi ya viongozi hawa tumekuwa tukiwashuhudia Kwenye vyombo vya habari wakieleza mambo ya Polisi, Uhamiaji, Magereza, Zimamoto, Madawa nk.

Tatizo langu Mimi hapa siyo kulewa au kunywa, tatizo langu lipo kwenye maeneo yafuatayo;
1. Wanapokuwa bar lazima wajitambulishe Kwa vyeo vyao?

2. Wanapokuwa maeneo ya starehe lazima wapigiwe saluti au kuitwa Afande na kila anajiunga kwenye meza zao?

3. Kimaadili, ni sahihi viongozi hawa kunywa kwenye kila bar au wanatakiwa kunywa kwenye bar zenye hadhi flani na wajitenge?

4. Endapo wanaruhusiwa kujamiana na raia, ni Nani anaweza kulinda pombe zilizomo vichwani mwao zisiathiri mafili ya serikali yaliyopo vichwani mwao ambayo sisi raia hatupaswi kuyajua?

5. Ni sahihi Kwa viongozi Hawa kukaa katika ya Wananchi bar Hulu wanajadili matatizo sijui ya Wal chini Yao, sijui mafuta ya doria, sijui kukosoa utendaji wa serikali, matisho na mambo mengi yanayofanyika ofisoni? Kwanini wasikatazwe kuzungumza namna wanavyotuweka mahabusu tukilewa( kwanini wasikatazwe kujadili hoja za ofisi bar?)

6. Hawa watu wengine simu wanabebewa na walinzi wao au wanabeba wenyewe, kwanini wapokee simu Kwa sauti kubwa Hadi wavuruge utulivu wetu wapiga gambe?

7. Hakuna utaratibu wa kujitenga na jamii unapotaka kupokea simu ya kikazi? Nakumbuka nikiwa Dodoma Kuna mzee mmoja alilewa akaelekeza askari sijui waandikwe maelezo akiwa bar kila mtu anasikia anavyofoka...au ndo huwa wanajifanyisha kututega tuwaogope tusiwaombe bia?

8. Inakuwaje kiaongozi wa manjagu ampe barmed simu yake smartphone akae nayo, inakuwaje njagu anaruhusu mapenzi na wivu kwenye simu anayotumia kazini SI wadada watafungua nakujionea charting za magroup Yao wanayojadili mambo ya KAZI? Baby huyo uliyekwenda kuongea naye huko mbali ni nani naomba kama unanijali nione asiwe demu wako.

9 Kwanini Hawa watu wasiache smartphone home, wakajiwekea meza Yao mbali japo wengine bila kuwa na jimama awawezi kusikia ladha la pombe, wakaacha masaluti na uafande huko, wakaenda bar na gari za kiraia na wakaacha kabisa kujadili mambo ya KAZI kwenye sehemu za starehe?

Kwa kweli kwangu Mimi hata Kama ndo wanakuwa wanajilinda wasibuguuziwe Ila naona inakuwa kero ,inatia aibu hasa unapokabidhi simu kwa mwanamke umemkuta bar, unavyofokea watu kisa wewe una walinzi. Lakini pia nakereka sana mtu nakunywa bia yangu anaanza kubwatuka unajua Mimi Nani?

Mbona Askari wadogo hawafanyi haya mambo? Mbona wao ukiwakuta bar awaitani Afande? Rekebisheni au tengenezeni bar zenu tuacheni tulipe Kodi Kwa Raha zetu
 
Mimi huwa napiga askari hasa wa police MAKOFI NA MANGUMI bar. .... Yaani mimi nawapiga sana bar na nawajeruhi mno na hawana cha kunifanya. NILIPIGA WAWILI HADI IJUMAA ILIYOPITA HADI LEO WANANITAFUTIA KISA HAWANA CHA KUNIFANYA.... nasubiri tena weekend nikawapasue tena halafu wawe na adabu.
 
Mimi huwa napiga askari hasa wa police MAKOFI NA MANGUMI bar. .... Yaani mimi nawapiga sana bar na nawajeruhi mno na hawana cha kunifanya. NILIPIGA WAWILI HADI IJUMAA ILIYOPITA HADI LEO WANANITAFUTIA KISA HAWANA CHA KUNIFANYA.... nasubiri tena weekend nikawapasue tena halafu wawe na adabu.
Dawa yako inachemka sababu kuna mmoja ulichukua na simu yake na taarifa zilizopo huwa unatembea na kisu bar sasa unyang'anyi wa kutumia silaha unakuhusu pamoja na kichapo cha mbwa koko lazima utembelee magoti halafu unajisifu kuwa mjanja.
 
Polisi ninaowajua kwanza hawapendi kukaa bar wanazojulikana.
Na wala hawajitambulishi.
 
Dawa yako inachemka sababu kuna mmoja ulichukua na simu yake na taarifa zilizopo huwa unatembea na kisu bar sasa unyang'anyi wa kutumia silaha unakuhusu pamoja na kichapo cha mbwa koko lazima utembelee magoti halafu unajisifu kuwa mjanja.
Hahaha..... dawa yenu ni bar tu.... mkishavua zile sare, hela hamna halafu mnakunywa pombe za bure na kujikuta wajaanja...... UKISHAVUA SARE KUWA MPOLE MAANA HAMNGA KITU NYIE.

Huwa nawasambazia kichapo heavy. WEWE TAPATAPA TU LAKINI UKIJA KUNYWA BIA ZANGU HALFU UNILETEE MDOMO UTAJUA HUJUI...... Hiyo ya kisu na simu ni yako hiyo, mimi siyo wa hivyo. PIA UKIJICHANGANYA UTAJUA HUJUI.
 
Back
Top Bottom