Ni sahihi kulea mtoto wa Kambo?

Ni sahihi kulea mtoto wa Kambo?

Habar Wana JF!

Kuna Binti mmoja nimemuoa zaidi ya mwaka sasa, nimezaa naye mtoto mmoja. Lakini kabla ya hapo alikuwa na mtoto mwingine mwenye umri wa miaka mitano, na makubaliano yetu ilikuwa mtoto huyo aende akaishi na baba yake tutakapo oana, na yeye akaafiki na kweli baba mtoto alimchukua akawa anaishi naye, na baba wa huyo mtoto kaoa ana mke ana watoto wengine.

Sasa siku zimekatika majuzi huyu mke wangu kaenda kumsalimia mtoto wake Kwa baba yake , karudi ananiambia huyo mtoto wake anateseka sana huko, kakonda, hasomi nk, Kwa hyo anataka amchukue Kwa baba yake tuwe tunakaa naye sisi.

Naomba ushauri wenu wadau, itakuwa ni SAHIHI mimi kumlea mtoto wa KAMBO na baba yake yupo?.

Na kama mnavyojua changamoto za mtoto wa KAMBO sitakuwa na uhuru wakutosha kumlea ninavyotaka coz sio damu yangu. Hii imekaaje wadau?
Ulipooa single mother uliomba ushauri? Hao ni kwa matumizi ya dharula tu kuondolea kutu.
 
Mlee kwa upendo mkubwa sana. Kwa sababu kesho na kesho kutwa utazaa watoto wengine na mkeo na hao watoto watakuwa ndugu yao. Yule mtoto kweli anaweza kuwa anateseka na mama wa kambo asihangaike na malezi ya mtoto kwa kigezo kuwa mbona mama yake yupo kwa nini nihangaike. Mtoto atakuwa hana pa kukimbilia akikua ndo anaanza chuki na ndugu zake kuwa wao wamepata malezi ya baba na mama lkn mimi wazazi waliniacha. Japo si mama wote wa kambo ni wabaya. Simama kama baba
Watoto huwa wanaangalia upendo wa wale wanaowalea. Mtoto wa miaka 5 bado mdogo anahitaji sana upendo wa mama.
 
Back
Top Bottom