Kama hawakabidhi madaraka kwa hiari,watafanya kwa lazima!
Hakuna mtu wa kufanya hivo, hizo ni ndoto za mchana, ambazo kimsingi si nzuri, usiwe kama mjinga na usijiweke kwenye kundi la nyumbu, kwa kuwa hamtaki kusumbua vichwa vyenu ndo maana mnapata shida kuelewa haya mambo.
Kimsingi haitakiwi kutumia nguvu kama unavofikiri ww, na kwa kuwa hatuna wapinzani wa kweli kwa maana wengi wao ni wapiga dili2, ccm ingeweza kuondoka hata bila vurugu, kama haya yangefanyika mapema.
Walitakiwa kuwekeza kwa nguvu zote kwenye ubunge na udiwani, wametumia vipindi vinne bila mafanikio, lakini leo hii tungekuwa tunachuana kwa wabunge na madiwa na urais kwa nguvu zote, kwa sababu tungekuwa tumekwisha kufanya maandalizi kwa miaka 20.
Huwezi kutaka urais au kushinda urais wakati huo ulikuwa na wabunge wa kuchaguliwa 27, huo ni wenda wazimu mkubwa, huwezi kusema unataka mabadiliko kwa kuwekeza nguvu kubwa kwenye urais bila kuweka nguvu kwa wabunge na madiwani. ukipata urais bila wabunge ni nini utachokacho kifanya kwenye mambo haya, Katiba mpya, tume huru, kubadili mikataba na mambo mengine mengi, bunge tu ndo lenye uwezo wa kufanya yote hayo na si urais, ndo maana ccm itaendelea kuwa madarakani hadi hapo tutakapoamua kufanya mambo ya msingi kwanza. wapinzani wengi ni walaghai tu na hawapendi kutoa elimu kwa wanachama wao, ndo maana inafikia mahala Mbowe anatamani kuvunja sheria za tume na kuwalazimisha vijana kulinda kura wakati huo mawakala wapo ndani ya vyumba vya kupigia kura-huo ndo umburla wenyewe.