Ni Rais gani aliyepita Tanzania aliyewahi kufanya sherehe ya kutimiza mwaka mmoja madarakani

Kitu kikubwa kinachonipa hofu watu wanasifia mpaka wanapitiliza Yani kasoro hazisemwi ni sifaaa sifaaaa sifaaa mpaka basi,Kama mama asipokuwa makini na kukumbuka alipotoka atafeli Sana.
Hao ni chawa walimpotosha magu akavimbiwa
 

Hayupo

Tulianza na J.K. Nyerere, hakuwahi kufanya hivi!

Akaja, A.H. Mwinyi hakuna kumbukumbu ya kufanya kitu hiki!.

Akaja B.W. Mkopa, hakuna kumbukumbu ya kufanya kitu hiki!

Akaja Msogaboy J.M. Kikwete, hakuna kumbukumbu ya kufanya kitu hiki!

Yaani hata mbabe, mpenda sifa J.P. Magufuli hakufanya kitu hiki!!

LABDA NDIYO ULE USEMI WA; "...Kila zama na kitabu chake". Yaani huyu mama naye anataka aandike kumbukumbu zake!

Lakini mimi naona anakabiliwa zaidi na tatizo la "insecurity" kunakopelekea akose kujiamini kiasi cha kutafuta extra ingredients anazodhani zitampa ukamilifu wa uhalali wake

Hili ndilo tatizo lililomkabili Bwana John Pombe Magufuli kiasi cha kuanza kutumia mamlaka yake vibaya kwa kufanya mambo ya kijinga na kipumbavu just kutafuta recognition
 
Tanzania Sisi Ni Wapuuzi.

Tanzania Ndio Wa kwanza Tunatumia Hela Nyingi Kusherekea Mwaka Mmoja Wa Kiongozi
Bado tuko Nyuma Sana

umaskini Hauta Tuachaaa Kamweee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…