Ni rahisi kumtangaza mshindi kipropaganda Igunga

Donyongijape

JF-Expert Member
May 28, 2010
1,497
810
Wadau katika pita pita zangu niimekutana na hii makala hapa chini. Naomba muisome kwa makini wale
ambao hawajafanikiwa kuiona. Sitaki kutoa comment yangu mapema ili kutoi-bias.

Imeandikwa na Joseph Lugendo;

WIKI hii ni ya lala salama ya kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga mkoani Tabora, ambazo zinatazamwa na kila Mtanzania, zikihusishwa na ukuaji wa demokrasia au ubomokaji na uimara wa vyama vya siasa au udhaifu wake.

Kimsingi, hakuna chama cha siasa ambacho hakielezi kuwa kitashinda tena kwa kishindo na ushindani ni kati ya CCM; waliokuwa na jimbo hilo, Chadema yenye madiwani wawili kati ya 26 na CUF; kilichoshika nafasi ya pili katika uchaguzi mkuu uliopita nafasi ya mbunge katika jimbo hilo.

Tayari, kuna baadhi ya matukio ya vurugu, yaliyoripotiwa si mazuri, hasa la kijana wa CCM kumwagiwa tindikali usiku, baada ya kumaliza kazi yake ya kubandika mabango ya mgombea wa chama hicho, Dk. Peter Kafumu.

Pia, kumetokea vurugu mbaya, ambapo Mkuu wa Wilaya, Fatma Kimario, alidhibitiwa na wafuasi wa Chadema, tukio ambalo kwa maadili tu ya Kitanzania pamoja na kuwa mahakamani ni la udhalilishaji.

Aidha, kumetokea matukio ya kukatana mapanga, ubakaji na hata uchomaji nyumba moto, ambayo waathirika ni wanachama na viongozi wa CCM huku vyama vya siasa, hasa CCM wakituhumu Chadema kwa kuhusika nayo.

Ukiacha matukio hayo, mengine kama ya kuonekana kwa polisi wengi, wakisindikiza magari ya wagombea, kuwepo kwa gari la maji ya kuwasha, ambalo tangu niingie hapa Igunga wiki tatu zilizopita, sijaona likitoka nje ya kituo cha Polisi lilikopakiwa ni mambo ya kawaida ya kuimarisha ulinzi na usalama wa wananchi.

Ni muhimu ulinzi kuimarishwa, kwa kuwa uchaguzi huu, una umuhimu mkubwa katika demokrasia ya vyama vingi, hasa hivyo vitatu vilivyokamiana, kwa kuwa ndio uchaguzi wa kwanza mdogo mara baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana na katika kila chama na hasa hivyo vitatu, una umuhimu mkubwa kwa namna tofauti.

CCM ambao ndio watetezi wa jimbo hilo, kwa nafasi yao tu wanayo kila sababu ya kufanya kila linalowezekana kurudisha jimbo hilo. Chadema kinavizia kuongeza viti vyake bungeni, lakini CUF ni zaidi ya kuongeza viti bungeni, bali pia kina kazi nzito ya kujenga ushawishi katika siasa za Tanzania Bara.

Kwa hiyo haishangazi vyama hivyo vya siasa, kutumia nguvu kubwa ya kitaifa, kifedha, kipropaganda na kimkakati kusaka ushindi na nguvu hizo na pia haina ubishi, kuwa nguvu hizo zitaongezeka maradufu wiki hii, kwa kuwa ndio siku za lala salama.

Ni vyema pia Watanzania, wajue kuwa vyama hivyo vitatu katika nguvu ya fedha Igunga karibu viko sawa, kwa maana uwezo wa kutumia fedha na vyote vinachoma ruzuku, ambayo ni kodi ya wananchi.

Kwa hali ilivyo sasa, vyama hivyo vinashindana kupeperusha bendera, vinashindana kupitisha magari ya kifahari aina ya mashangingi, kusambaza picha za wagombea.

Ingawa kifedha kwa maana ya ruzuku, CCM wana uwezo mkubwa, lakini katika siasa za Igunga, chama tawala, Chadema na CUF wanaweza kukaribiana kwa matumizi ya fedha pamoja na kuwa hakuna kinachoweza kuweka wazi.

Kwa sasa matumizi ya fedha hizo, yanaweza kupimwa kwa idadi ya magari, ambayo ni wazi si ya wagombea wa Igunga, ambayo kwa Chadema, CUF na CCM karibu yanalingana; idadi ya nyumba za wageni zilizokodiwa kwa matumizi ya vyama; wageni hasa wabunge walioweka kambi kama vile kuna mkutano wa Bunge, kumbe kampeni.

Karibu vyama vyote, vimehamishia ofisi zao za kitaifa Igunga, kwa maana karibu watendaji wote wa ngazi za kitaifa, wako Igunga na hivi karibuni katika matumizi ya fedha; CUF waliituhumu Chadema kwa kuwapiga bao katika ukodishaji bajaj, CUF walitangulia kuweka makubaliano, Chadema wakapanda dau, CUF ikakosa bajaj za hamasa. Je mwisho wa safari hii, ambayo inakaribia ukingoni, ni nani atacheka na nani atanuna?

Katika nchi zilizoendelea katika demokrasia, maendeleo yao yanaonekana hata katika miundombinu ya kisiasa, kiuchumi na kijamii na Igunga ingekuwa huko, kwa hatua ya wiki hizi tatu za mwanzo za kampeni; ingekuwa rahisi kutabiri nani mshindi kati ya vyama hivyo hasimu.

Miundombinu hiyo ingeonekana wazi, ingewezesha kura za maoni kutoka kwa wananchi wa Igunga na sio Watanzania wote kwa umahiri wao wa kusoma na kutoa maoni katika mitandao, ingewezesha kura zilizokwishaamua, kuonekana na kura ambazo hazijaamua kujulikana.

Lakini, kwa hali ya Igunga kama ni kujaribu kutumia miundombinu inayoendana na hali ya maendeleo ya demokrasia ya Tanzania, basi CCM peke yao wenye mfumo mkongwe wenye uongozi wa nyumba kumi, ndio wanaoweza kutabiri kura zao, zilizokwishaamua na kuweka mkakati wa kura ambazo hazijaamua.

Vyama vingine kama vina miundombinu, vitatambia mafanikio ya uchaguzi uliopita tu, ambayo hata hivyo, CCM iliongoza na Chadema na CUF vikafuata, kwa maana ya Chadema kuwa wa pili katika kura za urais na udiwani kwa kupata kata moja ; na CUF wapili katika kura za ubunge.

Hata hivyo, ushindi wa CCM hauwezi kuipa kiburi, kwa kuwa mshindi katika uchaguzi uliopita, Rostam Aziz, ambaye bado ana nguvu kama mtu binafsi katika jimbo hilo, pamoja na nguvu zake, alipata chini ya asilimia 15 ya kura zote zilizotarajiwa kupigwa.

Katika uchaguzi uliopita, kura zilizotakiwa kupigwa ni 171,077 na Rostam alipata kura 35, 670 tu na kuwa mshindi, wakati Leopold Mahona wa CUF, aliambulia kura 11, 321 na kuwa wa pili. Kwa hiyo kuna kura 124,086 hazijulikani ziliko.

CUF wanatamba kuongeza kura zao, kwa kuwa wao pekee ndio waliosimamisha mgombea aliyekuwa wa pili katika uchaguzi uliopita, lakini hawaangalii ukweli kuwa pamoja na kuwa wa pili, hawakupata diwani hata mmoja. CCM ilishinda kata 25 na Chadema iliambulia kata moja ya Igunga Mjini, ambayo ikijumlishwa na nafasi moja ya viti maalumu, wanakuwa na viti viwili vya udiwani.

Hali hiyo, ilitokana na kutojitokeza kwa wananchi wengi katika uchaguzi uliopita, ama kwa kupuuza, au kutokana na mazingira ya jimbo lenyewe lina wafugaji wengi wa kizamani, ambao wakiamka wao na ng'ombe zao porini, hawana muda wa kupiga kura au mwamko mdogo wa ukomavu wa kisiasa.

Hata hivyo, Msimamizi wa Uchaguzi, Protas Magayane, anasema kuna tatizo la elimu, kwa kuwa wananchi wengi baada ya kupiga kura za maoni na kumchagua Rostam, waliona kuwa ndio wamemaliza na hivyo katika uchaguzi mkuu hawakwenda.

Lakini, kwa sasa CCM ilichagua mgombea wake kupitia kura za maoni za Mkutano Mkuu wa Wilaya na kama mtazamo wa Msimamizi wa uchaguzi ni sahihi, kura zitaongezeka lakini kimtazamo, kama zilikuwa kura za maoni za CCM, huenda zikawa kura za mgombea wa CCM.

Wako wanaojivunia mikutano mikubwa ya hadhara. Kwa ujinga wanaitafsiri ndiyo ishara ya kura watakazopata. Lakini, kwa vyama vyote, si tu kila mahali wamepata ushirikiano, tena bora CCM wana ushirikiano wa wanachama wao.

Lakini sehemu nyingine, vyama hivyo vimeambulia patupu, watoto tu ndio walikuwa wakiwashangaa. CCM ina mfumo wa wajumbe wa nyumba kumi, lakini vyama vya upinzani havina mfumo huo. Hali hiyo imesababisha baadhi ya vyama hivyo vya upinzani hasa Chadema, kutumia wasomi wa vyuo vikuu kufanya sampuli ya wapigakura, kupima upepo.

CCM wanaweza kutumia mabalozi wao na tayari baadhi wamekutwa wakiorodhesha wapiga kura wao, wanadaiwa kununua shahada. Lakini ukweli ni kwamba wanakusanya idadi ya kura zao zilizoamua ili wajue hali halisi.

CCM, Chadema na CUF wameweka mbunge katika kila kata, wanafanya kampeni za papo kwa hapo, kampeni za mwendelezo; sehemu moja inaweza kurudiwa na chama zaidi ya mara tatu, kuhakikisha tu hakuna mtu aliyeharibu au aliyebadili msimamo wa wananchi.

Kuna ushahidi pia wa vyama hasa CCM na Chadema, kutumia mamluki kuchunguzana. Wapo wanaotumwa katika mikutano ya hadhara, kusikiliza sera na kuwasilisha taarifa katika vyama ili makada waende kusafisha hali ya hewa; wenyewe karibu kila chama wanaita ‘kufukia mashimo’.

Wapo wengine wakiwemo waandishi, wanatumwa katika mikutano hasa ya CCM na Chadema. Kazi yao kuuliza maswali ya kuudhi na kupeleka taarifa kwa makada wa vyama vilivyowatuma haraka iwezekanavyo.

Kwa hiyo akipita kada katika eneo moja, atakachosema kinapelekwa moja kwa moja kwa chama pinzani, na wao wanatuma kada kuja ‘kufukia mashimo’. Kila chama, kati ya hivyo vitatu, Chadema, CCM na CUF, vinatangaza kushinda, havitaki wapigapicha wa magazeti na televisheni, kutoa picha za mikutano ambayo hawakupata watu.

Ndiyo maana nimesema tangu mwanzo kuwa CCM, Chadema na CUF, vimekamia katika ushindi propaganda. Havijui vitapata nini katika uchaguzi huu. Kwa hali ilivyo, mshindi akitangazwa tu, kutakuwa na madai ya kupinga ushindi huku magari aina ya mashangingi, yatatoweka Igunga na kurejea yalikotoka.

SOURCE: HabariLeo | Ni rahisi kumtangaza mshindi kipropaganda Igunga
 

TUNTEMEKE

JF-Expert Member
Jun 15, 2009
4,587
575
Mwandishi wa hii makala hajui anachokifanya ni wale makanjanja, chadema ina viti viwili vya udiwani igunga, igunga mjini na kata nyingine ya jinungu, ukiongeza na mmoja wa viti maalum, wanakuwa watatu, mwandishi wa habari unaongea kitu cha uongo kwenye media, hivi hata wahariri kazi zao ni zipi? Huu ni ujinga na upuuzi, huwezi toa kitu bila kuwa na data, wachina wanasema , no reserch no right to speak, sasa anatoa data zisizo za kweli tena anaact kama anajuwa kumbe hajui
shame on you, kama anahitaji hata majina ya wale madiwani sisi tunayo tutampa
wadau katika pita pita zangu niimekutana na hii makala hapa chini. Naomba muisome kwa makini wale
ambao hawajafanikiwa kuiona. Sitaki kutoa comment yangu mapema ili kutoi-bias.

imeandikwa na joseph lugendo;

wiki hii ni ya lala salama ya kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la igunga mkoani tabora, ambazo zinatazamwa na kila mtanzania, zikihusishwa na ukuaji wa demokrasia au ubomokaji na uimara wa vyama vya siasa au udhaifu wake.

Kimsingi, hakuna chama cha siasa ambacho hakielezi kuwa kitashinda tena kwa kishindo na ushindani ni kati ya ccm; waliokuwa na jimbo hilo, chadema yenye madiwani wawili kati ya 26 na cuf; kilichoshika nafasi ya pili katika uchaguzi mkuu uliopita nafasi ya mbunge katika jimbo hilo.

Tayari, kuna baadhi ya matukio ya vurugu, yaliyoripotiwa si mazuri, hasa la kijana wa ccm kumwagiwa tindikali usiku, baada ya kumaliza kazi yake ya kubandika mabango ya mgombea wa chama hicho, dk. Peter kafumu.

Pia, kumetokea vurugu mbaya, ambapo mkuu wa wilaya, fatma kimario, alidhibitiwa na wafuasi wa chadema, tukio ambalo kwa maadili tu ya kitanzania pamoja na kuwa mahakamani ni la udhalilishaji.

Aidha, kumetokea matukio ya kukatana mapanga, ubakaji na hata uchomaji nyumba moto, ambayo waathirika ni wanachama na viongozi wa ccm huku vyama vya siasa, hasa ccm wakituhumu chadema kwa kuhusika nayo.

Ukiacha matukio hayo, mengine kama ya kuonekana kwa polisi wengi, wakisindikiza magari ya wagombea, kuwepo kwa gari la maji ya kuwasha, ambalo tangu niingie hapa igunga wiki tatu zilizopita, sijaona likitoka nje ya kituo cha polisi lilikopakiwa ni mambo ya kawaida ya kuimarisha ulinzi na usalama wa wananchi.

Ni muhimu ulinzi kuimarishwa, kwa kuwa uchaguzi huu, una umuhimu mkubwa katika demokrasia ya vyama vingi, hasa hivyo vitatu vilivyokamiana, kwa kuwa ndio uchaguzi wa kwanza mdogo mara baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana na katika kila chama na hasa hivyo vitatu, una umuhimu mkubwa kwa namna tofauti.

Ccm ambao ndio watetezi wa jimbo hilo, kwa nafasi yao tu wanayo kila sababu ya kufanya kila linalowezekana kurudisha jimbo hilo. Chadema kinavizia kuongeza viti vyake bungeni, lakini cuf ni zaidi ya kuongeza viti bungeni, bali pia kina kazi nzito ya kujenga ushawishi katika siasa za tanzania bara.

Kwa hiyo haishangazi vyama hivyo vya siasa, kutumia nguvu kubwa ya kitaifa, kifedha, kipropaganda na kimkakati kusaka ushindi na nguvu hizo na pia haina ubishi, kuwa nguvu hizo zitaongezeka maradufu wiki hii, kwa kuwa ndio siku za lala salama.

Ni vyema pia watanzania, wajue kuwa vyama hivyo vitatu katika nguvu ya fedha igunga karibu viko sawa, kwa maana uwezo wa kutumia fedha na vyote vinachoma ruzuku, ambayo ni kodi ya wananchi.

Kwa hali ilivyo sasa, vyama hivyo vinashindana kupeperusha bendera, vinashindana kupitisha magari ya kifahari aina ya mashangingi, kusambaza picha za wagombea.

Ingawa kifedha kwa maana ya ruzuku, ccm wana uwezo mkubwa, lakini katika siasa za igunga, chama tawala, chadema na cuf wanaweza kukaribiana kwa matumizi ya fedha pamoja na kuwa hakuna kinachoweza kuweka wazi.

Kwa sasa matumizi ya fedha hizo, yanaweza kupimwa kwa idadi ya magari, ambayo ni wazi si ya wagombea wa igunga, ambayo kwa chadema, cuf na ccm karibu yanalingana; idadi ya nyumba za wageni zilizokodiwa kwa matumizi ya vyama; wageni hasa wabunge walioweka kambi kama vile kuna mkutano wa bunge, kumbe kampeni.

Karibu vyama vyote, vimehamishia ofisi zao za kitaifa igunga, kwa maana karibu watendaji wote wa ngazi za kitaifa, wako igunga na hivi karibuni katika matumizi ya fedha; cuf waliituhumu chadema kwa kuwapiga bao katika ukodishaji bajaj, cuf walitangulia kuweka makubaliano, chadema wakapanda dau, cuf ikakosa bajaj za hamasa. Je mwisho wa safari hii, ambayo inakaribia ukingoni, ni nani atacheka na nani atanuna?

Katika nchi zilizoendelea katika demokrasia, maendeleo yao yanaonekana hata katika miundombinu ya kisiasa, kiuchumi na kijamii na igunga ingekuwa huko, kwa hatua ya wiki hizi tatu za mwanzo za kampeni; ingekuwa rahisi kutabiri nani mshindi kati ya vyama hivyo hasimu.

Miundombinu hiyo ingeonekana wazi, ingewezesha kura za maoni kutoka kwa wananchi wa igunga na sio watanzania wote kwa umahiri wao wa kusoma na kutoa maoni katika mitandao, ingewezesha kura zilizokwishaamua, kuonekana na kura ambazo hazijaamua kujulikana.

Lakini, kwa hali ya igunga kama ni kujaribu kutumia miundombinu inayoendana na hali ya maendeleo ya demokrasia ya tanzania, basi ccm peke yao wenye mfumo mkongwe wenye uongozi wa nyumba kumi, ndio wanaoweza kutabiri kura zao, zilizokwishaamua na kuweka mkakati wa kura ambazo hazijaamua.

Vyama vingine kama vina miundombinu, vitatambia mafanikio ya uchaguzi uliopita tu, ambayo hata hivyo, ccm iliongoza na chadema na cuf vikafuata, kwa maana ya chadema kuwa wa pili katika kura za urais na udiwani kwa kupata kata moja ; na cuf wapili katika kura za ubunge.

Hata hivyo, ushindi wa ccm hauwezi kuipa kiburi, kwa kuwa mshindi katika uchaguzi uliopita, rostam aziz, ambaye bado ana nguvu kama mtu binafsi katika jimbo hilo, pamoja na nguvu zake, alipata chini ya asilimia 15 ya kura zote zilizotarajiwa kupigwa.

Katika uchaguzi uliopita, kura zilizotakiwa kupigwa ni 171,077 na rostam alipata kura 35, 670 tu na kuwa mshindi, wakati leopold mahona wa cuf, aliambulia kura 11, 321 na kuwa wa pili. Kwa hiyo kuna kura 124,086 hazijulikani ziliko.

Cuf wanatamba kuongeza kura zao, kwa kuwa wao pekee ndio waliosimamisha mgombea aliyekuwa wa pili katika uchaguzi uliopita, lakini hawaangalii ukweli kuwa pamoja na kuwa wa pili, hawakupata diwani hata mmoja. Ccm ilishinda kata 25 na chadema iliambulia kata moja ya igunga mjini, ambayo ikijumlishwa na nafasi moja ya viti maalumu, wanakuwa na viti viwili vya udiwani.

Hali hiyo, ilitokana na kutojitokeza kwa wananchi wengi katika uchaguzi uliopita, ama kwa kupuuza, au kutokana na mazingira ya jimbo lenyewe lina wafugaji wengi wa kizamani, ambao wakiamka wao na ng'ombe zao porini, hawana muda wa kupiga kura au mwamko mdogo wa ukomavu wa kisiasa.

Hata hivyo, msimamizi wa uchaguzi, protas magayane, anasema kuna tatizo la elimu, kwa kuwa wananchi wengi baada ya kupiga kura za maoni na kumchagua rostam, waliona kuwa ndio wamemaliza na hivyo katika uchaguzi mkuu hawakwenda.

Lakini, kwa sasa ccm ilichagua mgombea wake kupitia kura za maoni za mkutano mkuu wa wilaya na kama mtazamo wa msimamizi wa uchaguzi ni sahihi, kura zitaongezeka lakini kimtazamo, kama zilikuwa kura za maoni za ccm, huenda zikawa kura za mgombea wa ccm.

Wako wanaojivunia mikutano mikubwa ya hadhara. Kwa ujinga wanaitafsiri ndiyo ishara ya kura watakazopata. Lakini, kwa vyama vyote, si tu kila mahali wamepata ushirikiano, tena bora ccm wana ushirikiano wa wanachama wao.

Lakini sehemu nyingine, vyama hivyo vimeambulia patupu, watoto tu ndio walikuwa wakiwashangaa. Ccm ina mfumo wa wajumbe wa nyumba kumi, lakini vyama vya upinzani havina mfumo huo. Hali hiyo imesababisha baadhi ya vyama hivyo vya upinzani hasa chadema, kutumia wasomi wa vyuo vikuu kufanya sampuli ya wapigakura, kupima upepo.

Ccm wanaweza kutumia mabalozi wao na tayari baadhi wamekutwa wakiorodhesha wapiga kura wao, wanadaiwa kununua shahada. Lakini ukweli ni kwamba wanakusanya idadi ya kura zao zilizoamua ili wajue hali halisi.

Ccm, chadema na cuf wameweka mbunge katika kila kata, wanafanya kampeni za papo kwa hapo, kampeni za mwendelezo; sehemu moja inaweza kurudiwa na chama zaidi ya mara tatu, kuhakikisha tu hakuna mtu aliyeharibu au aliyebadili msimamo wa wananchi.

Kuna ushahidi pia wa vyama hasa ccm na chadema, kutumia mamluki kuchunguzana. Wapo wanaotumwa katika mikutano ya hadhara, kusikiliza sera na kuwasilisha taarifa katika vyama ili makada waende kusafisha hali ya hewa; wenyewe karibu kila chama wanaita ‘kufukia mashimo’.

Wapo wengine wakiwemo waandishi, wanatumwa katika mikutano hasa ya ccm na chadema. Kazi yao kuuliza maswali ya kuudhi na kupeleka taarifa kwa makada wa vyama vilivyowatuma haraka iwezekanavyo.

Kwa hiyo akipita kada katika eneo moja, atakachosema kinapelekwa moja kwa moja kwa chama pinzani, na wao wanatuma kada kuja ‘kufukia mashimo’. Kila chama, kati ya hivyo vitatu, chadema, ccm na cuf, vinatangaza kushinda, havitaki wapigapicha wa magazeti na televisheni, kutoa picha za mikutano ambayo hawakupata watu.

Ndiyo maana nimesema tangu mwanzo kuwa ccm, chadema na cuf, vimekamia katika ushindi propaganda. Havijui vitapata nini katika uchaguzi huu. Kwa hali ilivyo, mshindi akitangazwa tu, kutakuwa na madai ya kupinga ushindi huku magari aina ya mashangingi, yatatoweka igunga na kurejea yalikotoka.

Source: habarileo | ni rahisi kumtangaza mshindi kipropaganda igunga
 

TUKUTUKU

JF-Expert Member
Sep 14, 2010
11,769
4,032
Mwandishi wa hii makala hajui anachokifanya ni wale makanjanja, chadema ina viti viwili vya udiwani igunga, igunga mjini na kata nyingine ya jinungu, ukiongeza na mmoja wa viti maalum, wanakuwa watatu, mwandishi wa habari unaongea kitu cha uongo kwenye media, hivi hata wahariri kazi zao ni zipi? Huu ni ujinga na upuuzi, huwezi toa kitu bila kuwa na data, wachina wanasema , no reserch no right to speak, sasa anatoa data zisizo za kweli tena anaact kama anajuwa kumbe hajui
shame on you, kama anahitaji hata majina ya wale madiwani sisi tunayo tutampa
Safi sana mkuu,umenena!
 

koo

JF-Expert Member
Mar 9, 2011
257
65
Huyu mwandishi licha ya kutoa takwimu zisizo sahii lakini ameoneka kutozingatia sababu nyingi kiasi akaona kama mabalozi nimtaji kwa ccm lakini nimkumbushe tu kwamba wanaokatazi waandishi kupiga picha mikutano isiyo na watu ni ccm kwani chadema wamenyimwa caverage kwa kiasi kikubwa sana katika mikutano yote ambayo kunakuwa na umati mkubwa wa watu tv hazitasubutu kuonyesha lakini ile yenye watu kidogo ndiyo inayopata nafasi yakuonekana hii ninjama ya ccm kuonyesha umma kwamba wako ngoma droo na cdm ili wakichakachua nakushinda kwa kura moja uma uweze kuamini lakini tulio hapa kwenye uwanja wa mapambano tunashuhudia uungwaji mkaono wakiwango cha juu kutoka kwa wanaigunga tbc wanajua hilo na wanapambana sana kuficha watanzania wasilione lakini nahakika hata waibe vipi hazitatosha kuiangusha chadema. chadema imejipanga sio kuiba bari kufanya kampeni zakisomi nikweri mtandao ulioundwa niwakina sana kuliko kutumia mabalozi ambao wanafanya kampeni kimazoea na cdm imeweza kuidhibiti ccm kwasababubu wanaopambana uwanjani niwatu wawili tofauti sana cdm imehakikisha inatoa elimu kwa vijana ili katika mijadala katika makazi ya wananchi mabalozi unakuta wanajiuma nakufoka pasipo kujua nnini kinawaangusha kutumia mabalozi kufanya analysis niukichaa cdm imefanya sahihi kutumia wasomi kwani wameimarisha sana mikakati na kufanikisha kilichokusudiwa ndugu yangu najua wanaotangaza ushindi kiplopaganda ni ccm cdm itakamata jimbo amini nakwambia
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom