Ni njia zipi bora zitumike na mamlaka kwa watanzania katika kutatua matatizo yao

tatum

JF-Expert Member
Jan 16, 2018
5,786
4,490
Kumekuwa na malalamiko kila kona kuhusu namna ambavyo Serikali,Bunge,Mahakama na vyombo na taasisi zingine za kiserikali namna ambavyo zimekuwa zinatatua matatizo ya wananchi hapa Tanzania.

Kila jambo linalofanywa ili kutatua na kuongeza ubora kimaisha kwa wananchi wa nchi yetu watu wanalalamika tu bila hata kutoa michango yao namna ya kufanya iwe nzuri au bora zaidi.

Sasa labda niwaulize wale ambao wanaona hizo mamlaka zilizopewa wajibu wa kuwasaidia wananchi watumie njia gani ili wewe mwananchi wa kawaida uridhike na hizo njia zinazotumika katika kutatua matatizo yanayowazunguka.

Kinyume na hapo kila siku Taifa la Tanzania litakuwa ni la kulalamika tu mpaka mwisho wa dunia.
 
Back
Top Bottom