Ni nini tofauti kati ya Visa na Passport?

Apr 9, 2020
16
16
Ni nini tofauti Kati ya VISA na PASSPORT?

Je, mtu mmoja anaweza kumiliki passport zaidi ya moja?

Je, mtu mmoja anaweza kumiliki Visa zaidi ya moja?

Je, inawezekana mtu mmoja akamiliki passport na visa?
 
Visa ni kibali kinachotolewa Na nchi husika ili uweze kuishi ktk nchi hiyo Kwa shughuli/jambo Fulani.

Mfano kuna visa ya Biashara & Utalii.
Passport

Ni hati/Nyaraka inayomilikiwa Na nchi husika,ambayo inamuwezesha muhusika kusafiri kutoka nchi moja kwenda nyingine.
 
Kwa kuongezea sababu wengine wameshajibu tayari, passport ni haki yako ya msingi kuwa nayo kama mzawa wa nchi husika lakini visa ambayo ni kibali cha kwenda nchi fulani either kibiashara/masomo/ugonjwa/michezo na mengineyo mengi ni uamuzi wa nchi husika unayotaka kwenda waamuue kukupa ama kutokupa na ikiwa hawaakupa vile vile wanatoa sababu gani au zipi zimefanya usipewe visa ya nchi yao uliyokua unakusudia kwenda.
 
"yatakuja ma watu pori kumpoteza" alisikika mlevi mmoja akiropoka!?
 
Visa ni kibali kinachotolewa Na nchi husika ili uweze kuishi ktk nchi hiyo Kwa shughuli/jambo Fulani.

Mfano kuna visa ya Biashara & Utalii.
Passport

Ni hati/Nyaraka inayomilikiwa Na nchi husika,ambayo inamuwezesha muhusika kusafiri kutoka nchi moja kwenda nyingine.
Asante sana kwa ufafanuzi mkuu
 
Kwa kuongezea sababu wengine wameshajibu tayari, passport ni haki yako ya msingi kuwa nayo kama mzawa wa nchi husika lakini visa ambayo ni kibali cha kwenda nchi fulani either kibiashara/masomo/ugonjwa/michezo na mengineyo mengi ni uamuzi wa nchi husika unayotaka kwenda waamuue kukupa ama kutokupa na ikiwa hawaakupa vile vile wanatoa sababu gani au zipi zimefanya usipewe visa ya nchi yao uliyokua unakusudia kwenda.
Kumbe sasa naanza kukuelewa Mkoloni Mjermanai alipata wapi visa ya kuja kutawala Tanganyika? ! tuanzie hapo kwanza!
 
Tanganyika hata haikuwepo kulikuwa na machief,akina mangungo ndo walimpa
Huyu Mangungo wa msovero? wa juzi juzi ilikuwa kwao siyo kwa tanganyika! na tanganyika ilikuwepo sababu wavuvi walikuwa wakiweka matanga kwenye nyika. ndiyo ikawa Piga Matanga kulee nyikani hence wachora ramani walipo uliza how do you call this place? wazaramo wakajibu kule ni kutia Matanga nyikani hence the word Tanganyika!
 
Wajerumani ndo walikuja kuanzisha kitu kinaitwa Tanganyika na serikali. Hapo awali hakukuwa na nchi.
 
Astaghafiluuu! Babu zetu hao walitawala nini mawee! Mkwawa, Milambo, Mkama marumbo, isike weee temea mate chini! somo la Hx ulikimbia wewe!
 
Kwa kuongezea, passport inatolewa na nchi yako, visa inatolewa na nchi unayotaka kwenda.

Kwa mfano wewe ni mtanzania, basi unapaswa kuwa na passport ya tanzania.

Kama unataka kwenda Marekani, basi wakati unafuatilia utaratibu pale ubalozi wa US, wataibandika visa ya Marekani kwenye passport yako.
(Baadhi ya nchi wanagonga muhuri tu na kujaza idadi ya siku utakazo kaa kwenye passport yako)

Kwahiyo passport ni utambulisho wako kama mtanzania huko ugenini, wakati visa ni kibali cha wewe kuingia na kufanya shughuli iliyokupeleka huko ugenini.

NB. Passport inakua na kurasa nyinginyingi, hivyo kila anaposafiri viza huwekwa kwenye ukurasa tofauti, hadi pale passport yako itakapo jaa.
 
Visa ni kibali kinachotolewa Na nchi husika ili uweze kuishi ktk nchi hiyo Kwa shughuli/jambo Fulani.

Mfano kuna visa ya Biashara & Utalii.
Passport

Ni hati/Nyaraka inayomilikiwa Na nchi husika,ambayo inamuwezesha muhusika kusafiri kutoka nchi moja kwenda nyingine.
Passport ni kibali cha kutoka nchini kwako,
Visa ni kibali cha kuingia nchi unayoenda
 
Kwa kuongezea sababu wengine wameshajibu tayari, passport ni haki yako ya msingi kuwa nayo kama mzawa wa nchi husika lakini visa ambayo ni kibali cha kwenda nchi fulani either kibiashara/masomo/ugonjwa/michezo na mengineyo mengi ni uamuzi wa nchi husika unayotaka kwenda waamuue kukupa ama kutokupa na ikiwa hawaakupa vile vile wanatoa sababu gani au zipi zimefanya usipewe visa ya nchi yao uliyokua unakusudia kwenda.
Asante nimejifunza kitu
 
Back
Top Bottom