Ni nini kinaendelea stendi ya mawasiliano

gamaweshi belo

JF-Expert Member
Nov 25, 2012
453
173
Leo nimepita mawasiliano nimeshangazwa na biashara ndogondogo aka machinga zinazoendelea kuzunguka eneo la stendi na ndani biashara zimewekwa hadi kwenye parking za private car na karibu na maeneo ya choo.

Nimeshindwa kuelewa kama ni rasmi au wamevamia maana itakuwa kero sasa hivi watapanga vitu hadi barabarani, barabara itakuwa ndongo na kusababisha msongamano mkubwa wa magari yanayoingia kituoni

Tafadhali mamlaka husika mliangalie hili swala stendi ilikuwa nzuri sana ila sasa inataka kuchafuka maana muda si mrefu biashara zitaanza hadi kwenye sehemu tunazokaa abiria kusubiria magari na pia mtashindwa Ku control usafi wa eneo hilo.

Pili mjenge basi vibanda vizuri na kule nje kuzunguka stendi kama mlivyofanya ndani ya soko ili kuwe na muonekano mzuri na mfanye jitihada kuwadhibiti wafanyabiashara wa ndani kufanya biashara eneo rasmi tu na sio vinginevyo.
 
wananchi wenyewe ndio tunapalilia hii hali. Kama raia wakigoma kununua bidhaa hawatabaki
 
Nyie mnataka watu wakale wapi wakuu..?
Mbona wale vijana pale mawasiliano wamepanga bidhaa zao vizuri tu??
Barabara gani imeathiriwa pale?

Wamejiajiri tu wanatafuta maisha.
 
Acha wajitafutie mkate wa kila siku kwa halali mkuu, ukiwazuia utakumbana nao kitaa kwa roba za mbao hao hao
 
Afu nashangaa mawasiliano wamepakana na viwanja viwili havijajengwa kama ni vya serikali wangejenga soko maana wafanyabiashara waliobaki nje wachache sana
Maana kule nje mvua zikichanganya watapata shida kunatope baya pale
 
Wengi waliondolewa ubungo wakapelekwa kule na mstahiki meya wa kinondoni ili wafanye biashara zao vizuri...lakini nadhani wapo wachache walioingilia maeneo yasiyo rasmi bila kufuata taratibu...
 
Leo nimepita mawasiliano nimeshangazwa na biashara ndogondogo aka machinga zinazoendelea kuzunguka eneo la stendi na ndani biashara zimewekwa hadi kwenye parking za private car na karibu na maeneo ya choo.

Nimeshindwa kuelewa kama ni rasmi au wamevamia maana itakuwa kero sasa hivi watapanga vitu hadi barabarani, barabara itakuwa ndongo na kusababisha msongamano mkubwa wa magari yanayoingia kituoni

Tafadhali mamlaka husika mliangalie hili swala stendi ilikuwa nzuri sana ila sasa inataka kuchafuka maana muda si mrefu biashara zitaanza hadi kwenye sehemu tunazokaa abiria kusubiria magari na pia mtashindwa Ku control usafi wa eneo hilo.

Pili mjenge basi vibanda vizuri na kule nje kuzunguka stendi kama mlivyofanya ndani ya soko ili kuwe na muonekano mzuri na mfanye jitihada kuwadhibiti wafanyabiashara wa ndani kufanya biashara eneo rasmi tu na sio vinginevyo.
Njiani ganii imezuia amamulitokea kale kabar kajiranj NA wape taarifa kuanzia jtatuu wakiuza SAA asbh tunaweka ndan..
 
Nyie mnataka watu wakale wapi wakuu..?
Mbona wale vijana pale mawasiliano wamepanga bidhaa zao vizuri tu??
Barabara gani imeathiriwa pale?

Wamejiajiri tu wanatafuta maisha.
Mkuu hata kama wanatafuta inatakiwa pia kuwe na mpangilio sio kila sehemu biashara tu kama hapo kuna sehemu imetengwa kwa ajili ya kufanya biashara ingetumika hiyo hiyo na sio kuzagaa kila kona ya stendi
 
Back
Top Bottom