Ni nini kinachomuogopesha Magufuli ndani ya chama chake CCM?

isho_boy

JF-Expert Member
Sep 22, 2015
2,145
1,892
Ninavyoona mkulu kuna uoga flani unamtatiza sana kwenye chama chake tokea niijue CCM mpaka nafika hapa sijawai sikia fukuza fukuza kwenye chama cha mapinduzi. Na sababu inayopelekea fukuza fukuza hii ni kutokana na utofauti wa mitazamo ukionekana unaenda kinyume kimtazamo unaonekana msaliti.

Je hii ni haki kweli? Watu kuimba wana imani na lowasa ni jambo ambalo linaonekana lilimuuma sana mkulu. Je kufanya hivi ni kufanya wanachama kuwa waoga na kufata kila kitu mkulu anataka au kweli ndo mabadiliko ya kweli ya chama?

Nasikia kuna uwezekano wa katiba kubadilishwa baadhi ya vipengele ikiwemo Mwenyekiti wa chama awe anapita bila kupingwa unafika uchaguzi wa kumpata mwakilishi wa chama kugombea urais.

Je huu siyo uoga ambao unamtesa mkulu akihisi kuwa ikitokea uchaguzi 2020 anaweza asipite au ni nini maana yake.

Naomba kuwasilisha.
 
Ninavoona mkulu kuna uoga flani unamtatiza sana kwny chama chake tokea niijue ccm mpk nafika apa cjawai sikia fukuza fukuza kwenye chama cha mapinduzi. Na sababu inayopelekea fukuza fukuza hii ni kutokana na utofauti wa mitazamo ukionekana unaenda kinyume kimtazamo unaonekana msaliti je hii ni haki kweli. Watu kuimba wana imani na lowasa ni jambo ambalo linaonekana lilimuuma sana mkulu.....je kufanya ivi ni kufanya wanachama kuwa waoga na kufata kila kitu mkulu anataka au kweli ndo mabadiliko ya kweli ya chama?

Nasikia kuna uwzekano wa katiba kubadilishwa baadhi ya vipengele ikiwemo mwenyekiti wa chama awe anapita bila kupingwa unafika uchaguzi wa kumpata mwakilishi wa chama kugombea urais, je huu cyo uoga ambao unamtesa mkulu akihisi kuwa ikitokea uchaguzi 2020 anaweza asipite au ni nn maana yake...naomba kuwasilisha.
Pitia historia.Seif Sharif Hamad,Mazrui,na wengine wengi wameshafukuzwa CCM.Si mara ya kwanza.
 
Rejea maneno ya Hatai Mwl JKN....1987 alisema "chama kina matatizo mengi na mazito inabidi tuyatafakari na kuyatatua ikiwemo uongozi mbovu wa chama....." sio nukuu rasmi....najaribu kukumbuka mtiririko sasa chama kina watu ambao sio sahihi kwenye chama! Hiki ni chama cha siasa sio chama cha jeshi!!
 
Ccm ilishafanya maamuzi kama haya miaka ya 80.kwa wajuvi wa masuala ya kisiasa wanayajua haya.Fuatilia historia za akina jumbe(alikuwa na wadhifa mkubwa sana ndani ya chama na serikali),fuatilia historia ya maalim seif,mazrui nk. Kwa hiyo yanayotokea leo yalishatokea marakibao huko nyuma lakini pia hata vyama vya upinzani kama chadema rejea historia ya dk kaborou na akina Zito na wenzake
 
Je sababu za ufukuzwaji wa hawa wanachama na uliowataja zinafanana....maana sababu ya ya kuwafukuza hawa inaonekana very weak sana mkuu?
 
Naamini msaliti hana rafiki na ukisha mjua huna haja ya kukaa nae karibu naamini hata chadema walimwita zitto msaliti sidhani kama walikosea au walipatia ila ogopa mtu anaitwa msaliti
Uoga ndo unamsumbua mkulu wetu....anawatia wanachama uoga hata wa kuhoji....maana ukionekana unaenda kinyume na matamko ya mkulu utaitwa msaliti......
 
Tatizo hasa ni kile kivuli cha Lowassa.
Sote tunafahamu kuwa hata uchaguzi urudiwe leo ndani ya CCM au nchi nzima bado Lowassa atamshinda Magufuli.
Na hicho ndicho huenda kinamnyima usingizi Magu.
 
Je sababu za ufukuzwaji wa hawa wanachama na uliowataja zinafanana....maana sababu ya ya kuwafukuza hawa inaonekana very weak sana mkuu?

Siasa ni Mchezo Mchafu!

Nchimbi, Sofia Simba na Adam Kimbisa wote walijitokeza hadharani kupinga Uamuzi wa Kamati kuu July, 11 2015 lakini cha kushangaza kosa lile lile Mmoja kafukuzwa , Mwingine kakaripiwa na Mwingine kasamehewa. Akili Kumkichwa
 
Rejea maneno ya Hatai Mwl JKN....1987 alisema "chama kina matatizo mengi na mazito inabidi tuyatafakari na kuyatatua ikiwemo uongozi mbovu wa chama....." sio nukuu rasmi....najaribu kukumbuka mtiririko sasa chama kina watu ambao sio sahihi kwenye chama! Hiki ni chama cha siasa sio chama cha jeshi!!
Ni mtume LOWASSA.
 
Nimeangalia ile Video Clip ya wajumbe wa NEC waliokuwa wakiimba "Tuna imani na Lowassa" nikamwona na Kasimu Majaliwa(PM) kimtindo naye alikuwa akiimba tuna imani na Lowassa, tena pale kwenye Chorus ndio kabisaaa.

Nawaza tu, ipo siku Magu ataichungulia hiyo Clip vizuri na kuchukua hatua stahiki....
 
Je sababu za ufukuzwaji wa hawa wanachama na uliowataja zinafanana....maana sababu ya ya kuwafukuza hawa inaonekana very weak sana mkuu?
Sababu zinaweza zisiwe na katika siasa si kila sababu, ni mazingira ya wakati huo. Na usaliti hata Mungu alimfukuza Shetani kwa kujaribu kuwa msaliti.

Usaliti hauvumiliwi popote pale.
 
Sababu zinaweza zisiwe na katika siasa si kila sababu, ni mazingira ya wakati huo. Na usaliti hata Mungu alimfukuza Shetani kwa kujaribu kuwa msaliti.

Usaliti hauvumiliwi popote pale.
Tatizo Mm nililonalo mkuu.. Ni usaliti upi maana issue nzm Inaonekana kujikita kwenye wale walioimba tunaimani na lowasa! Kama huo ndo unaitwa usaliti basi kunauwezekano kwa kubaki ma yes man tu.. Na hapo mkulu akipiga hata chafya tu watu wanaufyata.. Kwa mwenendo huu atakuwa anafanya anavyotaka... Tuwe makini jamaani akitoka chamani anarudi kuishughulikia nchi kama sio tayari ashaanza!
 
Huyu mkuu wetu hajiamini......kivuli cha lowasa kinamtesa.....hata leo lowasa akirudi ccm na kgombea anapita bila kupingwa
 
Back
Top Bottom