Mimi nimeleta kile nilicho kisikia kama wewe unaangalia namna ya uandishi hilo halinihusu cha msingi mimi nilitaka kujua zaidi kwa hicho nilichokisikia,,,, na sorry ni kaskazini kati, mimi sio mtaalamu wa ugawaji wa dayosisi.
Hujanielewa.
Hakuna tatizo lolote ktk uandishi wako
Ishu iko kwenye logic & content
Mfano, umetaja kitu kinachoitwa "dayosisi" bila kueleza ni kitu gani kwa maana ya mtu au......
Na kukusaidia tu ni kuwa mimi ni muumini wa dini ya kikristo ktk madhehebu ya kilutheri
Katika dhehebu letu "dayosisi" ni eneo la kiutawala la kanisa linalojumuisha majimbo na sharika na mitaa.
Hapa maana yake ni kuwa ktk structural organization ya kanisa la K.K.K.T unaanza na MTAA na mitaa kadhaa inaunda USHARIKA na sharika kadhaa zinaunda JIMBO na majimbo kadhaa yanaunda DAYOSISI.
Hata hivyo, yapo pia madhehebu mengine ambayo hutumia neno hili "Dayosisi" kumaanisha eneo flani la kiutawala kikanisa. Mfano Anglican, AIC nk
Sasa maswali kwako ni haya;
Katika andiko lako ulimaanisha dayosisi kwa maana eneo la huduma za kikanisa? Kanisa gani hilo kwa sababu ninavyoelewa mimi Arusha na Manyara yako makanisa mengi tu!!
Hii ndiyo ilikuwa point yangu
USHAURI: Siku nyingine ukisikia jambo ambalo hulielewi, achana nalo kwa sababu utalibeba na kukumbana na maswali kama haya na wewe kuishia kujibu, "mimi nilisikia tu!!".
Ni bora sana kuhangaika na unachokielewa!!