Ni nini kimetokea dayosisi ya Kaskazini?

Playboy

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2011
Posts
1,170
Reaction score
945
Sina uhakika kama huu uzi uliwai kuwepo au laaah.Kama mtanzania mpenda kujua nini kinaendelea katika nchi yangu ikiwemo kisiasa, kiutamaduni, kiuchumi na kijamii pia, leo nikiwa Arusha nikakuta story inayohusu dayosisi ya kaskazini ikijumisha majimbo ya Arusha na Manyara kama sijakosea kuwa wanadaiwa na benki ya CRDB KIASI CHA BILIONI 13 NA NUSU

Katika hizo story nikasikia kuwa wasipo timiza hilo deni , mali za dayosisi zitapigwa mnada ikiwemo hospitali ya Selian, na hilo deni nasikia limetokana na watu kufanya ufisadi katika moja ya vitega uchumi vya dayosisi hiyo ya hoteli inaitwa Corridor spring,.

So kutokana nilikuwa na haraka sikuweza kujua kisa kizima, nimeleta hapa kwq wanaojua sakata hili, imekuweje mpaka dayosisi inadaiwa kiasi kikubwa hivyo ni nini kilitokea hasa...nawasilisha
 
Aiseee!!!! ngoja na mimi nikae hapa pembeni nisubiri huenda akatokea mwenye kujua akatujuza zaidi.
 
Kajipange tena na uzi wako acha papara mkuu..
 
Ulichoeleza ni kisa kizima na hukubakisha cha kuongezewa. Labda dayosisi ni kaskazini kati.
 
Arusha ni dayosisi ya kasikazini kati. .hata ivyo hili swala ni la muda mrefu sana na tulishaanza kulipa toka mwaka juz sisi kama waumini
 
Waumini tunalipa, kwetu tumepangiwa laki mbili kila muumini. .
Tatizo siku hizi michango inasuasua kutokana na Ukata wa wananchi. ....Muda uliobaki ni kidogo sana. .........Mungu tuhurumie
 
Poleni sana!
 
Sina uhakika kama huu uzi uliwai kuwepo au laaah.Kama mtanzania mpenda kujua nini kinaendelea katika nchi yangu ikiwemo kisiasa, kiutamaduni, kiuchumi na kijamii pia, leo nikiwa Arusha nikakuta story inayohusu dayosisi ya kaskazini ikijumisha majimbo ya Arusha na Manyara kama sijakosea kuwa wanadaiwa na benki ya CRDB KIASI CHA BILIONI 13 NA NUSU

Katika hizo story nikasikia kuwa wasipo timiza hilo deni , mali za dayosisi zitapigwa mnada ikiwemo hospitali ya Selian, na hilo deni nasikia limetokana na watu kufanya ufisadi katika moja ya vitega uchumi vya dayosisi hiyo ya hoteli inaitwa Corridor spring,.

So kutokana nilikuwa na haraka sikuweza kujua kisa kizima, nimeleta hapa kwq wanaojua sakata hili, imekuweje mpaka dayosisi inadaiwa kiasi kikubwa hivyo ni nini kilito
kea hasa...nawasilisha

Dayosisi mtu au taasisi?

Na kama ni taasisi, basi sema inajihusisha na nini kwa watu gani

Samahani lakini.

Ila ukweli ni kuwa umepost hii kitu kana kwamba umemtumia rafiki yako "private message" huku mkijuana ninyi kwa ninyi mnaongelea nini!!

Kumbuka hii ni "public forum" na unapoanzisha mada, basi iweke ktk namna ambayo kila mtu ataielewa kwa urahisi ili ipate response tarajiwa.

Else, mada yako haiko kamili....jisome tu utaelewa !!
 
Asante kwa taarifa hata Mimi nimewahi sikia MTU akiongea ila nikaona ni issue ndogo
 
Waumini tunalipa, kwetu tumepangiwa laki mbili kila muumini. .
Tatizo siku hizi michango inasuasua kutokana na Ukata wa wananchi. ....Muda uliobaki ni kidogo sana. .........Mungu tuhurumie

Wengine wafisadi,nyie mlipe? Kweli elimu inatakiwa.
 
Dayosisi mtu au taasisi?

Na kama ni taasisi, basi sema inajihusisha na nini kwa watu gani

Samahani lakini.

Ila ukweli ni kuwa umepost hii kitu kana kwamba umemtumia rafiki yako "private message" huku mkijuana ninyi kwa ninyi mnaongelea nini!!

Kumbuka hii ni "public forum" na unapoanzisha mada, basi iweke ktk namna ambayo kila mtu ataielewa kwa urahisi ili ipate response tarajiwa.

Else, mada yako haiko kamili....jisome tu utaelewa !!
Mimi nimeleta kile nilicho kisikia kama wewe unaangalia namna ya uandishi hilo halinihusu cha msingi mimi nilitaka kujua zaidi kwa hicho nilichokisikia,,,, na sorry ni kaskazini kati, mimi sio mtaalamu wa ugawaji wa dayosisi.
 
Back
Top Bottom