Karibu mama yoyo....
Mwanaume hapendi kusaidiwa mke.....ndiyo maana hatusamehi sisi.
Live long Laiboni...(nimekupandisha cheo toka lile jina nililoshindwa litamka...laigunian sijui nimepatia aahahah).
Na kila mwanaune ajitwike kichwani mke wake muda wote bila kuchoka, ili asijemtua au kumuweka pembeni akajikuta anasaidiwa na mwanaume mwingine mkewe kubebwa na kutwikwa kwenye kichwa cha mwanaume mwingine.....
Haya mafikiri yamenijia tuu na nikawa naandika jinsi yanavyotiririka kwenye tafakuri za bi. Kasinde.
Mtwike mkeo kichwani kwako muda wote bila kuchoka maana mwanamke huwa hachoki kukaa kichwani na hupenda na hufurahia kubebwa na mwanaume muda wote....
Baba yeyoo, sina tafsiri yeyote ya niliyoyaongea bali yamenijia tuu hayo maneno nami nimeyaandika bila kuedit.
Yanipasa nikishayatuma nami nirejee kuyasoma naweza pata somo la kujifunza ama laah boresho kwenye Mahaba....
K' Matata.
Aahahahahahahaaa baada ya kurejea kusoma nilichoandika nimejikuta nakumbuka mchezo mmoja tulioufanya tukiwa vijana miaka ileeeee.
Tulikiwa vijana watupu wa kike kwa wa kiume. Tulikuwa eneo la fukwe ya bahari aka beach. Mchezo huo ulitaka kila mwanaume achague mwanamke bila kujua akishakumchagua nini kitafuata...
Baada ya hapo wakaambiwa wanaume wajipange mstari na wanawake waliowachagua wakae nyuma yao.
Muongoza mchezo akasema mchezo ni mbio fupi anayetakiwa kukimbia ni mwanaume ila akimbie huku akiwa amembeba mwanamke aliyemchagua. Atambebaje atajua mwenyewe ( mgongoni, shingoni, mabegani, mbele kama kupakata mtoto, kichwani mithili ya mzigo wa kuni) na wa kwanza hadi wa tatu kumaliza mbio ni washindi. Aahahahahahahaaa kila mwanaume aligeuka kuangalia aina ya mwanamke aliyemchagua na kuna jamaa mmoja alijitoa maana yeye mwembambaa Ila lichagua mwanamke XXXXL na hakutaka kuwa wa mwisho aahahahaa
Ulikuwa mchezo wa kufurahisha wakati ule ila wenye mafunzo, na nilikuja kuuelewa tafsiri yake baadae sanaa maisha yamechanganya niko kwenye 40+ hivii.