Ni Nini Chanzo Cha U-Terrorist? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni Nini Chanzo Cha U-Terrorist?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lusajo, Jan 5, 2009.

 1. Lusajo

  Lusajo JF-Expert Member

  #1
  Jan 5, 2009
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 451
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Naomba kuuliza hili swali? Ni nini chanzo cha U-Terrorist?
  • Kwa nini mambo hayo yanatokea?
  • Kwa nini watu wa West na wanaosapoti mambo ya West ndio Target?
  • Kwa nini inahusishwa na Uislam na wakati waislam wengi tunaishi nao kwa Amani?
  • Kwa nini Mandela alikuwa kwenye Terror watch List?

  Kwa sababu sidhani mtu mwenye akili zake anaweza akaamua kuwa tayari kufa kwa ajili tu hampendi mtu fulani na huyo mtu hajamfanyia kitu chochote. Au mtu anayeweza kuuliza vizuri anaweza kuuliza na yule mwenye majibu mazuri anaweza kuyaweka. Kama kumewahi tokea U-terrorist mahali pengine unaweza ukaweka na kutoa sababu ya kwa nini ilikuwa hivyo?
   
 2. Echolima

  Echolima JF-Expert Member

  #2
  Jan 6, 2009
  Joined: Oct 28, 2007
  Messages: 3,169
  Likes Received: 531
  Trophy Points: 280
  Ninavyosikia sikia unahusishwa na Uislamu sababu kuna eti aya zinazohamasisha watu wajitoe mhanga,tena nasikia kuwa kama mtu akijitoa mhanga basi huko peponi anaandaliwa kupewa zawadi nono mojawapo ni kufutiwa dhambi zake zote harafu anapata free-pass kwenda peponi. hizo ni tetesi mwenye habari za uhakika atupe.
   
 3. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #3
  Jan 6, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Mhh!!!! yangu macho ngoja waje wasoma vitabu
   
 4. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #4
  Jan 6, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Nasikiaga sikiaga kwamba wanaandaliwa na mabikira wakifika tu huko mbinguni wanabandua tu.......
   
 5. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #5
  Jan 6, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  MoD nakuomba Ifute hii post ya huyu jamaa inapindisha mada, kama mtu hujui kitu kaa kimya. No evidence no right to post. Nafikiri sasa waislam watatuona hapa kijiweni tunakuwa hatuna discipline kwenye dini yao. Huyu jamaa ni mwongo au atuwekee hiyo aya hapa.
   
 6. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #6
  Jan 6, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Different labels given to the same individual for the same action, i.e. ‘terrorist’ and ‘patriot’

  Before Mozambique achieved full independence from Portugal; some freedom fighters of Mozambique who did not subscribe to non-violence were labelled as terrorists by the Portuguese government. The same individuals have been lauded by Mozambique and African for the same activities and hailed as ‘patriots’. Thus two different labels have been given to the same people for the same set of actions. One is calling him a terrorist while the other is calling him a patriot.

  Those who believed that Portugal had a right to rule over Mozambique called these people terrorists, while those who were of the view that Mozambique had right to rule Mozambique called them patriots and freedom fighters.

  It is therefore important that before a person is judged, he is given a fair hearing. Both sides of the argument should be heard, the situation should be analyzed, and the reason and the intention of the person should be taken into account, and then the person can be judged accordingly.

  Read this...
  WASHINGTON — Nobel Peace Prize winner and international symbol of freedom Nelson Mandela is flagged on U.S. terrorist watch lists and needs special permission to visit the USA. Secretary of State Condoleezza Rice calls the situation "embarrassing," and some members of Congress vow to fix it.

  The requirement applies to former South African leader Mandela and other members of South Africa's governing African National Congress (ANC), the once-banned anti-Apartheid organization. In the 1970s and '80s, the ANC was officially designated a terrorist group by the country's ruling white minority. Other countries, including the United States, followed suit.

  Because of this, Rice told a Senate committee recently, her department has to issue waivers for ANC members to travel to the USA.

  Read:
  Mandela in CIA Terrorist Book


  Ah ah ah ah... Tuwasubiri wapendwa...! Au wenye kutetea udini bila kutumia Akili...na farsafa zao...! lol!
   
 7. Nyikanavome

  Nyikanavome JF-Expert Member

  #7
  Jan 6, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 448
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Ugaidi ulikuewepo tokea kuanza kwa binadamu kuwepo katika dunia hii na chanzo chake ni dhuluma kutoka kwa mtu kwenda kwa mwingine au kutoka kwa jamii moja kwenda nyingine. Pindi wale waliodhulumiwa wanapoanza kudai haki yao kwa kutumia nguvu baada ya njia za mezani kushindikana ndipo watu wanapoanza kupeana majina ya uterrorist, mkombozi, baba wa taifa, baba wa vita nk. na wengine wanapoansisha orodha za kuwaorodhesha wabaya wao kama magaidi na wale ambao hawana madhara nao kama wenzetu.

  Kuhusu namna ya mapambano inategemea mazingira yaliyopo na kiwango cha resources walichonacho wapambanaji, mfano hebu soma jinsi wajapan walivyofanya kwenye mwaka 1944 ambapo walikuwa wanawatumia kamikaze

  The Kamikaze (神風, Kamikaze? common translation: "divine wind") ( [kamikazɛ] (help·info)) were suicide attacks by military aviators from the Empire of Japan against Allied shipping, in the closing stages of the Pacific campaign of World War II, to destroy as many warships as possible.

  Kamikaze pilots would attempt to intentionally crash their aircraft — often laden with explosives, bombs, torpedoes and full fuel tanks – into Allied ships. The aircraft's normal role was essentially converted to that of a manned missile in a desperate attempt to reap the benefits of greatly increased accuracy and payload over that of a normal bomb. The goal of crippling as many Allied capital ships as possible was considered critical enough to warrant the sacrifice of an aviator and his aircraft.

  These attacks, beginning in October 1944, followed several critical military defeats for Japan. A combination of a decreasing capacity to wage war – along with the loss of experienced pilots – and rapidly declining industrial capacity relative to the United States, as well as the Japanese government's reluctance to surrender, led to the use of kamikaze tactics as Allied forces advanced towards the Japanese home islands.

  Kamikazes were the most common and best-known form of Japanese suicide attack during World War II. They were similar to the "banzai charge" used by Japanese soldiers. In addition, the Japanese military used or made plans for various suicide attacks, including submarines, human torpedoes, speedboats and divers.

  The tradition of suicide instead of defeat and capture and perceived shame was deeply entrenched in the Japanese military culture. For instance, it was one of the main traditions in the Samurai life and the Bushido code, particularly loyalty and honor unto dea
   
 8. S

  Stone Town Senior Member

  #8
  Jan 6, 2009
  Joined: May 28, 2007
  Messages: 108
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Asalamu Alaykum.

  Mimi napenda au nashauri panapotolewa mada kama hizi ambazo zina faida kubwa kwa jamii au wana JF tuwe serious katika kuchangia na isiwe tunafanya mzaha au kuweka fitna ndani yake kwa sababu tuliomo humu ni watu tofauti kwa maana ya dini, rika, jinsia, mila khulka, silka na hata utamaduni lakini kinachotuunganisha ni kuwa sote ni waafrika na ninapenda sana kujinasibisha kama ni mwaafrika ambaye ninauthamini uafrika wangu na utanzania wangu.

  Kwa maana hiyo mada inayoletwa tuijadili kwa kina with ushahidi na napendekeza kama alivyotangulia mwenzangu kusema kwamba iwapo mtu hana la kusema basi ni vyema akasoma then akanyamaza bila ya kuweka comments zake ambazo zinaweza kuleta fitna kwa wasomaji wengine katika mtandao huu ambao sote ni ndugu kama ni waafrika au ni watanzania bila ya kujali hayo niliyotataja juu ambayo zaidi ni dini tofauti na ambazo kila mmoja anapaswa kuheshimu dini ya mwenzake bila ya kuikashifu wala kuitia dosari.

  Mimi ni muislamu lakini pia ninaheshimu sana dini nyengine hasa ukristo kwa sababu ni ndugu zangu ambao wengi wao ni damu moja kwa hapa zanzibar familia nyingi zimechanganya dini na huwezi kufahamu kati ya waislamu na wakristo na suala hili nimekuwa nikilizungumza sana sana katika kueleza namna tofauti za dini mbili hizi ambazo ni kuu hapa kwetu.

  sasa nije katika mada inayouliza 'nini chanzo cha U- terrorist?' kwa hakika sababu kubwa ni kama alivyokishwa eleza mwenzangu hapo juu kwamba inatokana na dhulma kati ya kundi moja dhidi ya jengine.

  terrorist huitwa ni ugaidi lakini hakuna definition hasa ya neno hilo maana kila mmoja anatoa maana yake kuhusiana na neno hillo, na tukiangalia katika historia tutaona kuwa sio waislamu peke yake wanafanya ugaidi au wananasibisha na ugaidi lakini hili la kutumika kwa waislamu limefanywa makusudi kwa lengo la kuchafua dini ya uislamu ingawa wapo watu wanaokamatwa kwa ugaidi lakini mara nyingi hutangazwa kuwa waislamu ndi waliokamatwa na kosa hilo.

  Ikiwa mtu amekamwata kwa kosa hilo basi atakuwa amefanya kosa hilo sio kwa sababu ya dini bali ni udhaifu wake ndio uliopelekea kufanya hivyo kwa sababu dini ya kiislamu ni dini ya amani na pia inaheshimu dini nyengine na haijaelezwa kuwa afanye hujuma dhidi ya dini iliyokuwa sio ya kiislamu.

  na inapaswa mtu anapokamatwa kama amefanya makosa ya aina hiyo basi ashitakiwe kutokana na mtu mwenyewe lakini asinasibishwe na dini kwa sababu hajatumwa na dini yake kufanya hivyo bali ni matakwa yake kwa sababu wapo waliokuwa sio waislamu pia hukamatwa kwa makosa kama hayo na hatusikii kuwa wakitajwa kwa dini zao, sasa hapo ndipo inapotakiwa watu waone kama hizi ni nyama za makusudi lakini bila ya shaka ipo siku watu watafahamu kama kuna hujuma na si kitu chengine.


  thanks
   
 9. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #9
  Jan 6, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Swali la nyongeza...
  Kwa nini chama CUF miaka ya 1994-2001 kilijulikana kama ni chama cha materrorist?
   
 10. Echolima

  Echolima JF-Expert Member

  #10
  Jan 6, 2009
  Joined: Oct 28, 2007
  Messages: 3,169
  Likes Received: 531
  Trophy Points: 280
  Nasikiaga-sikiaga,samahani wakuu kama nilikuwa labda nimevuka mipaka lakini mimi nilitaka tu kujua kama kuna yeyote mwenye aya inayosungumzia hayo.
  Kwa ufafanuzi unaoendelea kutolewa na jamaa INAANZA kueleweka kwangu..
   
 11. mwakatojofu

  mwakatojofu JF-Expert Member

  #11
  Jan 8, 2009
  Joined: Dec 17, 2008
  Messages: 200
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  1. mi naamini mambo haya ya ugaidi yanatokea kwasababu watu hao (magaidi) hawakubaliani na hali ilivyo au mambo yanavyoenda.

  weusi wakati wako kwenye harakat za kupigania uhuru walikuwa wanaitwa magaidi. walikuwa wanaitwa hivyo na wazungu au vibaraka wao. sisi tuliokuwa upande wao tulikuwa tunawaita wapigania uhuru. mara nyingi naamini hatukupenda kuwaita magaidi. marehemu dk. jonas savimbi tulikuwa tunamuita gaidi (sio sisi wote). kwa wengine walikuwa wanamuita shujaa.
  lakini mara nyingine watu humuita gaidi hata wanayemuunga mkono. kwamfano, hata wafuasi wa dk. jonas savimbi wangeweza kukubali kuwa dk. alikuwa anafanya ugaidi kupambana na serikali halali ya angola. na bado wangeweza kumuunga mkono kwa sababu moja au ingine.

  lakini wengine wanakuwa magaidi kwasababu ya kushawishiwa au kufuata mkumbo. inawezekana kabisa miongoni mwa wapiganaji wa savimbi kuna waliojiunga kwa kushawishiwa, kwa nguvu, kufuata mkumbo na nk. lakin wakishakuwa kundi moja wote ni magaidi kwetu. mwingine anaweza kuambiwa ukifanya hiki na kile utakuwa umempendezesha mungu. akilishwa maneno hayo kwa muda wa kutosha anaweza fanya hata ujinga mkubwa kabisa

  2. kuhusu u-west naona hii ipo kati ya uarabu/uislam na umagharibi (ulaya/amerika) ambao naweza sema ni ukristo zaid. tunaambiwa wayahud (wako na wakristo?) na wapalestina (waislam/waarabu?) wanapigana muda mrefu wakigombea ardhi. na tumekuwa tukipata ripoti za matukio ya kujitoa muhanga (vyombo vya habari vingi ninavyosikia vinaita ugaidi). na tumekuwa tunasikia pia kuwa waarabu au waislam wanaona u-west unaporomosha tradition yao.
  kwahiyo naweza sema israel iko karibu zaid na amerika ambayo iko karibu na ulaya. naona ni vita ya ardhi na tradition

  3. kuhusu kuhusishwa na uislam hata mi nashangaa. labda baadae, lakin kwasasa mi nna marafik wengi waislam kuliko wakristo. labda wanatuzuga. au waislam wanaohusishwa na ugaid ni wale wenye siasa kaliiiiiiii ambao kusema kweli mi sijakumbana nao. na kama ni magaid, siombei

  4. kwa upande wao na maslahi yao na definition yao kipind kile alifit kwenye ugaidi
   
 12. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #12
  Jan 8, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Malafyale Lusajo, hakuna kitu kama terrorism katika dunia hii.Hii term terrorist ni a political term ambayo inajaribu kutolitazama kiini cha tatizo lililopo.
  Mtu akimzidi mwenziwe uwezo na nguvu kwa kiasi kikubwa na hapo hapo akamuonea kwa waziwazi bila kumsikiliza, ndipo inapotokea mgomgano mkubwa wa kimtazamo wa ugomvi huo.
  Yule mdogo naye anakuwa hapungukiwi na uwezo wa kuangamiza ingalau sehemu tu ya jamii ya yule mkubwa, na wakati huo huo yule mkubwa pamoja na ukubwa wake anakuwa hana uwezo wa kumdhibiti yule mdogo katika maisha ya kila siku.
  Hii tumeiona katika sehemu nyingi sana.Kenyatta alitofautiana na wakoloni hivyo alikuwa terrorist wa Maumau na baadaye akwa rais.
  Mandela vilevile alikuwa terrorist wa ANC baadaye akawa rais.Moshe Dayan wa Israel alipigana dhidi ya Waingereza naye alikuwa terrorist wa kutupwa!
  Waheshimiwa hawa wanaposema kuna terrorist sanasana wanataka kusema kuna jamaa tunao waonea , wankuja juu, na hatutaki hata kuwa sikiliza ili kuelewa matatizo yao!
   
Loading...