Mungu ni chanzo cha hekima

Mungu ni chanzo cha hekima

Wakusolve

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2020
Posts
549
Reaction score
930
Marko 6:2
Na ilipokuwa sabato, alianza kufundisha katika sinagogi; wengi waliposikia wakashangaa, wakisema, Huyu ameyapata wapi haya? Na, Ni hekima gani hii aliyopewa huyu? Na, Ni nini miujiza hii mikubwa inayotendeka kwa mikono yake?

Mungu ndiye chanzo cha hekima, ukiwa unapita njia za Mungu atakusaidia kukupa hekima kwenye mambo mengi katika maisha yako.

bwana Yesu kristo alipokuwa ana hubiri njili katika mji aliozaliwa nazareti walikuwa wana shangaa hekima yake lakini hekima inatoka kwa Mungu.

Kupitia kumtafuta Mungu kama kusoma mafundisho yake kama bibilia utapata hekima,
bibilia ni sehemu Mungu kajifunua hivyo unaposoma mara kwa mara na maombi

unajenga uhusiano imara na Mungu hii itakusaidia Mungu kuanza kukupa hekima kwenye maisha yako.

Pia Mungu anaweza kukupitisha kwenye changamoto mbalimbali za kimaisha hii itakusaidia kujenga hekima na kutumia kwenye maisha yako.

Yesu kristo alikuwa anafundisha mambo ya ndoa lakini yeye alikuwa ajao(hana mke) lakini kupitia hekima ya Mungu aliweza

sababu ukiwa na Mungu unakuwa na uwezo wa kuelewa mambo mengi atakama wewe haupo kwenye eneo hilo.

Marko 10:2
Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamwuliza, Je! Ni halali mtu kumwacha mkewe? Huku wakimjaribu.

Hekima ya Mungu itakusaidia kufanya vitu kwa usahihi kwenye ndoa utachagua mtu sahihi, kwenye miradi, biashara au kazi utakuwa unafanya kwa usahihi,

hekima ya Mungu inakusaidia kufanya maamuzi kwa usahihi.

ni muhimu kama unafasi ya uongozi kumuomba Mungu hekima,

maana ndio itakayokusaidia kwenye uongozi, sulemani aliomba hekima kwa Mungu kwanza na sio mali sababu hekima ndio utajiri wenyewe,

hekima ndio iliyozalisha utajiri wake kupitia biashara, iliongoza ufalme wake,
bila hekima uwezi kuwa kiongozi bora pia kutunza utajiri na kuendeleza kunaitaji hekima ya Mungu.
 
Back
Top Bottom