Ni nani wa kuitekeleza bajeti ya 2011/2012 ?. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni nani wa kuitekeleza bajeti ya 2011/2012 ?.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nguluvisonzo, Jun 23, 2011.

 1. n

  nguluvisonzo JF-Expert Member

  #1
  Jun 23, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 511
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  [FONT=&quot]Labda Ningeanza kuangalia namna serikali yetu inavyofanya kazi na mfumo mzima wa uongozi ambao tunafikiria utafanya hiyo kazi iliyoainishwa ndani ya bajeti.[/FONT] [FONT=&quot]Uongozi sehemu kubwa ni wakisiasa zaidi na si wa kitaaluma(professionalism is not applicable).[/FONT] [FONT=&quot]Sehemu kubwa ya viongozi wetu wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na Taasisi nyeti wengi wapo kwenye kundi la wanasiasa zaidi kama alivyokuwa NAPE,hivyo maamuzi mengi ni ya kisiasa zaidi kuliko ya kitaalamu kama inavyotakiwa,kundi hili sana lipo kwa ajili ya kuanagalia kesho itakuwaje kwa yeye na familia yake,maamuzi yao hasa kwenye mambo muhimu hayana utafiti na sana utakuta ni kukidhi haja za kisiasa zaidi na si taaluma.Wajibu wao mkubwa ni kusikiliza bwana mkubwa anataka nini,hii huonekana dhahiri katika kipindi cha uchaguzi na ni lazima ashinde uchaguzi,ili na yeye awe na uhakika wa kuendelea kuwepo madarakani huku akitokomeza matumaini ya maendeleo ya Mtanzania,je hawa ndio wa kutekeleza majukumu yaliyomo ndani ya bajeti?[/FONT]
  [FONT=&quot]Kwa mawazo yangu binafsi bajeti haitatekelezeka ziko sababu , mara nyingi mtengeneza bajeti ni mtu mwenye weredi na inatengenezwa kisayansi kutokana na mahitaji ya kisayansi(yaani mahitaji yamefanyiwa utafiti na majibu kupatikana).[/FONT] [FONT=&quot]Utayarishaji wa bajeti mara nyingi huwa yana shindikizo za kisiasa zaidi na si taaluma,maamuzi mengi yapo kisiasa hata wangepewa ushauri namna gani wao wamezoea kuonekana jambo ambalo watawala wanaona watapata credit toka kwa walalahoi,ikishindikana kunakuwapo na porojo na uongo mwingi kupita kiasi ilimradi tukubali wanalotudanganya, hali ikiwa mbaya zaidi wahusika hujificha kwa kalatasi la nailoni wakituchungulia tunavyoumia kwa uongo wao,mfano ni suala la umeme,kina cha maji Kidatu na Mtera kidogo,mvua zikinyesha kwa wingi,matengenezo ya mitambo ya SONGAS,hivi sasa waziri hataki tena kusema juu ya umeme, je hawa ndio watakao tekeleza yaliyomo katika bajeti mpya?[/FONT] [FONT=&quot]Bado hatujaelewa vizuri namna ya kutumia wataalamu tulionao katika fani zao ipasavyo kikubwa ni kuwakatisha tamaa na kuwanyanyasa kisakolijia kwa manufaa ya wachache wanapopingana na mawazo yao ya kisiasa,sikushangaa wakati Prof Sarungi alipokuwa mkuu wa mkoa kuingia chumba cha upasuaji kusaidiana na madaktari wa Tumbi kuokoa maisha ya majeruhi wa ajali,hii ilikuwa dalili ya kuwaonyesha watawala kuwa walikosea Prof alipashwa kubaki Muhimbili akilipwa fedha nyingi kuliko za mbunge ili asitamani kujaribu siasa ambako walimfanya waziri wa ulinzi.Mifano ipo mingi lakini angalia huu wa mwanasheria mkuu kushindikiza spika avunje sheria na hata kushindikiza askari wa bunge atumike kukandamiza sheria ahsante kwa wabunge walisimama kidete sheria ifuatwe,linguine ati wabunge wanataka waonekane kwenye TV,huyu ni mtaalamu wetu,je mikataba vipi?ni aibu sana kwa taifa letu.[/FONT] [FONT=&quot]Sekta ambazo ni muhimu kuangaliwa ni pamoja na Elimu, Madaktari na wanasayansi wengine ambao wanaleta tija katika maendeleo ya taifa letu.[/FONT] [FONT=&quot]Muhimu pia ni kuangalia upya, je viongozi ambao tunategemea kuleta maendeleo kwa kutekeleza yaliyomo katika bajeti 2011/2012 wanao uwezo wa utawala?au kwasababu ni mwanajeshi na wanasiasa basi wataweza tu,hapana kinchotakiwa ni taaluma halisi ya uongozi,kuanzishwa Chuo Cha Uongozi Mzumbe haikuwa bahati mbaya kulikuwa na sababu maalum,kuwapa watanzania elimu ya kungoza maendeleo na si vinginevyo,staili ya leo umeangushwa ubunge basi unawekwa kuwa mkuu wa mkoa au Mkuu wa wilaya hatutafika hata kidogo.[/FONT] [FONT=&quot]Mimi sikuona kama kuna haja ya kuongeza mikoa na wilaya mpya kwangu ni kuongeza matumizi makubwa ya serikali pasipo sababu kwangu ni kuwapa ulaji marafiki na mzigo kubebwa na watanzania walipa kodi kwa ajili ya utawala wa mikoa na wilaya mpya huk serikali kwenye suala la elimu ikianguka kifo cha mende upande wa pili kila leo tukishangili uchumi umekuwa kwa asilimia.... na pato la mwanachi limeongezeka hawaweki data kamili ni ulaghai tu.[/FONT] [FONT=&quot]Hivi sasa serikali kwa namna moja imeridhia matumizi ya fedha za kigeni na kuidharau shilingi yetu,naamini hili lipo kisiasa zaidi kwa nguvu ya matajiri wenye uwezo wa uiamuru serikali juu ya nini wanataka,hakuna kosa kubwa kama hili katika uchumi wetu na tumekwisha chelewa sana juu ya hili,je tutajenga uchumi huku tukisujudia fedha za nje kutumika ndani,mbona Kenya,Botswana na kwingineko sio hivyo?[/FONT] [FONT=&quot]Namshauri kuangalia upya watendaji je wanakidhi haja?maana mawaziri wetu wanalala hovyo bungeni mpaka magazeti sasa yameamua kila siku kuwatoa picha zao angalieni Mwanachi la 21 na 22 juni 2011,je hawa wanasikia kinazungumzwa bungeni au wakiamka wanakwenda tekeleza ndoto zao za mchana?Hawa ndio kila linalo kuja toka upinzani wao ni kupinga,staili hii ya wana CCM bungeni ni hatari kwa taifa letu,maana wahafanyi upembuzi yakinifu na kutoa msimamo juu ya mstakabali wa taifa letu,hii ni kwasababu ya vitisho toka kwenye uongozi.Taifa linaangamia wakulaumiwa ni CCM kwani ndio walipotufikisha leo.[/FONT] [FONT=&quot]Spika wetu mpendwa ameshidwa kabisa kutambua kuwa yeye hatakiwi kufanya kazi ya SIASA mjengoni ni hatari sana alione hili na abadilike ili kuleta uhuru wa bunge kuisimamia serikali katika utendaji asigeuke nay eye kuwa waziri wa kuilinda serikali.[/FONT] [FONT=&quot]Kwa viongozi tulionao sasa mimi siafiki kabisa,kunahitajika mageuzi makubwa ya kiuongozi kuanzia ngazi ya chini mpaka juu,[/FONT] [FONT=&quot] [/FONT] [FONT=&quot]Mwisho nasema unapokuwa muongo usiwe msahaurifu,utaumbuka,mungu ibariki Tanzania na wabariki watu wake.[/FONT]
   
 2. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #2
  Jun 23, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Duh!nimeisoma mbaka nasikia kizunguzungu lakini sijafika mwisho!kesha nitamalizia sehemu iliyobaki!!
   
Loading...