Ni nani mwenye mamlaka ya kuhoji mamlaka ya Mungu?

Say no to actors

JF-Expert Member
Aug 9, 2016
638
1,000
Ndugu wana jamvi,

Kwa hali ya kawaida na isiyokuwa ya kawaida na kwa muumini wa dini yoyote ile anajua hakuna chombo chochote iwe mbinguni ama duniani cha kuhoji mamlaka ya Mungu. Ni jambo la kushangaza dunia na mbingu na tena muujiza mkubwa ambao haujawahi kutokea leo kuona hicho chombo chenye kuwa na uwezo ya kuhoji mamlaka ya Mungu kinaonekana Tanzania.

Labda nieleweke kuwa Mungu ana mamlaka yoyote kwa viumbe wake na hasa mwanadamu. Anayo mamlaka ya kuongea na kiumbe wake pale anapoona inafaa na amemchagua huyo kiumbe kati ya wengine wote, na Mungu amekuwa na kawaida ya kuongea na watu wake aliowachagua kwa kupitia NDOTO au MAONO. Ndugu Godbless Lema (mbunge) amedai kuongea na Mungu juu ya tabia ya Rais na kinachoweza kutokea kama hatojirekebisha.

Kwa upande wangu sipingani na hilo kwani hakuna anayempangia Mungu aongee na nani na kuhusu nini. Sasa cha kustaajabisha huyu mtu anashtakiwa kwa kuwa ameongea na Mungu. Swali: Where did we get the authority of questioning the power of our creator? Je nani atasimama mahakamani kutoa ushahidi ya kwamba Mungu hajaongea na ndugu Lema?

Wadau naomba kujibiwa Haya maswali.
 
dustless

JF-Expert Member
Oct 21, 2016
799
1,000
Me nafikiri atumie tena fursa alionayo kuongea na Mungu ili abadili hukumu aliyopewa na wandamu so long as yeye yuko karibu na Mwenyezi Mungu.

Otherwise, let's not mix up the two.
 
mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
6,950
2,000
Fafanua vizuri kuhusu LEMA kushitakiwa kwa kuwa aliongea na Mungu. Usidhani kuwa kila mmoja anajua undani was suala la LEMA. Hivyo mtoa mada ungetupa kwanza background ya suala zima. Vinginevyo uzi utadoda!
 
Nena

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
2,306
2,000
Me nafikiri atumie tena fursa alionayo kuongea na Mungu ili abadili hukumu aliyopewa na wandamu so long as yeye yuko karibu na Mwenyezi Mungu.

Otherwise, let's not mix up the two.
Mungu anaruhusu, angekuwa haruhusu basi Yuda Escariot asingemsaliti Yesu. Mwanadamu amepewa uhuru wa kuchagua destiny yake. But remember TAKE WHAT YOU WANT AND PAY FOR IT!, SAYS GOD (msemo wa wahispaniola) wa Kiswahili unasema MALIPO HAPA HAPA DUNIANI
 
Say no to actors

JF-Expert Member
Aug 9, 2016
638
1,000
Fafanua vizuri kuhusu LEMA kushitakiwa kwa kuwa aliongea na Mungu. Usidhani kuwa kila mmoja anajua undani was suala la LEMA. Hivyo mtoa mada ungetupa kwanza background ya suala zima. Vinginevyo uzi utadoda!
NDOTO kwa kawaida huwa zina ujumbe na hapa naomba kutofautisha NDOTO na MAONO. Ndoto hutokea mtu awapo usingizini lakini Maono si lazima mtu awe usingizini, pia ndoto hushirikisha akili lakini maono hushirikisha roho na vyote hivi viwili Mungu huwa anavitumia kuongea na watu wake au mtu wake aliyemchagua amtumie kufikisha ujumbe. Hatuwezi kumpangia amchague Magufuli, Lema au Mwigulu yeye ndiye mwenye maamuzi. Na Mungu hana tabia ya mtu wa aina gani amchague kufikisha ujumbe kwa watu wake au kwa watawala kwa hiyo aweza kuchagua mtu dhaifu, mwenye nguvu, mcha Mungu au mtu wa mataifa. Ndo maana tunaona ktk biblia watu wenye wa aina mbalimbali walichaguliwa na Mungu kuwatumi. Mf. Mfalme Daudi, Sauli(Paulo), Muda nk. Hoja ya kwamba je Lema ni nabii au mtume wa Mungu mpaka aongee naye kupitia ndoto au maono juu ya Rais Magufuli na tabia yake? Hapo naweza nikasema si hoja kwa kuwa hata Sauli anaongea na Mungu hakuwa nabii wala mtume na amekuja kuwa mtume baada ya kuongea na Mungu. Je ni kweli Mungu aliongea na Lema kupitia Ndoto au Maono? Kwa hili Mimi na wewe hatuna jibu bali Lena na Mungu ndo wenye majibu na wala jeshi la polisi, mahakama, Gambo na hata hiyo mamlaka ya juu haina jibu kuhusu ukweli wake. Je swali sasa Lema anashtakiwa kwa lipi hasa kuhusu ndoto yake? Je kosa na kufikisha ujumbe aliopewa na Mungu kuhusu tabia ya Magufuri? Je ni kusema uongo kuwa kaongea na Mungu? Au ni nini haswa?
 
swamila

Senior Member
Apr 4, 2015
159
225

Hivi Mungu nyie watu CDM mnamuona niwakuchezea kama mnavyotuchezea wtz kwa kubadikisha gia angani na mpaka zingine ziwani tena ziwa Nyasa. Siamain kama kweli Lema alioteshwa hao make Mungu awezi kuotesha mtu kutabiria mwenzake kifo make yeye ndo mwenye mamlaka tu na uhai wa MTU.Kwahiyo kama ni kweli aliotesha ningetegemea huyo Mungu wake amuoteshe tena siku ya kutoka mahabusu.
 
ELI-91

JF-Expert Member
Aug 24, 2014
3,598
2,000
Kwa bahati mbaya uwepo wa MUNGU unatia mashaka. dini zilizopo ni propaganda tu... watu wameandika vitabu ili ku justify uhalifu wao kama kupora ardhi za nchi za watu eti mungu wao kawaambia, kuua na kutesa wasioamini mungu wao. Yani ni upuuzi tu, lakini kundi kubwa duniani halioni hou mchezo kutokana na uoga wa kuhoji na umbumbumbu
 
Augustino Fanuel Massongo

JF-Expert Member
Dec 23, 2016
1,280
2,000
Ndugu wana jamvi,

Kwa hali ya kawaida na isiyokuwa ya kawaida na kwa muumini wa dini yoyote ile anajua hakuna chombo chochote iwe mbinguni ama duniani cha kuhoji mamlaka ya Mungu. Ni jambo la kushangaza dunia na mbingu na tena muujiza mkubwa ambao haujawahi kutokea leo kuona hicho chombo chenye kuwa na uwezo ya kuhoji mamlaka ya Mungu kinaonekana Tanzania.

Labda nieleweke kuwa Mungu ana mamlaka yoyote kwa viumbe wake na hasa mwanadamu. Anayo mamlaka ya kuongea na kiumbe wake pale anapoona inafaa na amemchagua huyo kiumbe kati ya wengine wote, na Mungu amekuwa na kawaida ya kuongea na watu wake aliowachagua kwa kupitia NDOTO au MAONO. Ndugu Godbless Lema (mbunge) amedai kuongea na Mungu juu ya tabia ya Rais na kinachoweza kutokea kama hatojirekebisha.

Kwa upande wangu sipingani na hilo kwani hakuna anayempangia Mungu aongee na nani na kuhusu nini. Sasa cha kustaajabisha huyu mtu anashtakiwa kwa kuwa ameongea na Mungu. Swali: Where did we get the authority of questioning the power of our creator? Je nani atasimama mahakamani kutoa ushahidi ya kwamba Mungu hajaongea na ndugu Lema?

Wadau naomba kujibiwa Haya maswali.
OK siwezi kusema sana juu ya source ( scriptures)zingine lakini Kibiblia kuhoji unabii au hata uhalali wa nabii mwenyewe ruksa, Biblia inakataza kuwaamini maanbii bila kuwapima kwa neno la Mungu na kuzijaribu roho zinazowaongoza sababu katika siku za mwisho maandiko ya nasema pataibuka manabii wengi waongo watakao watabiria watu maono ya mioyo yao wenyewe huku wakilenga kutimiza matakwa ya nafsi zao. Vile vile nabii kuwekwa kizuizini na hata kuuwawa ni jambo la kawaida sana katika maandiko,hivyo huyu wa kizazi kipya maadamu anaona maono kinyume na watawala he has to pay the cost.
 
LebronWade

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
1,615
2,000
Mambo yote na ya huyo Mungu na huyo Shetani mnaemfikiria na kuwaongelea kila siku ni vitu vya kusadikika tu hamna halisi hata moja...

Wanadamu tunajihangaisha sana,tunagenerate ma-theories kibao ya kusadikika tu no proof whatsoever...huyo mungu hayupo wala huyo shetani hayupo,ni ma-theories tu ambayo ni mufilisi
 
pilipili kichaa

JF-Expert Member
Sep 3, 2013
10,944
2,000
Ktk Biblia takatifu Mungu aliwahi kuongea na watu mbalimbali (manabii) ambao aliwaambia kitakachowapata watawala mbalimbali, wako waliombiwa watapatwa na magonjwa, wataondolewa madarakani kwa vita na hata kuuawa na ilikuwa hivyo.
 
stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
21,593
2,000
Mkuu labda nikupe ushauri mdogo tu kua maswala ya Mungu usiyafanyie masihara hata kidogo!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom