Say no to actors
JF-Expert Member
- Aug 9, 2016
- 637
- 640
Ndugu wana jamvi,
Kwa hali ya kawaida na isiyokuwa ya kawaida na kwa muumini wa dini yoyote ile anajua hakuna chombo chochote iwe mbinguni ama duniani cha kuhoji mamlaka ya Mungu. Ni jambo la kushangaza dunia na mbingu na tena muujiza mkubwa ambao haujawahi kutokea leo kuona hicho chombo chenye kuwa na uwezo ya kuhoji mamlaka ya Mungu kinaonekana Tanzania.
Labda nieleweke kuwa Mungu ana mamlaka yoyote kwa viumbe wake na hasa mwanadamu. Anayo mamlaka ya kuongea na kiumbe wake pale anapoona inafaa na amemchagua huyo kiumbe kati ya wengine wote, na Mungu amekuwa na kawaida ya kuongea na watu wake aliowachagua kwa kupitia NDOTO au MAONO. Ndugu Godbless Lema (mbunge) amedai kuongea na Mungu juu ya tabia ya Rais na kinachoweza kutokea kama hatojirekebisha.
Kwa upande wangu sipingani na hilo kwani hakuna anayempangia Mungu aongee na nani na kuhusu nini. Sasa cha kustaajabisha huyu mtu anashtakiwa kwa kuwa ameongea na Mungu. Swali: Where did we get the authority of questioning the power of our creator? Je nani atasimama mahakamani kutoa ushahidi ya kwamba Mungu hajaongea na ndugu Lema?
Wadau naomba kujibiwa Haya maswali.