Ni nani mtunzi wa wimbo, "Mabepari Walia" na yuko wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni nani mtunzi wa wimbo, "Mabepari Walia" na yuko wapi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Njaare, Mar 28, 2012.

 1. N

  Njaare JF-Expert Member

  #1
  Mar 28, 2012
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 1,075
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Wanajamvi,
  Kwa wale wanaokumbuka vizuri miaka ya sabini na themanini kulikuwa na huu wimbo, Mabepari walia, mabepari walia wakatiwa mirija. Walipotangaziwa, walipotangaziwa azimio la Arusha.
  Wengi walisikitika, wengi walisikitika wakarukwa na akili ....................."

  Naomba kuuliza ni nani mtunzi wa huu wimbo na yuko wapi kwa sasa?

  Je, bado anashangilia kuona mabepari wakilia?

  Je, ipo siku utaimbika tena hadharani?

  Je, Kuna tofauti gani katu ya ubepari na uwekezaji?
   
 2. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #2
  Mar 28, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Napita wakuu
   
 3. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #3
  Mar 28, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  dah, enzi hizo, vijana tunaitumikia nchi kwa imani na ushupavu kabisa.
   
 4. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #4
  Mar 28, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Good question .. I would say!!!Mkuu wewe umeguswa na nini haswa mpaka kurusha uzi huu!!?
   
 5. N

  Njaare JF-Expert Member

  #5
  Mar 28, 2012
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 1,075
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Nilikuwa natafakari jinsi binadamu wanavyogeuka. Huu wimbo uliimbwa sana kwenye mikutano ya CCM. Sasa CCM hao hao ndo wamekuwa mawakala wa ubinafsishaji. Nikawa najiuliza hivi mtunzi haswa wa huu wimbo bado yuko CCM au naye kabadilika?
   
 6. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #6
  Mar 28, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu umenikumbusha mbaaaaali! Umenikumbusha mirija, mabepari, makabaila.

  Wawekezaji = Mabepari tena si mabepari tu bali Mabeberu (NB Ubeberu ni ubepari uliokomaa)
  Makabaila = Kilimo kwanza
   
 7. m

  mwabaluhi JF-Expert Member

  #7
  Mar 28, 2012
  Joined: Oct 16, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Interesting observation
   
 8. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #8
  Mar 28, 2012
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  Huu mwimbo ulisaidia sana kuengeneza group la watu waitwao proletariants(walala hoi). Maana ubepari baada ya kufa watu wengi sana walipoteza kazi baada ya viwanda na mashamba ya bepari kuendeshwa na watu wasiokuwa na hekima ya kazi. Ubepari ndio uwekelezaji, hivyo tunapofatafuta wawekelezaji ina maana tunalilia ubepari urudishiwe heshima yake.

  Kenya hawakumnyang'anya Lonho mali zake na hivyo huyu jamaa kaitangaza chai ya kenya duniani kote na inauzwa mpaka marekani katika maduka ya uthnic store. kweli kufanywa wajinga ni kosa baya sana . tulipokuwa tunaimba wimbo huu pale uwanja wa taifa hatukujua kuwa tunatanga kifo cha soko la ajira ambalo vijana wengi hivi sasa wanhaha kusaka kazi za viwanda na ujanzi.

  Shilika la mwananchi engineerin Company(MECCO) lilikuwa na Bepari. Ona sasa walipokabidhiwa wazarendo, limeishia kutendeneza majeneza tuu na wala kazi za ujenzi haziaminiki tena,. halitoi ajira akabisaaa!
   
 9. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #9
  Mar 29, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Wewe ni muongo wa kutupa. Mimi naishi Marekani, sijawahi kuona chai ya Kenya hapa. Huwa nanunua paketi nikienda Nairobi. Kamwe ubepari hautajenga Tanzania. Utajenge matabaka ya wamiliki na watwana. Ndiko huko tunakoelekea sasa kwa sera za CCM. Huwezi kutengeneza ajira bila viwanda. CCM imeua viwanda vyetu na kuwakabidhi wageni ambao wamevibadilisha kuwa go downs za kuagizia bidhaa za nje ambazo tungeweza kuzalisha wenyewe nchini. Aliyekuita muongo hajakosea kabisa.
   
 10. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #10
  Mar 29, 2012
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Kuna ubaya gani kukiwa na matabaka. Niko Marekani na tabaka langu ni la working class but I have everything I need.
   
 11. k

  kaka miye Senior Member

  #11
  Mar 29, 2012
  Joined: Sep 25, 2011
  Messages: 157
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ameuliza mtunzi wa wimbo na je yupo wapi maana tungejua kuwa kama yupo tuweze kuwasiliana nae na kujua ana hali gani ya maisha je na bado ana msimamo wake uleule aliokuwa nao alipokuwa anaimba wimbo huo
   
 12. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #12
  Mar 29, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Naona Wamarekani mnatupa uzoefu wenu. Wewe uko working class ya huko Marekani na unapata kila kitu; je unaijua working class ya Tanzania? Unajua kuwa haipati mshahara bali inapata maskhara?
   
 13. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #13
  Mar 29, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Zakumi,
  In a developed country tabaka si kitu kibaya sana kwa sababu working class ni kama middle class. Halafu hapa unakuta tabaka la wakulima wanatengeneza pesa kuliko working class. Lakini katika nchi zetu wakulima bado ni mafukara wa kutupwa. Tukifikia hali ambapo wakulima wetu wanaweza kumudu maisha, kusomesha watoto wao katika shule nzuri, kupata matibabu yanayokidhi, hapo tunaweza kusema hakuna ubaya na matabaka. Let Mitt Romney build his elevator for his cars, I do not care because I am living well on my salary.
   
 14. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #14
  Mar 29, 2012
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Kimbunga,

  Baba yangu alianza kazi na mshahara wa shiling 270 akiwa kama working class na alipata mahitaji yake. Na alistaafu akiwa afisa wa ngazi ya kati serikalini mwenye kupokea malaki lakini hakumudu maisha yake. Je ni kitu gani kilichofanya kupungua kwa thamani ya mishahara ya wafanyakazi? Jibu ni poor government policies. Policies zilizotaka kusawazisha, hizo hizo zikapunguza thamani ya mishahara.
   
 15. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #15
  Mar 29, 2012
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Ukitaka kumjengea kila mkulima shule nzuri, zahanati nzuri na huduma zingine nzuri ni lazima uongeze ukubwa wa serikali. Ukubwa huo utaongeza matumizi ya serikali na kufanya serikali kushindwa kutoa huduma nzuri au kulipa mishahara mizuri. Matokeo yake unakuwa na wafanyakazi na wakulima mafukara.

  Hivyo kutokujenga matabaka katika nchi kama Tanzania ni suala gumu. Na kutatuliwa kwake kunahitaji resources za mali na vichwa.
   
 16. S

  Stoudemire JF-Expert Member

  #16
  Mar 29, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 840
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mabepari walikuwa wanalia kipindi cha Nyerere siku hizi wanacheka tu!
   
 17. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #17
  Mar 29, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  siyo moses nnauye?
   
 18. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #18
  Mar 30, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  mkuu una maana kenya kuna ajira za kumwaga eeh! shituka wewe! huwezi kupata eneo la duara bila kuishirikisha pai, shirikisha ubongo wako.
   
 19. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #19
  Mar 30, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Zakumi,
  I would do it without increasing the size of government. Ningepunguza marupurupu wanayojilipa viongozi, kuongeza kodi na kufuta misamaha ya kodi. Can you imagine kampuni kama Vodacom mpaka sasa hawalipi kodi? What the hell is this?
   
 20. Osaka

  Osaka JF-Expert Member

  #20
  Mar 30, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 1,766
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Mmh! Mkuu una kumbukumbu nzuri, ubarikiwe. Mtunzi wa wimbo huo hata mie simjuhi japo nimeimba wimbo huo sana nikiwa primary kwenye miaka ya70s. Kuna mwingine: 'Kaburu matata huyo...
   
Loading...