Grand Master Dulla
JF-Expert Member
- Jul 20, 2012
- 411
- 152
- Thread starter
-
- #41
I see huyu chalii alikuwa ni noma, yeye pamoja na ndugu zake kina Shedadi, Ayat na dada yao alikuwa anaitwa Chola. Kwao mtu aliyekuwa ametulia alikuwa mdogo wao alikuwa anaitwa Ally Tungu. Utemi wa kuchukua mademu kinguvu alikuwa haufanyii disco tu bali hata mitaani, akimtaka demu halafu akatae maisha yake yatakuwa magumu sana hivyo wengi walikuwa wanakubali yaishe.
Alipigwa risasi na dereva wa lori baada ya kusimama mbele ya lori hilo na kulizuia lisiondoke mpaka atake yeye, akamkuta mzee wa kihehe amedata zaidi yake akamuwasha. Kaka yake Ayat alifariki kwenye tukio la ujambazi.
Nakumbuka siku moja disco alikuja akakuta watoto kibao ambao walikuwa na kiingilio pungufu wako nje akawaambia leteni hela mlizonazo nitawaongezea muingie wote. Basi watoto wakampa hela zote baada ya hapo jamaa akazama ndani (na alikuwa halipi kiingilio, muulizeni Papaa Felicia Chaula wa FM academia anamfahamu vizuri).
Wale watoto wakawafuata Polisi wa patrol wakamshitaki. Polisi kuja jamaa akatoka akawaambia kwa ukali kuwa wasimsumbue yuko kwenye starehe zake kama wana shida naye wamfuate kesho, Polisi wakaondoka wamenywea. Dah!
daaaaah huu uzi umenifanya nitoe machozi mana da guy alikua anaishi nyumba ya pili yake kutoka kwetu pale Kitanzini kwa mzee Kalinga,ni watu ambao tulikua kama ndugu.
Duh mkuu wanasema Birds of a Feather..., isije ikawa na wewe ulikuwa unaonea watu kitaa kwa kuwapa kichapo na kuwanyanganya wasichana waodaaaaah huu uzi umenifanya nitoe machozi mana da guy alikua anaishi nyumba ya pili yake kutoka kwetu pale Kitanzini kwa mzee Kalinga,ni watu ambao tulikua kama ndugu.
jina lake halisi ni hilohilo kaka kulnine yahya,dada yake alikuwa anaitwa Chola,
Hayati ndo alikuwa mkubwa,kaka yao mwingine alikuwa anaitwa Shedadi
Nakumbuka enzi hizo watoto wa mtaani na wengine wanatoka mjini kuja kuangalia mazoezi yao
ya ngumi nje ya nyumba yao.
Dar mzee Yahya alihamia tu kaka ila iringa kitanzini ndo walipokulia.
Kulnine ana mtoto mkubwa tu nae anamwili ka wa baba yake anaitwa Ashlafu.
alikua akicheza usikanyage hata kivuli chake..............
Black Madonna vilikuwa ni vikundi vya watoto wa shule za msingi waliokuwa wakikutana huko Dodoma Mlimani chini ya kiongozi wao Edward Ndomba nakumbuka ni marehemu na kifo chake kilitokea katika purukaushani za namna hiyo hiyo kwa mtu kuchomwa na mshale kichwani. Hawa watoto walikuwa ni wale wa Halaiki za Chipukizihaya na nyie wa dodoma njooni na stori za black madonna, sasa
fafanua basi.
na mimi nauliza yule mtemi wa mitaa ya sinza miaka ile ya 2000-2006 alikuwa anaitwa "DAME" kashatoka jela?kuna jamaa aliniambia yupo gereza la segerea akinyea debe.
Mda wote nasoma uzi huu nlikuwa natafta stori za dame.Nafkiri alikuwa noma kuliko hata huyo cool 9 wao.Nliskia yupo jela ila sjui kwa msala gan.Wenye info zaid 2peane jaman
cool 9 alikuwa ni mtu maarufu sana mkoa wa iringa miaka ya 80- 90 nakumbuka kipindi dada zangu wakiwa wanasoma secondary wakiwa wanasafari za disco alikuwa anawasumbua sana ila kunasiku sister alikuwa anatoka iringa hotel kwenye graduation cool 9 akawa anataka kumfanyia fujo sister wacha ale kichapo na bro wangu tangu siku hiyo akawahawasumbui dada zangu. Mob ya kul nine ilikuwa kina chancella, shedad na vijana wengine ila baada ya shedad kufa kidogo utemi ukapungua mkoani kwetu mpaka walipojitokeza kina shetani aliebarikiwa kuanzisha ubabe tena sijui kama kuna mtu wa humu anaemfahamu shetani aliebarikiwa mtemi wa iringa.
Tangu watu waanze kumiliki bastola bila kupitia vikwazo vingi, ubabe wa ngumi haupo tena!