. Naomba kukuuliza mheshimiwa yafuatayo:
i. Kwani Mh. Waziri kaandaa hiyo bajeti peke yake?
ii. Wataalamu wa wizara ya Fedha, BOT, Mashirika ya Fedha nk hawakuhusika?
iii. Je ana muda gani hapo HAZINA hata tumtoe makosa kupitia bajeti aliyokuta imeandaliwa?.
iv. Mwisho usisahau ni mara ya kwanza yeye kusimama Bungeni na kupewa jukumu kubwa kama hili. It is obvious anaweza kuwa ametetereka ktk kuongea na kuwasilisha mada. Hilo lisitufanye tuendelee kumuona hafai.
v. Watanzania wenzangu safari ya ukombozi wa Mtanzania bado ni ndefu hivyo nasisitiza tumpe muda anaweza kuwa Daudi aliyemuua Goliati. Tupunguze negativity kubwa tuliyonayo inayosababisha upofu hata yaliyo mazuri hatuyaoni wala hatutayaona tukiendelea hivi. Tumuombee yeye na viongozi wengine watuongoze vizuri na kwa uadilifu, pia na tuiombee Tanzania yetu, nani ajuae Daudi amepatikana?
Qeen Esther
Utakuwa umesikia hata wabunge wa CCM ambao ni vilaza sana, wamekubaliana na mawazo yangu kuwa anapwaya, ameandaa bajeti kama ya city council, maneno ya mbunge wa CCM.
Ukweli ni kwamba hajaandaa pekee yake lakini ni flag carrier, hakuna upanuzi wa wigo wa walipa kodi, hakuna mipango ya kuongeza kipato ukitoa kuongeza kodi kwa walipakodi waliopo, mfanyakazi kodi bado kubwa sana, ukilipwa mil 3 unalipa kodi mil 1 kila mwezi, je wafanyabiasha wanalipa hiyo kodi? kwa nini mfanyakazi ambaye ni maskini ukilinganisha na wafanyabiashara?? JIBU ni dogo, wabunge hawalipi kodi kwenye mishahara yao, na pia ndo wafanyabiashara wakubwa TZ. Sasa waziri angevunja hilo, wabunge walipe kodi kwa mishahara, na wafanyabiashara kodi iongezeke kama ilivyo kwa mlipwa mshahara.
Je Mgimwa kama yuko fit kichwani, anadhani ni dhambi kunywa soda au bia? mbona nchi inaendeshwa na wanywa bia na soda, kodi kila mwaka inapanda kwenye maeneo hayo, ni kivipi??? Migodi na mikataba mibovu mbona haikuguswa?? Wezi au mafsadi je?, hiyo fedha mbona haipo kwenye bajeti, hii ina maana serikali haitaki kufuatilia watu hawa na kurejesha fedha zetu???
Pamoja na kukubaliana kwa kina na Mhagama kuwa bajeti ni mbovu tena kama ya city council, bado sikubaliani na hoja ya wabunge wa CCM eti pikipiki zisilipe kodi ya mapato, huu ni upumbavu mkubwa. Hakuna mtu ambaye afanye biashara bila kulipa kodi ya mapato, asiwepo ili kujenga uwezo wa kujitegemea, tena kodi yenyewe 90,000/-kwa mwaka!!! mimi napendekeza hata watoto wadogo from 5yrs walipe kodi ya 500/-kwa mwaka ili kuwajengea ufahamu na uzalendo kwa nchi yao. wajue ni wajibu kulipa kodi kwa maendeleo ya nchi yao.
Kwa ufupi bajeti haina matarajio ya watu wenye akili timamu, ni mbaya haina jipya wala haitupeleki kwenye kujitegemea, kukuza uchumi na mengineyo. Japo mabadiliko yamefanyika juzi tu, lakini haimanisha waziri wa fedha aseme pumba harafu tunyamaze vile kaingia juzi, hilo ni kosa kubwa, ingekuwa uwezo wangu vile CCM hakuna watu kwa sasa wenye akili nzuri, ZITO angepewa hiyo wizara na bajeti mbadala yake ingekuwa ndo bajeti ya nchi 2012/13. Tusione aibu, tunajenga nchi.