Ni nani atakayerithi nafasi ya Mwalimu Christopher Mwakasege?

Mwalimu Christopher Mwakasege ni mtumishi wa Mungu wa muda mrefu alijitolea kufundisha neno la Mungu kwa mapana zaidi.

Amejizoelea umaarufu kwa kufundisha neno la Mungu bila kuingiza siasa, kulisema au kusema watumishi wengine na amekuwa akifundisha neno pekee la Mungu.

Je, ni nani atakaye kuja kumrithi mwalimu maana huduma yake itakoma ni suala la muda kutokana na umri.

Wakina Kapola, Mwamposa, Lusekelo wote naona wamekaa kimchongo
Mungu atatuinulia nabii mwingine wa taifa
 
Mwakasege amekaa kipentekoste japo ni mlutheri anayefundisha mafundisho ya kipentekoste. Labda kuna mrithi wa huduma yake atakuwa amemuandaa kama Musa na Haruni, Eliya na Elisha
 
Bwana anaweza muinua mwingine. Ila kuna huyu DANIELY JOSHUAN ni mtumishi mzuri sana sema tu naona bado ana yale maisha ujuu zaidi, kutembea escorts za polisi kama watumishi wengine ambao kwao Injili ni pesa.

Huyu Mtumishi nimemsikiliza na nimesikiliza shuhuda kadhaa kanisani kwake, yupo vizuri sana aiseee. Namwombea kwa Mungu, Mungu ampe neema asiishi kama mitume na mananii wengine waishivyo ambao huitumia injili kwa matumbo yao.
 
Mwalimu Christopher Mwakasege ni mtumishi wa Mungu wa muda mrefu alijitolea kufundisha neno la Mungu kwa mapana zaidi.

Amejizoelea umaarufu kwa kufundisha neno la Mungu bila kuingiza siasa, kulisema au kusema watumishi wengine na amekuwa akifundisha neno pekee la Mungu.

Je, ni nani atakaye kuja kumrithi mwalimu maana huduma yake itakoma ni suala la muda kutokana na umri.

Wakina Kapola, Mwamposa, Lusekelo wote naona wamekaa kimchongo
Mungu aliyemuinua atatupa mwingine.

Kama ambavyo alimuinua mtanguliz wake Musa .
 
Wakina Kapola, Mwamposa, Lusekelo wote naona wamekaa kimchongo,,😂😂😂
 
Mwalimu Christopher Mwakasege ni mtumishi wa Mungu wa muda mrefu alijitolea kufundisha neno la Mungu kwa mapana zaidi.

Amejizoelea umaarufu kwa kufundisha neno la Mungu bila kuingiza siasa, kulisema au kusema watumishi wengine na amekuwa akifundisha neno pekee la Mungu.

Je, ni nani atakaye kuja kumrithi mwalimu maana huduma yake itakoma ni suala la muda kutokana na umri.

Wakina Kapola, Mwamposa, Lusekelo wote naona wamekaa kimchongo
Hata mimi huwa nafikiria sana
Huwa sioni mbadala wa huyu Baba,
Ila amini, Mungu ana vijana wengi wazuri sana, ni vile tu bado watu hawajawajua.
 
Itakuwa ni makosa ya Karne na ubinafsi wa hali ya juu kama ajaandaa mtu wa kurithi nafasi yake. Maana Kila nabii aliicha mtu mnyuma atakayefuata baada ya yeye kumaliza kazi yake. Siamini kama Mwakasege hajaandaa mtu wa kuchukua kijiti baada ya yeye.
 
Ndo changamoto za nchi zetu za kiafrica
 
Hata mimi huwa nafikiria sana
Huwa sioni mbadala wa huyu Baba,
Ila amini, Mungu ana vijana wengi wazuri sana, ni vile tu bado watu hawajawajua.
Angeandaa lakini huduma yake ni kubwa na amejitwalia utukufu mkubwa sana
 
Mwalimu Christopher Mwakasege ni mtumishi wa Mungu wa muda mrefu alijitolea kufundisha neno la Mungu kwa mapana zaidi.

Amejizoelea umaarufu kwa kufundisha neno la Mungu bila kuingiza siasa, kulisema au kusema watumishi wengine na amekuwa akifundisha neno pekee la Mungu.

Je, ni nani atakaye kuja kumrithi mwalimu maana huduma yake itakoma ni suala la muda kutokana na umri.

Wakina Kapola, Mwamposa, Lusekelo wote naona wamekaa kimchongo
hao uliowataja chini nakazia ni matapeli....Ibada nzima imejaa kupokea miujiza
 
Back
Top Bottom