Ni nani atakayemfunga paka kengele?

Mallata Jr.

JF-Expert Member
Feb 24, 2014
365
250
View attachment 205133

Kulikuwa na duka Kuubwa la Vyakula na Vinywaji katika mji. Panya Wengi waliishi katika duka hilo la vyakula na vinywaji. Chakula kilikuwa ni kingi sana kwa ajili yao. Walikula kila kitu na kuharibu mifuko yote ya vyakula. Waliharibu pia mikate, biskuti na matunda ya duka.

Mwenye duka alishikwa na wasiwasi kweli. Hivyo, yeye alipata wazo "mimi lazima ninunue paka na atakaa humu ndani ya hili duka. Kufanya hivo naweza kuokoa mambo yangu."

Alimnunua Paka mmoja mzuri, mkubwa na kisha kumwacha pale. Paka alikuwa na wakati mzuri wa kuwinda panya na kuwaua. Panya hawakuweza kuzunguka kwa uhuru sasa. Waliogopa kwamba wakati wowote paka ange wakamata na kuwala.

Panya walitaka kufanya kitu fulani. Wakaitisha mkutano na wote wakasema "Ni lazima kujikwamua na paka. Je, kuna mtu ana maoni? mwenyekiti aliuliza.
Panya wote wameketi kimya na kuogopa. panya mmoja mwelevu alisimama na akasema, "paka hatembea kwa upole. Hilo ni tatizo. Kama tunaweza kumfunga kengele kwenye shingo yake, basi mambo yatakuwa mazuri. Tunaweza kujua harakati zake zote ".

"Ndiyo, hilo ni jibu sahihi," walisema panya wote. panya wa miaka mingi alisimama polepole na akauliza, "Ni Nani atakaye Mfunga paka kengele? " Baada ya muda mchache hakukuwa na yeyote wa kujibu swali hili.

Swali:
Sasa tuulizane wasomi nini mafundisho ya hadithi hii ambayo kila mmoja wetu aliichukulia ya watoto wa shule ya msingi yaani kuleeeeeeee tuliko pita zamani.Kwa upande wangu inanifundisha ya kwamba UFUMBUZI MTUPU HAUNA THAMANI. Nini mafundisho yake kwa upande wako?
 
Mallata Jr.

JF-Expert Member
Feb 24, 2014
365
250
kazi nzuri wamefanya wabunge lakini swali liko pale pale NI NANI ATAMFUNGA SOSPETER MHONGO KENGELE?
 
linguistics

JF-Expert Member
Jun 22, 2014
4,530
2,000
Kengele zitafungwa kila mahali paka akipita anakuwa anazigusa hivo panya watasikia kila anapopita...teh teh
 
Prosper C Manasse

JF-Expert Member
Dec 8, 2015
636
1,000
Hili Ni Fumbo Na Linahitaji Kujibiwa Kwa Akili Sana.

Kila Mmoja Anaweza Akawa Na Mtazamo Wake Lakn Mtazamo Wa Nani Ni Sahihi?.

Ngoja Nami Nitoe Tafsiri Yangu Hapa, Naamini Sitakuwa Mbali Na Ukweli.

Duka= Nchi (Tz)

Mwenye Duka= Watanzania.

Bidhaa Za Dukani= Lasilimali za Watz.

Panya= Mafisadi.

Baada Ya Watz Kuliwa Sana Tukamweka Magufuli (Paka) Ili Kuzuia Ufisadi.

Panya (Mafisadi) Baada Ya Kuona Paka (Magufuli) Kawaharibia Dili Kwa Kuzuia Kula Lasilimali Za Watz , Wakaa Kikao Kisha Mmoja Wa Mafisadi Akatoa Mbinu Ya Kumfunga Paka (Magufuli) Kengere.

Fisadi (Panya) Mmoja Mzoefu Akauliza, Nani Wa Kumfunga Paka (Magufuli) Kengere.

Nafikiri Nimejaribu Mkuu.
 
Umetisha sana mkuu
 
mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
12,512
2,000
Kwa kuwa paka huwa hana kawaida ya kurudi nyuma panya kwa pamoja wanaweka kamba yenye sehemu ya kipimo sahihi usawa na kichwa wanaanza kumchezea kwa hasira paka hatajirusha usawa na wao na kunasa watavuta kamba mpaka anakufa chezea lgumi weye
 
Brightfame

JF-Expert Member
Sep 14, 2016
1,156
2,000
Hili Ni Fumbo Na Linahitaji Kujibiwa Kwa Akili Sana.

Kila Mmoja Anaweza Akawa Na Mtazamo Wake Lakn Mtazamo Wa Nani Ni Sahihi?.

Ngoja Nami Nitoe Tafsiri Yangu Hapa, Naamini Sitakuwa Mbali Na Ukweli.

Duka= Nchi (Tz)

Mwenye Duka= Watanzania.

Bidhaa Za Dukani= Lasilimali za Watz.

Panya= Mafisadi.

Baada Ya Watz Kuliwa Sana Tukamweka Magufuli (Paka) Ili Kuzuia Ufisadi.

Panya (Mafisadi) Baada Ya Kuona Paka (Magufuli) Kawaharibia Dili Kwa Kuzuia Kula Lasilimali Za Watz , Wakaa Kikao Kisha Mmoja Wa Mafisadi Akatoa Mbinu Ya Kumfunga Paka (Magufuli) Kengere.

Fisadi (Panya) Mmoja Mzoefu Akauliza, Nani Wa Kumfunga Paka (Magufuli) Kengere.

Nafikiri Nimejaribu Mkuu.
There you are, yaekekea somo la fasihi ulilifaulu vizuri.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom