Ni nani atakaye mfunga paka kengele?

Ni nani atakaye mfunga paka kengele?

Mallata Jr.

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2014
Posts
461
Reaction score
392
View attachment 205161

Kulikuwa na duka Kuubwa la Vyakula na Vinywaji katika mji. Panya Wengi waliishi katika duka hilo la vyakula na vinywaji. Chakula kilikuwa ni kingi sana kwa ajili yao. Walikula kila kitu na kuharibu mifuko yote ya vyakula. Waliharibu pia mikate, biskuti na matunda ya duka.

Mwenye duka alishikwa na wasiwasi kweli. Hivyo, yeye alipata wazo "mimi lazima ninunue paka na atakaa humu ndani ya hili duka. Kufanya hivo naweza kuokoa mambo yangu."

Alimnunua Paka mmoja mzuri, mkubwa na kisha kumwacha pale. Paka alikuwa na wakati mzuri wa kuwinda panya na kuwaua. Panya hawakuweza kuzunguka kwa uhuru sasa. Waliogopa kwamba wakati wowote paka ange wakamata na kuwala.

Panya walitaka kufanya kitu fulani. Wakaitisha mkutano na wote wakasema "Ni lazima kujikwamua na paka. Je, kuna mtu ana maoni? mwenyekiti aliuliza.
Panya wote wameketi kimya na kuogopa. panya mmoja mwelevu alisimama na akasema, "paka hatembea kwa upole. Hilo ni tatizo. Kama tunaweza kumfunga kengele kwenye shingo yake, basi mambo yatakuwa mazuri. Tunaweza kujua harakati zake zote ".

"Ndiyo, hilo ni jibu sahihi," walisema panya wote. panya wa miaka mingi alisimama polepole na akauliza, "Ni Nani atakaye Mfunga paka kengele? " Baada ya muda mchache hakukuwa na yeyote wa kujibu swali hili.

Swali
Sasa tuulizane wasomi nini mafundisho ya hadithi hii ambayo kila mmoja wetu aliichukulia ya watoto wa shule ya msingi yaani kuleeeeeeee tuliko pita zamani.Kwa upande wangu inanifundisha ya kwamba UFUMBUZI MTUPU HAUNA THAMANI. Nini mafundisho yake kwa upande wako?
 
Stories: We need to think outside the box. Not to concentrate in one solution which we think is the best and the only one. Kwa kuwa hii ni porojo naomba niijibu kwa hadithi hivyo hivyo: Kuna fictional solutions nyingi tu: WEIGHT SENSORS: Kwa kuwa paka ni mzito kuliko panya (normally), basi tuunge hivyo vi sensor vya uzito katika grids. Paka akikanyaga tu basi inatoa mlio au mwanga. MOTION SENSORS: Paka ni mrefu kuliko panya. Wekeni sensors kufikia urefu fulani ili panya wapite bila shida na paka atrip hiyo alarm. But iwapo tunaongelea uchaguzi na rushwa, solution ni moja tu: KATA MTI NA MIZIZI YAKE. CAN WE?
 
BMPINGO wewe ni Genius
 
Yule mdogo kuliko wote ataifanya kazi hii, von zerewski alikuwa na bunduki kali na akaua wapiganaji wengi wa kihehe kabla ya mtoto wa miak 16, hajajitoa mhanga na kumvamia kwa mkuki huku akiwa na bunduki yake, mtoto huyo ndo alimuua von zerewski na kupewa zawadi ya ng'ombe tatu enzi hizo.
 
Uzalendo siku hizi haupo mkuu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom