Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 118,919
- 221,297
Rais mstaafu wa Tanzania Mh Jakaya Kikwete katika viwanja vya Mnazi Mmoja wakati akihamasisha wananchi kupima Ukimwi kwa hiyari , alisema hivi , nanukuu , " KUJUA TATIZO NI NUSU YA JAWABU " Mwisho wa kunukuu .
Kwa tafsiri yangu maana ya Mh Kikwete kwenye kauli ile ilikuwa kwamba ukishajua kama una Ukimwi basi angalau ungeweza kujitambua na kuchukua hatua za kujiepusha na hatari zaidi pamoja na magonjwa nyemelezi ili uweze kuishi kwa muda mrefu zaidi.
Imekuwa kawaida sasa kwa JAMIIFORUMS kuhujumiwa panapokuwa na Tukio kubwa la kitaifa , Jf ambako kila chama na wapiga debe wao wanatumia kujieleza na kumwaga propaganda zao , inakuwaje ihujumiwe , ni nani anayefanya hivi , kwa manufaa ya nani ?
Sitaki kuamini kama TCRA wenye verified a/c hapa na wanaotumia jf kueleza mambo yao wanahusika , Ni vema sasa wakuu tukamfahamu kwa majina yote matatu anayeihujumu jf ili tujue namna ya kumdhibiti , Jf ni rafiki wa kila mtu wakiwemo viongozi na mawaziri kadhaa , Jf imetumika hata kuokoa maisha ya baadhi ya mawaziri na viongozi , ubaya wake ni nini ?