NI nani anahusika kuandaa kiongozi bora?

Kaitaba

JF-Expert Member
Jun 30, 2009
916
52
Nimefuatilia kwa makini hii sakata ya kutoa waraka (Nyaraka) na taasisi za kidini, na hapo hapo hapo wanasiasa wapinga jambo hilo, matokeo yake malumbano yanaanza.

Hivi kati ya;
1.Taasisi za kidini,
2.Wanasiasa,
3.Wananchi
Ni yupi anastahili kuandaa kiongozi bora?
 
Umesahau taasis muhimu sana katika kuandaa kiongozi, ''Familia"
Yanayofuata ni process na sio jambo la siku moja kuandaa kiongozi
 
Umesahau taasis muhimu sana katika kuandaa kiongozi, ''Familia"
Yanayofuata ni process na sio jambo la siku moja kuandaa kiongozi

Kama ni hivyo, sasa inakuwaje wanasiasa na taasisi za kidini zinashutumiana kwa kuandaa viongozi wa kisiasa?
 
Umesahau taasis muhimu sana katika kuandaa kiongozi, ''Familia"
Yanayofuata ni process na sio jambo la siku moja kuandaa kiongozi

Kama ni hivyo, sasa inakuwaje wanasiasa na taasisi za kidini zinashutumiana kwa kuandaa viongozi wa kisiasa? maana kama anayetakiwa kuandaa kiongozi ni familia, hakuna sababu ya kulumbana, je hao wanaolumbana wanalijua hilo?
 
Taasisi muhimu sana katika kuandaa kiongozi ni jamii yenyewe yaani wananchi wa kada mbalimbali katika jamii wana umuhimu mkubwa sana kuweza kuandaa viongozi wao ambao wanatakiwa watoke miongoni mwao.
 
Kama ni hivyo, sasa inakuwaje wanasiasa na taasisi za kidini zinashutumiana kwa kuandaa viongozi wa kisiasa? maana kama anayetakiwa kuandaa kiongozi ni familia, hakuna sababu ya kulumbana, je hao wanaolumbana wanalijua hilo?

It clear from this discourse that there is a very big misrepresention if not misinterpretation of the Waraka and Mwongozo. Taasisi za kidini hazina haja ya kuwaandaa viongozi bora. Walichofanya ni kuainisha vigezo vya kumpata kiongozi bora. Kwa mfano waraka unahimiza wananchi wajiulize maswali fulani na muhimu kabla ya kumchagua huyo kiongozi hususan je ni mwadilifu, mzalendo, mchapakazi, sio mchoyo, n.k. Hii ni tofauti na kuandaa mtu. Waraka na mwongozo vinalenga kutafuta watu mbali mabali na kuwaweka kwenye "kapu" moja alafu anatafutwa mmoja mwenye kukidhi vigezo vilivyoahanishwa na huyo ndiye achaguliwe. Sio watu wachague kiongozi kwa sababu ya khanga, pombe, uzawa, utajiri n.k. Ingawa sijasoma mwongozo lakini jambo moja linalojichomoza sana ni kwamba unawataka waislam kuchagua kiongozi atakayetetea maslahi ya waislam maana wanasema they have been taken for ride for donkey years. Hii ni tofauti na kuandaa (groom) kiongozi wao.
 
Back
Top Bottom