Ni nani ampaye Slaa 'Mabomu'?

Kwaninini unafikiria kwamba kuna watu wanampa hayo mabomu? kwani yeye hayaoni kwa macho yake wakati yumo humohumo kwenye system anauona uovu wote unaotendeka? hata hao wengine wote wanajua each and every thing . sema tu Dr. slaa MUNGU kampa ujasiri ambao wengine hawakupewa na hata kama wapo waliopewa lakini wanashndwa kuutumia!! Dr. goooo goooo!! Tunakuombea hawakuwezi MH.
 
Dr. W. Slaa hajalipua bomi lolote jipya ambalo watanzania wa kawaida kama mimi na wewe hatukujua. Ninachomfagilia Dr. slaa ni ujasiri wa kusema kuwa hili limetendeka ndivyo SIVYO wakati sisi wengine tukishasikia tunajifanya hatujui. Issue za EPA, Richmond, Meremeta zilianza hapa JF kabla hata Slaa ahajazivurumusha. Hili la Meli za pembe kuwa ina mkono wa kada wa CCM kila mtu alikuwa analijua lakini hatukusema, Juzi Slaa kalilipua. Nachotaka kusema ni kuwa tukibaki kusema ni Slaa analipua mabomu na kuulizana nani anayempa tunampa kazi kubwa sana ya kuikomboa nchii hii maana tutakuwa kama tunajaribu kusema yeye pekee ndiye awezaye na sisi ni watazamaji tu. Nadhani swali lingekuwa ni lini nitalipua mabomu niliyonayo (ya level ya kijiji, kata, wilaya, mkoa, Taifa) kama Slaa?

Nafikiri cha msingi ni kulitambua bomu au kuliweka katika hali ya mlipuko mkumbwa, sasa wewe kama unayajua mabomu kwa nini usiyalipue? Dr. Slaa ana uthubutu, hivyo akiwa rais atasawazisha - land mines zote zitakwisha!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom