Ni nani ameufungia Mtandao wa X nchini Tanzania

Consigliere

Platinum Member
Joined
Sep 9, 2010
Posts
12,690
Reaction score
26,567
Hivi kuna uwezekano serikali ikaufungia mtandao wa 'X' (Twitter), lakini bado viongozi wake wakawa wanaendelea kuutumia kwa ku post na kufiatilia taarifa mbalimbali ikiwemo kuendelea kufanya online engagements?

Kabla ya kuufungia huo mtandao kuna taarifa yoyote rasmi serikali iliitoa kwa wananchi wake na watumishi wa umma kwamba serikali ime ban mtandao huo? Kwa muda gani? na sababu zipi? Au kuna watu tu wakajiamulia kuufunga?

Je viongozi na watu wengine wanaoendelea ku post kule, wenyewe wanatumia njia gani kuweza kuutumia mtandao huo? Kwanini? Kulikuwa na ulazima gani wa kuufunga?

Vipi kuhusu watu wafanyao biashara kupitia mtandao huo? ndiyo wahesabia kuwa maduka yao yamefungwa? Vipi hizo sababu zilizopelekea mtandao huo kufungwa hazipo kule TikTok , Instagram na facebook?

Kwa hali hii si ni rahisi sana Tanzania ikarudishwa gizani? Vipi kama vijana wa mataifa shindani wataitumia hiyo kama fursa ya kuwaondoa watanzania mitandaoni na kupunguza ushindani wa fursa za kimtandao?
 
⌚💯
 
Ndugu yangu umewaza kama nilivyowaza mimi... Shida iko hivi:
1.Tuko kwenye taifa ambalo watu wako tayari kuhoji ongezeko la bei ya vinywaji kuliko bei ya unga.
2. Tuko kwenye taifa ambalo mtu kutaka kujua haki yake anakuwa amefanya kosa.
3. Tuko kwenye taifa ambalo ukifanya wizi kwa kutumia akili kubwa unasifiwa.
4. Tuko kwenye taifa ambalo serikal yake iko tayari kutangaza hamasa ya ulipaji wa kodi bila kutangaza au kutoa kauli dhidi ya utekwaji wa watu unaoendelea nchini.

NB:
Sijasema kuwa serikal inahusika na watu wanaotekwa nchini. lakin swali langu ni moja... Hivi ukiwa unashutumiwa kwa maneno mbalimbali kukuhusu na ukakaa kimya bila kukanusha! maana yake ni nini?
 
Back
Top Bottom