Ni nani aliye hai kati ya wafu (CCM)?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni nani aliye hai kati ya wafu (CCM)??

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Paddy, Mar 16, 2011.

 1. Paddy

  Paddy JF-Expert Member

  #1
  Mar 16, 2011
  Joined: Sep 22, 2010
  Messages: 273
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Wana JF salaam!!

  Kwanza napenda ku-declare interest kwa kuwaomba msome my signature.

  Kwangu mimi CCM kama institution ni sawa na maiti inayotembea. Lakini hii hii institution ndiyo inayoendelea hadi sasa kutuwekea viongozi tusiowapenda na wala kuwatarajia. Ningependa leo niangalie kidogo hawa prospective candidates wa urais in 2015 kutoka CCM.

  Kwa majina machache ni hawa; Lowassa, Sumaye, Prof. Mark Mwandosya, Membe na Magufuli.

  Hapa nataka kuja na hoja ambayo most of you mtani-brand 'mkanda', yani nina ubaguzi wa kikanda. Lakini nataka tujadili hili swala japo kidogo tuelewe moja ya factor ambayo inaweza ikawa inaturudisha nyuma.

  Tuangalie marais waliopita na wanakotoka;
  1. Mwl. Nyerere - Musoma, mchapa kazi sana
  2. Mwinyi - Zanzibar (pwani), kila kitu ruksa (msisitizo wote wa nyerere katika kazi ulikufa hapa)
  3. Mkapa - Mtwara (pwani) - kidogo kazi ilifanyika lakini hakukua na tofauti kubwa na mwinyi
  4. JK - Bagamoyo (pwani) - kama kuna kazi mnaona imefanyika labda mniambie ninyi.

  Na sasa tuangalie viongozi tunaodhani ni wachapa kazi
  1. Magufuli - Lake zone
  2. Lowassa - Arusha
  3. Dr. Slaa - Arusha
  4. Mwandosya - Mbeya

  Mbali na kwamba baadhi yao hapo tunawajua ni mafisadi lakini walionekana au wanaonekana kutenda kazi kiasi flani. Sasa wanaJF, tuendelee kuwaachia nchi watu wa pwani kama Membe (one of the aspirants)? Lini tutajaribu watu wa bara kama tulivyofanya kwa nyerere?

  Sijatumwa na mtu kumchafua Membe ila napenda tu tujadili hili swala la watu wa pwani kushika nchi. Membe amefanya mangapi wizarani au jimboni zaidi ya kuwa muongeaji sana kama JK alivyokua????

  Karibuni tudiscuss kidogo
   
 2. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #2
  Mar 16, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Umewasahau na hawa nao wanatajwatajwa sana..........
  Asha-Rose Migiro(Sijui ni wa pande zipi) na Prof. Anna Tibaijuka(lake zone).
  Back to the topic...
  Ukanda au sehemu anayotokea mtu si ya muhimu sana, zaidi itazidi kutugawa kikabila, muhimu ni tupate watu wachapa kazi ambao wanaweza kupambana na ufisadi regardless wanatokea pande gani za nchi hii..
   
 3. Paddy

  Paddy JF-Expert Member

  #3
  Mar 16, 2011
  Joined: Sep 22, 2010
  Messages: 273
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Unachosema ni kweli kuwa inabidi tuavoid ukabila na ukanda but i think we need to be careful with the people we choose to lead us. Some of them are traditionally and culturally non-hard workers.
   
 4. M

  Marytina JF-Expert Member

  #4
  Mar 16, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  eneo atokako mtu halina uhusiano na utendaji wake kwani ROSTAM ni wa Pwanii?huyu ni mtu wa bara tabora mwanawani.
   
 5. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #5
  Mar 16, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 738
  Trophy Points: 280

  inashangaza sana kwa mtanzania kufikiria ukanda kwenye kutoa rais wa nchi hii.hujawahi soma katiba juu ya sifa za mtu awezae kuwa rais wa nchi hii? unatumia kigezo kipi kusema kiongozi hajafanya lolote la maendeleo jimboni au wizarani kwake.sijawahi fika rungwe kwa mwandosya au mtama kwa membe ila fanya utafiti kwanza kabla ya kusema hakuna lililofanyika.ninashangaa sana pia kumuweka lowasa katika list yako kwani hana nia njema na sie raia wa kawaida zaidi ya kuzidi kutuibia kwa kushirikiana na rafiki zake
   
 6. Paddy

  Paddy JF-Expert Member

  #6
  Mar 16, 2011
  Joined: Sep 22, 2010
  Messages: 273
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Sio nia yangu kuingiza ukanda, next time nikijenga hoja itabidi nizungumzie kuweka vigezo "strict" vya mtu kuwa kiongozi wa nchi hii. Mimi kwa upande wangu naumia sana kuona nchi inarudi nyuma badala ya kusonga mbele.
   
 7. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #7
  Mar 16, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 738
  Trophy Points: 280
  vigezo ni jambo lisiloweza kwepeka hata kidogo ila sidhani kiongozi bora anatoka kwenye kanda fulani
   
 8. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #8
  Mar 16, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Ni kweli uyasemayo, lakini hata katika zile kanda ambazo tunaona zina watu wachapa kazi pia wapo ambao si wachapa kazi. Muhimu inabidi kuwa makini katika kuchagua viongozi..
   
Loading...