Siasa za tanzania zinamezwa na vyama viwili CDM na CCM, kuna wakati vyote vinakosea na watz wangetamani mawazo nje ya vyma hivi viwili vikubwa nchini. Ukifanya uchambuzi vyama kama cuf,tlp,udp ni marehemu tayari huku bara. Chama pekee walau kinaweza kutoa mwanga huu ni nccr mageuzi kama kitawatumia wabunge wake vizuri kufikisha ujumbe na salamu za ukombozi. Ni wakati nccr waoneshe watz kuwa bado kuna matumaini nje ya ccm na cdm.nasema nccr kwasababu hakuna ubishi kuwa cuf ni sehemu ya sisiemu bada SUK, TLP,UDP ni matawi ya sisiemu miaka yote. Tumaini pekee hasa kwa vijana ni Nccr. Nawaomba viongozi nccr itazameni fursa hii watu wapo tayari. Mbatia ni mzoefu, dr Mvungi ni msomi aliyetukuka ktk taifa hili mkiunganisha nguvu na vijana wapambanaji kama mh machali na mh mkosamali mnaweza kuitumia hazina hii ya vijana wenye vipaji na tayari wapo bungeni. Ni wazo tu. Natoa wito kwa nccr kufungua njia kwa hoja na agenda zenu. Mambo ya migogoro yapotezeeni. Yatakwisha natural death. Hakuna sababu ya kujibizana baada ya maamuzi. Tusonge mbele jamani.
MchambuziFebruary,
3. CUF ( umaarufu wao ni kutokana na malengo na mafanikio yao kuwakomboa zanzibar ambao sasa ni taifa jipya with self determination; lakini kama ilivyokuwa kwa chama chochote cha ukombozi africa, kitapitia hatua tatu za maisha yake - growth, maturity, then saturation; Kwa sasa CUF ipo kwenye growth bado, na soon kitaingia kwenye hatua ya pili ambayo mafanikio yatatokana na utekelezaji wa ahadi zake za ukombozi; kikishindwa, na vikija vyama vipya zanzibar, CUF itaingia katiak maturity, na baadae saturation, njia ile ile tuliyopitia sisi TANU/CCM, katika siasa za bara).
Mchambuzi
Umesema chama cha ukombozi kinapitia hatua tatu growth, maturity then saturation nafikiri umesahau na death, kama chama chako CCM kimepitia hatua zote hizo unatuambia sasa kipo kwenye hatua ya mwisho ya kifo.
Nccr inaweza kweli kufufuka na kuwa chama chenye nguvu na mawazo mbadala? Mimi siamini Kama kinaweza.
February,
Usijali, kwani zamu yenu itafika tu kwani hakuna Chama chochote cha siasa hivi sasa kinachoendesha shughuli zake kwa itikadi, jambo ambalo lingewasaidia kupata wafuasi na mafanikio ya kudumu. Badala yake vyama vyote vina umarufu wa mpito:
1. Chama Changu Cha CCM (umaarufu wetu unatokana na personalities za baadhi ya wanasiasa ndani ya chama chetu ambazo zinawapa wananchi mvuto; tunamiliki dola na vimulimuli, hivyo wananchi wanaduwaa; na pia kuna suala la mazoea, hasa kwa wananchi wa vijijini - wana mazoea na CCM, so they are better off to deal with the devil that they know); Vinginevyo, Itikadi na Siasa yetu ya ujamaa na kujitegemea ipo kwenye vipeperushi tu;
2. Chadema (wao pia wana umaarufu wa mpito kama vile personalities na profile za baadhi ya viongozi wake ambao wanawapa wananchi mvuto; pia umaarufu utokanao na kampeni dhidi ya ufisadi; na suala la katiba mpya); CDM wana itikadi ya 'mrengo wa kati', lakini hatuoni idara yake ya siasa na uenezi ikiifikisha hii mioyoni mwa UMMA; ukichukua wananchi kumi randomly uwaulize unapenda chama gani? nina hakika majority watasema Chadema; Ukiuliza, Chama Chako Cha Chadema kina itikadi gani? atakukodolea tu macho, na punde ataanza masuala ya kuchoshwa na ufisadi, madai ya katiba mpya...
3. CUF ( umaarufu wao ni kutokana na malengo na mafanikio yao kuwakomboa zanzibar ambao sasa ni taifa jipya with self determination; lakini kama ilivyokuwa kwa chama chochote cha ukombozi africa, kitapitia hatua tatu za maisha yake - growth, maturity, then saturation; Kwa sasa CUF ipo kwenye growth bado, na soon kitaingia kwenye hatua ya pili ambayo mafanikio yatatokana na utekelezaji wa ahadi zake za ukombozi; kikishindwa, na vikija vyama vipya zanzibar, CUF itaingia katiak maturity, na baadae saturation, njia ile ile tuliyopitia sisi TANU/CCM, katika siasa za bara). Itikadi ya CUF ni uliberali, ambayo nayo haipo practised na chama, zaidi ya kauli mbiu ya 'haki sawa kwa watu wote' Isitoshe, itikadi ya uliberali ina mapungufu makubwa mno, kubwa ikiwa kutojali sana maisha ya watu wa chini. Give the fact kwamba wananchi wa Zanzibar waliokombolewa na CUF kutokana Tanzania Bara, ni wananchi walio nyuma sana kiuchumi, bila umakini, itikadi hii itaanguka kirahisi sana.
4. NCCR (umaarufu wenu unatokana na jitihadi zenu za kugombania umaarufu wa wenzenu; siasa zenu ni za kujitahidi kujaribu na nyinyi msipitwe na kila jambo 'la kupita'.);
Ndugu February, itikadi yenu NCCR ni ipi? tafadhali nielimishe.
Masuala haya yote hayana mashiko ya kudumu kwa vyama vyote hivi.
Hata Marekani, ilipata uhuru wake chini ya jamii isiyokuwa na vyama vya siasa, na hata katiba yake ilizaliwa katika mazingira yasiyokuwa na vyama vya siasa, na pole pole ikawa inafanyiwa marekebisho. Lakini pamoja na kutokuwepo kwa vyama vya siasa, jamii hii ilikuwa na itikadi zake mbalimbali, kwani itikadi sio zao la chama cha siasa bali ni zao la jamii, kama vile ilivyokuwa kwa chama cha siasa - chama sio zao la itikadi bali zao la jamii. Kumbuka,Itikadi ni:
"Mtazamo, mwongozo, value system, spirit ya taifa, around which matukio na matendo yote ndani ya jamii revolves, hivyo kuimarisha maana, mwelekeo, na tafsiri ya masuala mbali mbali ya ulimwengu, kwa jamii husika."
Ndio maana Marekani, ndani ya muda mchache, vyama vikaanza kuzaliwa ili kuanza kupigania itikadi zilizokuwepo kwenye jamii kwamba hii ni bora kuliko ile n.k; na matokeo yake ni vyama vikuu viwili democrats na republicans ambavyo core value zao wote ni itikadi.
Kwahiyo usiwe na wasiwasi na NCCR yenu, kwani kwenye suala la umaarufu wa mpito nyinyi ndio waasisi, kwani miaka ya mwanzo hadi katikati ya 1990, mlikuwa juu sana, na mngeweza kabisa kuchukua nchi kama palepale mngewekeza katika itikadi, badala yake mkazidi wekeza kwenye personalities - bagenda, kaborou, mrema, Lamwai, mabere marando, na vile vile kwenye agenda ya ufisadi chini ya utawala wa rais Mwinyi. Pamoja na umuhimu wa vitu hivi, hakuna ubishi kwamba ni vya mpito, na nyinyi NCCR ilitakiwa liwe funzo kwa vyama vingine. Lakini inaonekana hata vyama vingine vinatenda makosa yale yale.
Kwahiyo ningependa nikuhakikishie tu kwamba, as long as mambo yanabaki hivi hivi - yani siasa zisizoendeshwa kwa itikadi miongoni mwa CCM, CDM, CUF, zamu ya mafanikio yenu "PART 2" (kwani part one ni ile ya miaka ya 90), zamu yenu itakuja tu. Cha maana kwa sasa ni kuzidi kusali na kuombea vyama vilivyopo viendelee kung'a'gania masuala ya mpito badala ya kuendesha idara zao za siasa na uenezi kwa itikadi ambazo wanachama wao watazielewa na kuzishiba kama ndio core values za vyama vyama, hivyo kuwa na imani kwamba hiyo/hizo ndio direction wanataka taifa lao lielekee, na hivyo kuwa wanachama wa kudumu, wenye kupigania itikadi yao/zao na kuisambaza, huko kwenye makazi yao (mijini na vijijini), hata kwa kujitolea.
Mungu Ibariki Tanzania.
Mchambuzi
Idiology Tanzania? you must be joking, kitu hicho ni stage ya juu sana wa upeo kwenye nyanja za siasa especially wa nchi zetu hizi, hata kwa nchi zilizoendelea ni wachache sana wanaoangalia idiology ya chama wengi wanapelekwa na matukio wananchagua chama kutokana na matukio mfano vita vya Iraki, healthcare reform, nani kamuua Osama nk. Kwenye uchaguzi wa US uliopita Sarah Palin aliyekuwa mgombea mwenza wa Mc Cain aliulizwa na Gibson -"Do you agree with the Bush doctrine" akabaki anashangaa doctrine ni kitu gani, sasa unataka kwenda Merelani ukaulize idiology ya Chadema unategemea nini.
Mchambuzi unasema ufisadi ukiisha na katiba ikiandikwa Chadema itaishiwa hoja. Inaonyesha wewe si mwanasiasa bali ni mwanazuoni muumini wa siasa za vitabuni pale Kigamboni. Vita vya Iraki vimeisha Marekani imekosa cha kusema? Osama ameuawa je wameishia hapo kwamba wana relax? Kama unaamini kwisha kwa ufisadi ndio mwisho wa CDM hujiulizi kwa nini CCM haiwapeleki mahakamani watuhumiwa waufisadi. Wanajua wakithubutu kufanya hivyo utakuwa ni ushindi mkubwa mno wa Chadema wananchi ndio watazidi kukiamini chama tofauti na unavyofikiria. Elewa mwisho wa tukio ni mwanzo watukio lingine.
February,
Ndugu February, itikadi yenu NCCR ni ipi? tafadhali nielimishe.
Ndugu Mchambuzi,
Ukisoma katiba ya NCCR-mageuzi utaona kwamba ni chama kinachotumia itikadi ya Social Democracy (Itikadi ambayo inakataa unyama wa ubepari lakini haiko sana katika kukubali kila hoja ya ujamaa)
Aidha, mwanzoni mwa mwaka jana (2011) Halmashauri kuu ya NCCR-Mageuzi ililidhia kuboresha itikadi yake, na sasa Chama Kinajitambulisha kwa Falsafa na Itikadi ya UTU.
Chama kinasema, misingi ya UTU ni UMUHIMUWaKE, yaani
UDUGU
MAADILI
USAWA
HAKI
IMANI
MABADILIKO au MAGEUZI
UKOMBOZI
WAJIBU
KAZI
ENDELEVU (sustainability)
Misingi hii yapaswa kuwa ndio kiongozi cha masuala ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.
Chama kiko mbioni kuchapisha kitabu chenye ufafanuzi wa kina wa Itikadi hii
Mkuu ni mara ya kwanza mwana CCM kidogo kuongea jambo makini ongera
Masikini Mchambuzi niliposema wewe ni mwanazuoni wa siasa za vitabuni sikukosea inawezekana unasoma sana vitabu vya siasa na kusahau kuwa siasa hazina formula.Then hii ni itikadi more practical kuliko zote zilizopo sasa - ni more promising kuliko itikadi za to CCM, CHADEMA na CUF, kwani angalau hii ina upenyo wa kupingana na majangili wa IMF na WorldBank, kwani CCM, CDM, wote wanaendesha siasa za kuwapigia magoti watu hawa. Wanachoshindania CCM na CDM ni kwenda ikulu kuwa mtekelezaji wa masharti ya IMF na World Bank kwa ufanisi kuliko mwenzake. Hakuna sehemu ya sera zao ambako wanatambua jinsi gani madudu haya yanachangia umaskini katika nchi yetu. The future of Tanzanai lies on Political Parties with Social Democracy Orientation. Nitakuja kufafanua hili siku nyingine, kwani najua maelezo haya yameacha wengi na maswali zaidi. Natamani siku moja vyama hivi vikae kwenye TV LIVE, mada iwe ni kujadili itikadi za vyama mbali mbali, kuuza itikadi zao, na umma upate muda wa ku interact na wahusika - Nape, Mnyika, Mtatito, Mvungi,..., hakika mtabaini mapungufu mengi sana nayo yazungungumzia.