Ni mwenyezi Mungu yupi anatajwa katika dua za Bunge

VIVIANET

JF-Expert Member
Aug 30, 2015
2,129
2,918
KUNA WATU HUPENDA KUCHANGIA HOJA BILA KUSOMA VIZURI MADA, WENGINE WANA KASUMBA YA KUPENDA KUBEZA KILA WANACHOKIONA. ILA NAOMBA TUJADILI KWA PAMOJA

AWALI YA YOTE NINGEPENDA KUFAFANUA KWAMBA WANADAMU CHINI YA MBINGU HAWAABUDU MUNGU MMOJA, HII NI KUTOKANA NA MISINGI YA IMANI ZAO WAPO WANAABUDU MITI,MAWE.MILIMA,WANYAMA,BAHARI,MAZIWA ,JUA, MWEZI,NYOTA AU MITO NK. ILA WAPO WENGI WANAOSEMA KWAMBA WANAMWABUDU MUNGU WA MBINGUNI, ILA SIAMINI KAMA WANAABUDU MUNGU MMOJA MAANA WAMETOFAUTIA SANA KUHUSU HUYO MUNGU WA MBINGUNI,NA HATA MISINGI YA IMANI ZAO IMETOFAUTIANA SANA KUHUSU HUYO MUNGU WA MBINGUNI KWAHIYO NAAMINI WANAABUDU MIUNGU TOFAUTI KAMA ANGEKUWA HUYO MMOJA LAZIMA IMANI ZAO ZINGEFANANA

SASA SWALI LANGU NI HILI JE DUA YA KUOMBEA BUNGE WANAOMBA KWA MUNGU YUPI?

KWA MAANA MUNGU WA MBINGUNI ALIYEUMBA VITU VYOTE,MTAKATIFU ANACHUKIA
1-UNAFIKI
2-UONGO
3-KUDHULUMU HAKI
4-CHUKI NA FITINA
5-UBINAFSI UCHOYO NK
HAYO YOTE NA MENGINE MENGI YAMEJAA KATIKA NI WANAFIKI SANA, WANAWEZA KUTETEA JAMBO AMBALO WANAJUA HALINA UKWELI KWA MASLAHI YA VYAMA VYAO NA HUKU WATOKA KUOMBA DUA YA KUMWAMBIA MUNGU AWAONGOZE.SIJUI NI MUNGU YUPI ANAYEWAONGOZA KWENYE KUTETEA UONGO,DHULUMA NA CHUKI.

WABUNGE WAMEKUWA WAKITUMIA VIBAYA PESA ZA UMMA HUKU WATANZANIA YATIMA,MASKINI,WAJANE NA WAGONJWA WAKIKOSA MSAADA.MUNGU YUPI WANAYEMUOMBA? ASILIMIA KUBWA YA WABUNGE NI WAONGO HAWAWEZI KUSIMAMA KTK KWELI...VIONGOZI WENGI WENGI HAWATENDI HAKI NA MAHALI POPOTE ALIPO MUNGU WA KWELI LAZIMA HAKI HUSIMAMA...SASA HUYO MUNGU WANAYEMUOMBA NI YUPI?
 
Naongezea,asilimia kubwa ya wabunge wamepata ubunge wao kwa kuweka maagano na shetani.Sasa sijui wanapoapa kwa kutumia Bible au Quran wanamaanisha nini?I hope I didn't go out of the topic.
 
Binadamu katika ubora wake! Ndio viumbe wake hao...angeamua kuwaumbua na kuwahesabia maovu yao na jinsi walivyoshinda. ..tungeshuhudia maajabu
 
..

AWALI YA YOTE NINGEPENDA KUFAFANUA KWAMBA WANADAMU CHINI YA MBINGU HAWAABUDU MUNGU MMOJA, HII NI KUTOKANA NA MISINGI YA IMANI ZAO WAPO WANAABUDU MITI,MAWE.MILIMA,WANYAMA,BAHARI,MAZIWA ,JUA, MWEZI,NYOTA AU MITO NK. ILA WAPO WENGI WANAOSEMA KWAMBA WANAMWABUDU MUNGU WA MBINGUNI,...

SASA SWALI LANGU NI HILI JE DUA YA KUOMBEA BUNGE WANAOMBA KWA MUNGU YUPI?

....SASA HUYO MUNGU WANAYEMUOMBA NI YUPI?
Kwanza elewa ndugu, wanasiasa wote kasoro wawili ni matapeli tu. Siasa ni utapeli. Na Bunge ni jumba la kufanyia siasa.Utapeli unaofanywa kisheria.
Wenyewe wanasiasa wanasema tusichanganye dini na siasa kwa sababu wanajua wakimtaja taja Mungu wanajiingiza matatani. Kama ulivyosema Mungu hapendi uongo na unafiki. Wanasiasa kwa uongo na unafiki hawana mpinzani katika jamii. Kwa hiyo, ukimsikia mwanasiasa anakwambia, "niombee au niombeeni kwa Mungu" kama umo ndani toka nje ya nyumba na angalia nyumba yako haijaekwa alama ya X? Pia jiangalie kiooni kama una kipele, chunusi au jipu fanya utaratibu wa kuliziba kwa plasta ili asilione, akiliona umeumbuka.

Mungu yupi ni Mungu wa wanasiasa?
Hao watu wana mungu mbili tu, mungu matumbo yao na Ile mungu ya kingunge ngombale mwiru.
Na wanaomba kwa mungu hizo.
 
Wewe mbona unazini,
Unasengenya, unasema uongo, unatamani vya wenzio, unaenda kwa waganga, hutoi sadaka,
Unanyanyasa mayatima, husaidii maskini,
Na mengine mengi tu,

ILA UNAMUABUDU MUNGU NA MAOMBI YAKO ANAKUPATIA.

Acha kuhukumu, huna mamlaka hayo.
 
Mungu wa 2 korintho 4:4

Ha ha ha! Huo mstari unasema hivi:-

"The god of this age has blinded the minds of unbelievers, so that they cannot see the light of the gospel that displays the glory of Christ, who is the image of God".
 
KUNA WATU HUPENDA KUCHANGIA HOJA BILA KUSOMA VIZURI MADA, WENGINE WANA KASUMBA YA KUPENDA KUBEZA KILA WANACHOKIONA. ILA NAOMBA TUJADILI KWA PAMOJA

AWALI YA YOTE NINGEPENDA KUFAFANUA KWAMBA WANADAMU CHINI YA MBINGU HAWAABUDU MUNGU MMOJA, HII NI KUTOKANA NA MISINGI YA IMANI ZAO WAPO WANAABUDU MITI,MAWE.MILIMA,WANYAMA,BAHARI,MAZIWA ,JUA, MWEZI,NYOTA AU MITO NK. ILA WAPO WENGI WANAOSEMA KWAMBA WANAMWABUDU MUNGU WA MBINGUNI, ILA SIAMINI KAMA WANAABUDU MUNGU MMOJA MAANA WAMETOFAUTIA SANA KUHUSU HUYO MUNGU WA MBINGUNI,NA HATA MISINGI YA IMANI ZAO IMETOFAUTIANA SANA KUHUSU HUYO MUNGU WA MBINGUNI KWAHIYO NAAMINI WANAABUDU MIUNGU TOFAUTI KAMA ANGEKUWA HUYO MMOJA LAZIMA IMANI ZAO ZINGEFANANA

SASA SWALI LANGU NI HILI JE DUA YA KUOMBEA BUNGE WANAOMBA KWA MUNGU YUPI?

KWA MAANA MUNGU WA MBINGUNI ALIYEUMBA VITU VYOTE,MTAKATIFU ANACHUKIA
1-UNAFIKI
2-UONGO
3-KUDHULUMU HAKI
4-CHUKI NA FITINA
5-UBINAFSI UCHOYO NK
HAYO YOTE NA MENGINE MENGI YAMEJAA KATIKA NI WANAFIKI SANA, WANAWEZA KUTETEA JAMBO AMBALO WANAJUA HALINA UKWELI KWA MASLAHI YA VYAMA VYAO NA HUKU WATOKA KUOMBA DUA YA KUMWAMBIA MUNGU AWAONGOZE.SIJUI NI MUNGU YUPI ANAYEWAONGOZA KWENYE KUTETEA UONGO,DHULUMA NA CHUKI.

WABUNGE WAMEKUWA WAKITUMIA VIBAYA PESA ZA UMMA HUKU WATANZANIA YATIMA,MASKINI,WAJANE NA WAGONJWA WAKIKOSA MSAADA.MUNGU YUPI WANAYEMUOMBA? ASILIMIA KUBWA YA WABUNGE NI WAONGO HAWAWEZI KUSIMAMA KTK KWELI...VIONGOZI WENGI WENGI HAWATENDI HAKI NA MAHALI POPOTE ALIPO MUNGU WA KWELI LAZIMA HAKI HUSIMAMA...SASA HUYO MUNGU WANAYEMUOMBA NI YUPI?
huyuhuyu
 
Vivianet,DUA hili lingesemwa na wabunge wote lingeleta maana zaidi kuliko kusomwa na mtu mmoja.Kwa maana ya kwamba unapokuwa unitafakari DUA ya BUNGE kwa UMAKINI wake basi wabunge wangekuwa na utulivu na kwa uhakika wangefanya mjadala ule kwa HEKIMA,BUSARA na kuweka UTAIFA mbele.DUA inaposomwa na mtu mwingine ukaisikiliza tu,haileti maana yoyote sababu utakuwa unafikiri kitu kingine kabisa.

Ningelishauri Bunge kama kuna wabunge wanapitia huku DUA ile isomwe na wabunge wote ili ilete maana kamili ya DUA
 
Yaap umenena mkuu.
Isomwe na wote kama wanavyoimba wimbo wa taifa.

Vinginevyo kwa kweli wabunge na bunge lao wanafanya tu ibada kama zile za kina Firauni (laana ya mwenyezi Mungu iwe juu yake).
 
Sidhani kama ni sala ya MUngu wa Mbinguni kwani UTAIFA hauwekwi mbele bali maslahi binafsi zaidi tena ki wiziwizi. Angalia mikataba mibovu inayotuharibu ubinafsi umeitawala!
 
Yaap umenena mkuu.
Isomwe na wote kama wanavyoimba wimbo wa taifa.

Vinginevyo kwa kweli wabunge na bunge lao wanafanya tu ibada kama zile za kina Firauni (laana ya mwenyezi Mungu iwe juu yake).

Asante kwa kunielewa.Na pia iwalazimishe wabunge kuwepo muda wa DUA hiyo.Kama yupo Dodoma basi lazima aingie kwanza kwenye DUA hiyo ndipo aendelee na safari zake
 
Mungu wanayemtaja wabunge kwenye dua lao ni Mungu wa kila mtu ambaye kila mtu anamjua yeye ni mungu yupi(mungu binafsi).Kwa mfano kama mtu anaabudu Ng`ombe kama Mungu akiomba dua huyo Mungu anayemaanisha ni Ng`ombe wake anayemwabudu ndiye anamwomba amsaidie na alisaidie bunge.Kama mtu anaabudu kinyesi kama Mungu anapoomba ile dua mungu anayemaanisha ni kinyesi.Mtu kama Mungu wake ni Joka kubwa anaposali ile dua anakuwa anaomba kwa Joka analolitambua kama Mungu.Kwa mwislamu anakuwa anaomba Dua kwa ALLAH kwa Mkristo anaomba kwa Yehova NK.Ni sawa na wimbo wa Taifa unaweza imbwa na watu wa dini zote wanaoamini miungu tofauti tofauti kila mtu akaimba lakini kila mtu akiomba mungu wake amjuaye mwenyewe.

Hiyo dua ya BUNGE imewekwa makusudi kuhakikisha miungu yote iliyoko duniani na iliyoko inje ya dunia inayojulikana na isiyojulikana ya ukweli na ya uongo yote imo kwenye hiyo dua kwa ajili ya watu wa imani zote kama ulivyo wimbo wa taifa.

Dua na nyimbo za Taifa ziliwekwa enzi hizo na watu wenye akili mno wa enzi hizo wajuao kuweka makundi tofauti yenye imani tofauti pamoja
 
Mwenyezi Mungu anayetajwa kwenye dua la bunge ni yule yule anayetajwa makanisani na misikitini. Kusema kwamba eti kwa sababu kuna mengi mabaya yanayoidhinishwa na bunge basi Mungu anayeombwa dua sio yule wa sehemu nyingine, sio jambo sahihi. Katika zile sadaka na zaka zinatolewa misikitini na makanisani, baadhi ya wanaozipeleka kule ndio hao hao wanaohusika katika kesi za ufisadi, baadhi yao ndio hao hao majambazi wenye sifa ya kupora maduka na mali za watu mbalimbali. Duniani wanaishi wanadamu hawaishi malaika, hakuna na hakutawahi kutokea taasisi ambayo itakuwa na uadilifu na usafi kwa asilimia mia moja. Haitawahi kutokea taasisi safi kabisa yenye kuongozwa na watu wenye jeuri ya kujiita wasafi kiasi cha kukosa madoa ya aina yoyote ile.

Humo bungeni wapo wana CCM, chama ambacho kimekuwa na sifa mbaya kiasi cha rais Magufuli kukiri hadharani. Humo bungeni wapo wana CHADEMA, chama ambacho na chenyewe hakina jeuri ya kujiita ni chama chenye maadili mema, sio chama ambacho hakiwezi kukwepa kuhusishwa na siasa za ufisadi. Hakuna binadamu anayetembea duniani, mwenye jeuri ya kujiita msafi ambaye eti anao uhalali wa kulitumia jina la Mungu kwa haki kwa sababu anastahili. Mabunge ya Marekani na Russia yanazo dua ambazo zinaelekezwa kwa Mungu. Ina maana mataifa hayo mawili makubwa hayafanyi unyama kwingineko duniani. Russia inaweza vipi kukwepa hatia ya mauaji ya mamilioni ya wananchi wa Syria?. Marekani inaweza vipi kukwepa hatia ya unyama na mauaji ya mamilioni ya raia wa Iraq?. Lakini wabunge wa mataifa hayo mawili makubwa wanaenda kanisani na misikitini.

Bunge letu linamtegemea Mungu yule yule ambaye ni mkuu kuliko chochote kile kama ambavyo mabunge mengine yanavyomtegemea. Ubinadamu siku zote hauwezi kuukwepa udhaifu.
 
Mie nakwambia kama moto wa jehanamu upo sidhani kama watu walio wengi watapona maana hawatekelezi hata wanayohapa ngali wameshika biblia am kuruhani.
 
Back
Top Bottom