GUSSIE
JF-Expert Member
- Dec 2, 2014
- 3,866
- 11,100
Tatizo la bei kupanda ni upungufu wa uzalishaji au kuna pesa nyingi kwenye mfumo wetu wa uchumi?
Vijana wengi sasa wana bet, Ni nani anajishughulisha na uzalishaji Mali, Kama hakuna anayelima, Vyakula tutatoa wapi? Kila mtu ana pesa ya kubet mfukoni. Bei za vitu zitazidi kwenda juu
Kila chombo cha habari kinasema baada ya dakika 10 za kubeti tu unavuna Milioni 20, Nani atakubali kwenda Kuongeza uzalishaji kwa hamasa ya Shinda kwa kubeti, Hakuna muujiza wa bei kushuka kama kila mtu ana pesa mfukoni za haraka haraka lazima azitumie kwenye bidhaa ambazo sokoni ni chache hivyo wauzaji wanaamua kupandisha juu
Kupunguza pesa kwenye mfumo wetu yawezekana kuna msaada kidogo, Pesa zikipungua watu wanaweza kuanza kufanya kazi na bei za vitu zikaanza kushuka, Je baada ya Kupunguza kwa miezi kadhaa pesa kwenye uchumi kupitia Benki kuu imesaidia bei kushuka, Nadhani bei zinazidi kuongezeka
Tangu tupate uhuru sijawahi kusikia thamani yetu ya pesa ikiimarika zidi ya dola ya kimarekani,
Tangu tupate uhuru sijawahi sikia bei za vitu ni nafuu, Kila utakaye muuliza atakuambia zamani bei zilikuwa rahisi sana, Zamani hiyo ni ipi kwa kila mtu?
Waliozaliwa 1970 wanasema zamani bei za vitu ilikuwa nafuu
Waliozaliwa 1980 wanasema zamani bei ya vitu ilikuwa nafuu
waliozaliwa miaka ya 2000 nao wanasema zamani bei ya vitu ilikuwa nafuu
Katika suala la bei ni nani mkweli na tumuamini?
Wahenga humu ndani tumewahi kununua kilo moja ya mchele kwa shilingi 10 tu yaani TZS 10 tu, Na wazee wetu wao walinunua kwa senti
Suala la uzalishaji mdogo ni Chanzo kikubwa kinachofanya thamani yetu ya pesa kuporomoka siku hadi siku, Na hili linapelekea bei za bidhaa kuongezeka bei mwaka hadi mwaka
Ni nani wa kulaumiwa kwenye uzalishaji hafifu au kidogo? Ni Raia ambao wanatumia mfumo ule ule wa jembe la mkono na Ng'ombe waliokosa Lishe au Ni sera za serikali kuhusu sekta binafsi
Wewe mwana Jamii Forum unae piga kelele kuhusu bei kupanda umewahi kufikiria kuhusu kuanza Kuongeza uzalishaji ili bei zishuke au tunasubiri tuletewe mchele wa kitumbo toka Thailand, Na tunavyozidi kuagiza tunapelekea tuitafute dola zaidi ya kimarekani na kuipa heshima hivyo kufanya thamani ya shilingi kupoteza nguvu mwaka hadi mwaka
Ushauri:
Twendeni tukachape kazi, Muda bado upo wa kurekebisha uzalishaji wetu na bei za vitu zitakaa sawa