Ni mwaka gani ambao Serikali ya Tanzania iliwagawia bure wananchi wake chakula ?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
125,690
239,249
Naomba nikiri kwamba kwa umri mimi bado ni kijana mdogo , hivyo pia naomba nikiri kwamba kuna mambo yaliyotokea katika nchi hii , hasa yale ambayo kumbukumbu zake hazimo kwenye maandishi siwezi kuyafahamu .

Kwenye utawala huu wa awamu ya 5 nimesikia na kuona mara nyingi viongozi wa serikali wakitoa ONYO KALI kwa wananchi wake kwamba iwe masika au iwe kiangazi , SERIKALI HAITATOA CHAKULA KWA WANANCHI WAKE , kuna waliosema hata ikibidi watu kufa basi kufeni tu , lakini hakuna chakula cha bure kutoka serikalini , as if upo utaratibu huo ama labda ulipata kuwepo mwaka fulani .

Tangu nipate akili sina kumbukumbu ya wananchi kugawiwa bure chakula na serikali , sasa naomba wakubwa mliomo humu mnikumbushe kama serikali iliwahi kufanya hivyo kiasi cha neno " HAKUNA CHAKULA CHA BURE " kuwa maarufu kuliko wimbo wa Taifa .

Naomba kuwasilisha .
 
Kuna wakati njaa huchukua nafasi mpaka kwenye akili zetu na kuna wakati siasa huchukua akili zetu ila katika hili napenda siasa tuweke pembeni tupatiane majibu ambayo yatatufanya tujifunze kitu kwa faida ya watanzania wote
 
Ukiwa kiongozi halafu hujui upo pale kwa nini ni tatizo la kwanza.Ila kutoweza kuwasaidia wananchi katika madhila yao ni zaidi ya ujuha.Ukiwa kiongozi ni vema kufahamu upo pale kwa minajili ipi!
 
Wakati wa elnino... Hukumbuki maindi ya njano wewe na mchele kitumbo...
 
Ukiwa kiongozi halafu hujui upo pale kwa nini ni tatizo la kwanza.Ila kutoweza kuwasaidia wananchi katika madhila yao ni zaidi ya ujuha.Ukiwa kiongozi ni vema kufahamu upo pale kwa minajili ipi!
kwani kumsaidia mtu hadi umpe kitu.
mfano je mwalimu au mzazi anapomchapa mtoto lengo lake ni kumkomoa???
 
Unapoambiwa unapewa bure haimanishi lazima upewe buree, kinachofanyika ni punguzo kwa kiasi kikubwa sana, kwa mfano debe moja la mahidi unaweza linunua kwa sh1000 badala ya 15000, na hali ikiwa mbaya sana, huweza kugawiwa buree, ila hili la punguzo la bei, limeonekana maeneo mengi ktk taifa hili pale panapotokeaa maafa mbalimbali
 
Kama serikali haiwezi kutoa chakula cha bure, kile kinachohifadhiwa na serikali ni cha kuuzwa? Au ni cha nini? Au huwa hamna chakula kinachohifadhiwa?
Msaada kidogo hapo.
 
Usiwe mbishi tu kama Arsene Wenger ni kweli enzi za Nyerere watu tulipewa unga wa njano toka Marekani labda wewe ni wale watoto wa CCM au ulikuwa mjini..
hawakupewa tu kulikuwa na sababu ya kupewa,aidha kulikuwa na njaa lakini sio kwamba serikali ilijisikia tu kugawa chakula.
 
Back
Top Bottom