NI MUNGU: MUNGU NA UPONYAJI

NI MUNGU: MUNGU NA UPONYAJI

clion dismas

Senior Member
Joined
Aug 6, 2017
Posts
185
Reaction score
169
​
Habari zenu wapendwa, poleni na majukumu ya kila leo. Wale ambao kiafya hali siyo nzuri ni imani yangu mungu yu mwema na mkono wake usiopungua rehema, atawaponya. Wale buheri wa afya, tuzidi kumshukuru mungu kwa zawadi hiyo.

Nawiwa kusema walau na mtu mmoja ambaye ujumbe huu utamnufaisha, mungu ni mwema, katika dunia ya leo yenye magonjwa mengi bado hakutuacha wapweke bila ya msaada wowote. Mungu ametupatia matabibu wa bure kabisa, madaktari wasio na gharama, madaktari wanaofanya kazi masaa yote, usiku na mchana.

Je, wawajua matabibu hawa? Bila shaka wawajua, nao ni:-
  • Hewa safi
  • Mwanga wa jua
  • Maji safi
Kubali, kataa ukweli huu mungu kaongea na manabii zake watupao ujumbe kila leo katika vitabu vyao. Kitabu cha “ mashauri juu ya kilimo”, kilicho andikwa na mwandishi nguli, ellen g. White, kimetanabaisha haya yote.
Mbali na hayo matatu, mungu ametupa wasaidizi wengine , naweza kuwaita matabibu wenza,
Mazoezi ya viungo, Matunda, nafaka pamoja na mbogamboga za kondeni katika uasili wake( mwanzo 1:29-31)
Jaribu kuchunguza magonjwa kwa wingi wake yanayowasumbua watu, chanzo chake mara nyingi ni uchafu. Naam, uchafu wa kimwili, mazingira pamoja na kiroho.

Matabibu hao 3 mungu anasema inapaswa kwanza wakutibu, wakujengee afya njema lakini pia wakufundishe kwamba yupo aliyemuweza wa kila jambo.
Ni vyema ifahamike pia, tiba inaposhindikana kwa sababu ya kukiuka taratibu na kanuni za kiafya, mungu huyohuyo ananyosha mkono wake na kutumia matabibu wa pili, ambao ni wataalamu wetu wa afya. Kubali kataa, hata siku moja, uendapo hosiptali anaekutibu si daktari bali ni mkono wa mungu wenye upendo kupitia huyo tabibu.

Wote twajua, zaidi ya asilimia 80 ya mwili wa mwanadamu ni maji, twajua kazi za maji ni zipi, kusafisha mwili wote, ndani na nje. Masomo yametolewa mengi juu ya maji yasivyotengana na figo. Figo bila ya maji ni kifo.
Lakini zaidi yafahamika, umuhimu wa hewa safi, tena hewa ya oksijeni. Mungu ameitoa bure kabisa. Alijua kwanga shughuli karibu zote za ndani ya seli wa mwanadamu( metabolisim) utegemea hewa safi ya oksijeni. Ukitaka kujua kwamba mungu anaelewa zaidi yetu, hebu kaa katika chumba chenye hewa chafu, vuta kwa dakika kadhaa na uniambie utakutana na jambo gani. Taarifa nyingi zimeripotiwa za vifo kwa wale wanaowasha majiko ya mikaa na kulala nayo ndani uku wamefunga milango na madirisha. Hii ni kwasababu ya wao kuvuta hewa chafu monoksaidi ya kaboni, inayopelekea oksijeni kuisha kwenye damu na wao kufa.

Ukitaka kujua kwamba mwanga wa jua ni dawa, fanya jaribio dogo tuu, jifungie eneo ambalo kuna kila kitu lakini hupigwi na mwanga huu wa jua. Tofauti na kwamba utakosqa vitamini d, mwili wako utakua dhaifu sana na akili pia haiwezi fanya kazi kwa ufanisi. Sayansi iko wazi juu ya hili.
Sitaki kusema maneno mengi sana lakini nataka kusema ya kwamba, mungu ametupa akili. Tuishughulishe miili yetu, tutokwe jasho kila siku kwa mazoezi ya viungo. Naam, lazima tuondoe uchafu mwilini, lazima tuishughulishe akili lakini pia mwili huu.
Umewahi jiuliza kwanini watu wa shamba, sanasana wale ambao kazi zao ni kulima mashamba kwa jembe la mkono huwa wana afya isiyosumbuliwa na magonjwa? Naam, naamini wajua, wanafanya mazoezi ya kutosha, wanapata hewa safi ,mwanga wa jua lakini pia wanatumia vyakula visivyo na sumu nyingi.

Asubuhi unapanda gari, ofisini unakaa kwenye kiti cha kuzunguka, mchana unaletewa vyakula vyenye mafuta mengi na vyenye kukobolewa, jioni unarudi na gari, unafika nyumbani, kazi zote kafanya mdada wa kazi, unalala na unaamka na maisha yako ni ya hivyo kila siku. Kweli utaikimbia presha? Utakikwepa kisukari? Zaidi utaimarisha afya yam dada wa kazi huku wewe ukiwa jumba la magonjwa.




MUNGU NA UPONYAJI KATIKA MATUNDA , NAFAKA NA MBOGAMBOGA.

Hiki ni kitabu ambacho MUNGU amekileta kwako kupitia mimi kiumbe dhaifu, ujumbe ulioko ndani hapa unaelezea nguvu ya uponyaji wa mungu kupitia matabibu wako waliotuzunguka majumbani. Haihitaji gharama kubwa Zaidi ya kutii kile mungu alichotuelekeza kukifanya.
Mungu anasema kupitia kwa nabii wake kwamba, baada ya yule shetani mkuu kuhasi, aliketisha jeshi lake la mashetani na wakafanya maadhimio ya namna gani waweze kuwaangusha wanadamu ili wasiweze kuwa na afya njema, maazimio ya kikao chao ilikua ni kupitia chakula, KUHARIBU CHAKULA AMBACHO MUNGU ALIKITOA KWA AJILI YA MLO WA WANADAMU. KWA NJIA YA UKOBOAJI NA KUONGEZA SUMU KATIKA KILE KIINGIACHO MDOMONI MWA MWANADAMU,
SHETANI ANAJUA, ALIJUA AKIWEZA KUATHIRI KILE MWANADAMU ALACHO ATAMFANYA MTUMWA WAKE KATIKA MAISHA YAKE YOTE KWA KUUTAWALA UBONGO.( MASHAURI JUU YA KILIMO)

KWANINI UANGAMIE? WAKATI MUNGU KAMUWEKA SHETANI WAZI MBELE YAKO? HEBU UMPINGE, KWA KUWA NA MLO UNAOFAA, STAILI NZURI YA MAISHA UONE KAMA HATOKUKIMBIA.

Nitawagusia somo moja katika kitabu hiki na ninaamini litakubariki:-

SOMO LA 1


NJIA SALAMA ZA KUTUMIA MIMEA TIBA
​

Utangulizi

Madawa mengi ya kutibu wanadamu yapatikanayo kwenye famasi zote ulimwenguni utokana na mimea kwa asilimia kubwa.mimea hii yaweza tumika kabla haijaongezewa kemikali nyingi ili iweze kuifanya idumu kwa muda mrefu.

Kabla ya kutumia mimea hii, ni lazima taratibu salama zifuatwe za kiafya ili isijeleta matatizo makubwa mwilini mwetu. Ndio maana mtume Paulo anatupa tahadhari na kutwambia “NDIYO MAANA WENGI WENU NI DHAIFU NA WAGONJWA, NA BAADHI YAO WAMEKUFA”. (1 Wakorintho 11:30). Tusome kwa makini ili tusijekuwa kama taifa la Korintho.
HATUA SALAMA ZA KUFUATA

Baini chanzo cha Maradhi/Ugonjwa

Haijalishi dalili za ugonjwa ni ndogo au hafifu kiasi gani, uchukuapo mmea tiba na kuutumia, unahafifisha dalili za maradhi kwa muda, na waweza pata afueni ya kitambo lakini tatizo likiwa palepale.
Lakini, endapo chanzo cha dalili iyo yaani ugonjwa wenyewe usitambulike, utazidi kukua na kuwa sugu na utakapotokea tena utakua hatari zaidi na waweza kugharimu mauti.
Ni vyema, kila dalili za maradhi, uchunguzi yakinifu wa kitabibu ni lazima ufanyike na kubaini tatizo, ndipo mtu anaweza tumia mimea tiba.

Achana na tabia zisizo za kiafya
Endapo chanzo cha tatizo ni tabia zisizo za kiafya, kutumia mimea tiba ni kupoteza muda wako, na yaweza kuwa hatari zaidi kwa kuficha dalili nyingine za ugonjwa uku zikizidi kukua.
Jambo la kwanza baada ya kubaini tatizo ni kuishi maisha bora na safi ya kiafya, mfano huwezi tumia mimea kutibu ugonjwa wa mapafu wakati bado watumia sigara na hewa nyingi chafu wavuta.
Tumia mmea pekee utibuo maradhi
Haina haja ya kuchanganya madawa mbalimbali kwa kutibu ugonjwa mmoja, dozi ya dawa moja ikikamilika bila afueni ndani ya muda elekezi waweza pendekezewa dawa nyingine. Dawa hiyo ni vema iwe imethibitishwa na wataalamu wa dawa.

Acha kujipangia mimea tiba
Wataalamu waliobobea ndio wanaweza kukufafanulia dawa ya kutumia lakini siyo wewe. Kwa maana dawa hizi pia zina maudhi endapo zikitumiwa ndivyo sivyo.
Chukua tahadhari utumiapo mmea tiba kwa muda mrefu sana
Kiafya haipaswi kuvuka miezi mitatu, ikiwa hivyo, hakikisha uko chini ya uangalizi wa kitabibu. Kwa maana, kila kitu kinatumika kwa kiasi, kwa wingi wake kina madhara.


Tahadhari ya hali ya juu inatakiwa kwa wajawazito na watoto
Dawa nyingi huendana na uzito, hivyo umakini wa hali ya juu unatakiwa kama ilivyo kwa dawa zote zitolewazo hosipitalini. Maana, baadhi ya dawa hizi zina matokeo hasi kwa wajawazito na watoto wadogo.

KISA CHA KWELI


Yohana, aliyekuwa na umri wa miaka 55, ghafla alipoteza hamu ya kula na baadhi ya vyakula vyenye protini na fati nyingi vilimchefua sana. Jirani yake alimpatia mmea aliomwambia ungaliweza kumtibu. Ndani ya mwezi hali ilikua nzuri, baadaye, hali ya awali ikamrejea na kupungua uzito juu.
Aliamua kwenda kwa daktari wake. Baada ya vipimo ikafahamika tatizo la kukosa hamu ya chakula na kichefuchefu ilikua ni SARATANI YA TUMBO NA UVIMBE ULIKUA TAYARI MKUBWA KUWEZA KUUFANYIA UPASUAJI. MWISHOWE ALIFARIKI.


Funzo

Unapohisi kuna hali flani ngeni mwilini mwako, hima, wahi umuone mtaalamu wa afya mapema kabisa ili abaini ni kitu gani kinachokusumbua kwa kufanya vipimo. Mataizo mengine yakiwahiwa mapema, yanatibika.


UNAWEZA PATA KITABU HIKI KWA KUPAKUA APPLICATION YA UWARIDI, JINA CLION ODHIAMBO. KITABU: MUNGU NA UPONYAJI KATIKA MATUNDA, NAFAKA NA MBOGAMBOGA.

MAWASILIANO: odhiamboclion@gmail.com

+255759 15 44 79
 
Back
Top Bottom