Ni Muda muafaka wa kuwaondoa Lowassa, Mbowe, Lipumba, Seif kwenye Safu ya Juu ya wapinzani

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,735
Kila jambo na wakati wake. Nauona upinzani ukizidi kusinyaa na kukosa ubunifu kila kukicha. Mapungufu haya yanafichwa chini ya kisingizio cha ubanwaji wa democrasia, Pandikizi wa CCM, na sababu lukuki.

Kwa mtazamo, Upinzani unapaswa kuwaondoa hawa wazee kwa uhalili mstari wa mbele.
Wachukuliwe vijana machachali mstari wa nyuma wachukue nafasi zao nao wabaki kama washauri au watazamaji. Vijana waliojaribiwa na kuonekana wanafaa, wenye ubunifu, wenye changamoto chanya wasimame mstari wa mbele .
Mbadiliko haya yanapaswa kufanyika sio zaidi ya mwaka 2018.
 
Umemsahau mzee wa porojo na blah blah Tundu Lisu, huyu ndiyo wa kwanza kuondolewa kama Upinzani ulikuwa unataka kufika popote!
 
upinzani unapata changamoto si sababu ya watajwa bali hujuma na sisa chafu za dora ambazo ni hatari kwa nustakabari wa taifa letu: hasa vizazi vavyo ambao wataamini siasa ni uadui/vita kutokana na chuki za kihitkadi
 
Chuki chuki chuki. Sote tunaziona na hakuna anayezitaka isipokuwa ccm ambao wanadhani wanafaidi kumbe wanajizika.
God bless Lowasa, Mbowe, Lema, Mbatia, Tundu Lisu, Mnyika, Msigwa, HalimaMdee, professors, etc, etc.
We love them all.
And tired of ccm family which has become family business of few cadres only.
Where is Nyerere's legacy of transparency and credibility???
 
Mwenyedola ndio anapambana kuupoteza upinzani. Na upinzani uki-react bila mpangilio watakua wanajichimbia shimo wenyewe.
 
Ubabe ubabe ubabe. One day it will be like USA. Tutachagua jiwe kuliko ccm kama hali itaendelea hivi kama walivyofanya waamerika.
 
Lipumba ni kibaraka wa ccm. Kwa nini unamhusisha na wapenzi wetu wa moyo????
Seif ana shida gani. Ubaya wKe ni kushinda?
 
Mkuu anatafuta kuwafuta nanyie hapa mnawataka wapinzani wahamaki ili mkuu apate sababu ya kuwafuta.
Shame on you kwa kutaka kufuta democrasia katika nchi yetu yenye sifa kwa ajili ya kulinda ufisadi wa wenyewe ndani ya chama.
 
upinzani unapata changamoto si sababu ya watajwa bali hujuma na sisa chafu za dora ambazo ni hatari kwa nustakabari wa taifa letu: hasa vizazi vavyo ambao wataamini siasa ni uadui/vita kutokana na chuki za kihitkadi
unashauri nini kifanyike?
Tukiweka hayo yote pembeni huoni hitaji la upinzani kujisuka upya ili ufae zaidi kukabiliana na changamoto sio za taifa tu bali dunia. Kwa mtanzamo wangu wao wakuu wanapaswa warudi nyuma benchi la washauri na mbele wasimame vijana machachari ambao wako informed, wanaexposure, wananjia mibadala zaidi ya 10 katika kutatua changamoto za upinzani na taifa.
 
Mwenyedola ndio anapambana kuupoteza upinzani. Na upinzani uki-react bila mpangilio watakua wanajichimbia shimo wenyewe.
Miongoni mwa sifa bora ya upinzani jamii itayotarajia, ni uvumilivu na ukomavu katikati ya dhoruba yoyote ile ya kisiasa.
Ni uchanga kisiasa Kutusi,kurusha ngumi,kutumia technolojia kulaghai ili usiyempenda aonekane hafai, Mfano Cuf makosa au mwanya wautengeneze wao lakini lawama tunaaminishwa ni kwa Masajiri.
Ndio maana wengine tunashauri Kufanya mabadiliko ya waliomstari wa mbele ili Tupate sura na mawazo mapya.
 
hata
unashauri nini kifanyike?
Tukiweka hayo yote pembeni huoni hitaji la upinzani kujisuka upya ili ufae zaidi kukabiliana na changamoto sio za taifa tu bali dunia. Kwa mtanzamo wangu wao wakuu wanapaswa warudi nyuma benchi la washauri na mbele wasimame vijana machachari ambao wako informed, wanaexposure, wananjia mibadala zaidi ya 10 katika kutatua changamoto za upinzani na taifa.
wapinzani lazima wajitathmini na kuagalia mifumo na matatizi kwao
**jambo la msingi ni kwa watawala na wapinzani kuacha siasa chafu ambazo ni hatari kwa mustakabali wa nchi, Sababu ya kukosa maendeleo mojawapo ni saisa chafu kwani siasa zinatawala mfumo mzima wa maisha yetu
 
Mkuu anatafuta kuwafuta nanyie hapa mnawataka wapinzani wahamaki ili mkuu apate sababu ya kuwafuta.
Shame on you kwa kutaka kufuta democrasia katika nchi yetu yenye sifa kwa ajili ya kulinda ufisadi wa wenyewe ndani ya chama.
Hizo ni Hofu hewa, Yawezekana wapinzani wakawa na hisia za kufutwa lakini ukweli ni kwamba hayo malalamiko hayana uzito wowote. Yawezekana wakahisi wanabanwa lakini hisia za kufutwa ni kutafuta huruma za wananchi.
Kwa nini mpinzani ahamaki kama anajua majukumu yake na ana mental staminal ya kutosha na uvumilivu. Changamoto wanazopitia kwa upande wangu naona ni wito wa wao kufanya mabadiliko ya dhati ya ndani kabla hawajaja nje kwetu raia.
 
Dr Slaa ilikuwa aipiti wiki kadhaa keshazusha mambo either ya ukweli au kutunga lakini.CDM ilikuwa inapata publicity for the right reasons. Sasa hivi wakitokea ni kukosoa tu wakati mwenzao kila mara alikuwa anawafanya CCM wajitete.

Lowassa yeye ana mbinu tofauti kikubwa kwake his to serve his own selfish motives to become the president upinzani platform tu lakini anaenda kivyake kwa strategy yake.
 
Umemsahau mzee wa porojo na blah blah Tundu Lisu, huyu ndiyo wa kwanza kuondolewa kama Upinzani ulikuwa unataka kufika popote!
bado anahitajika leo kuliko siku nyingine. Mapungufu aliyonayo na umri wake yanarekebishika na anaweza kuwa kichocheo kizuri cha mabadiliko ya kweli. Watu wenye uwezo wa kukesha wanasoma mambo na kuyachakata kisha kuleta changamoto tunao wachache sio tu kwenye upinzani hata mitaani kwa raia wa kawaida. Anaweza kurekebishika kwenye hizo unazoziita porojo na kuwa msaada mzuri kwa siasa za tanzania. Mpe nafasi.
 
Dr Slaa ilikuwa aipiti wiki kadhaa keshazusha mambo either ya ukweli au kutunga lakini.CDM ilikuwa inapata publicity for the right reasons. Sasa hivi wakitokea ni kukosoa tu wakati mwenzao kila mara alikuwa anawafanya CCM wajitete.

Lowassa yeye ana mbinu tofauti kikubwa kwake his to serve his own selfish motives to become the president upinzani platform tu lakini anaenda kivyake kwa strategy yake.
mkuu umenena vyema. Hadi suala dogo la UDa alipoliongelea Kiongozi nao hao wakaanza vikao na kukanusha huku wakituhumiana kuchukua rushwa wakati kabla ya kuongelewa wote walikuwa kimya.

ndio maana tunapokuwa tunawaambia mabadiliko ndani yao wanatetewa na vibaraka huku na kujificha kwenye kichaka cha kuminywa democrasia. Inaweza kuwa kweli lakni sasa wanacheza ngoma ya watawala badala watawala kucheza ngoma yao.
Ndio maana tunaopenda changamoto tunaona wanapwaya sehemu. Waje kwa mbinu na mikakati advanced kidogo huku hawa wazee wakikaa pembeni kama washauri au kama ni wasaliti watolewe kwenye mifumo.
 
Upinzani ulikuwa enzi zileee! Sasa wanasingizia kubanwa lakini ukweli ni kwamba watu wamewachoka - viongozi wale wale, fikra zile zile, mbinu zile zile, ujanja ujanja ule ule, kupigania ruzuku kule kule. Wanapigania demokrasia lakini hata huko kwao demokrasia inasuasua na kuna wenyeviti na makatibu wa vyama wa kudumu. Wengine akina Cheyo mpaka vyama vimewafia lakini wamo tu.

Wapewe akina Mwaimu, Heche, Lissu, Mnyika, Sosopi, Mdee, Msigwa, Ben Saanane, Yericko Nyerere, Malissa na wengineo nao wajaribu kubadilisha mwelekeo na falsafa ya chama...
1586d3f29bc21d7cb8f509959c324f2a.jpg
Hicho kichwa hapo juu katikati kilikuwa na mikakati balaa. Halafu eti akaletwa huyu mwenzangu na mimi hapa chini kisa eti ni bingwa wa kuandaa migomo na ni Msukuma kwa hiyo atasaidia hukooo kanda ya ziwa. Matokeo yake hakuna cha mikakati wala nini ukiongezea na ile gia ya angani Aaaargh!
1d2a98b23ba5151fe4efbc9b848b5dbf.jpg
 
Upinzani ulikuwa enzi zileee! Sasa wanasingizia kubanwa lakini ukweli ni kwamba watu wamewachoka - viongozi wale wale, fikra zile zile, mbinu zile zile, ujanja ujanja ule ule, kupigania ruzuku kule kule. Wanapigania demokrasia lakini hata huko kwao demokrasia inasuasua na kuna wenyeviti na makatibu wa vyama wa kudumu. Wengine akina Cheyo mpaka vyama vimewafia lakini wamo tu.

Wapewe akina Mwaimu, Heche, Lissu, Mnyika, Sosopi, Mdee, Msigwa, Ben Saanane, Yericko Nyerere, Malissa na wengineo nao wajaribu kubadilisha mwelekeo na falsafa ya chama...
Zamani akisimama mpinzani anaevidence ambazo hazipingiki. Leo anatokea mmoja anasema kuna wabunge wamehongwa kwa maneno tu, Ushahidi fulani amesema zamani zilikuwa ni documents za kutosha kucemnt hoja wanazidiwa hata na mama mjane bhana. Anasimama mpinzani Tulishinda uchaguzi, Ushahidi kituo chetu cha kuhesabiwa kilivamiwa khaa!!!
Waphase out viongozi wote waweke kizazi kipya chenye changamoto chanya, Kizazi chenye updates, Kizazi chenye kupaza sauti siku moja ikasikika dunia nzima kila kona hadi kwenye tablet ya Trump. Kizazi ambacho hakiropoki bila research na ushahidi, Kizazi ambacho hakitoi tusi wala dhihaka hata kibanwe vipi maana sio sehemu ya mission yao.
Vijana wote machachari wa upinzani wanaweza kuwa shaped na kuleta changamoto chanya kwa taifa hili linalosuasua na lenye kuhitaji mawazo mapya kila leo Sio kupata umaarufu kwa Kejeli,Matusi,Kumtajataja kiongozi mkuu bali umaalufu wa Ideas and concepts that will shake authority.
 
Naona siku hizi ndugu yangu Mitale na Midimu umepevuka na kuona ukweli wa wanasiasa wetu na mabadiliko ya kweli tunayoyataka watanzania na si mabadiliko wanayoyataka wanasiasa.
Nimependa hoja zako zilizokwenda shule.
 
Kila jambo na wakati wake. Nauona upinzani ukizidi kusinyaa na kukosa ubunifu kila kukicha. Mapungufu haya yanafichwa chini ya kisingizio cha ubanwaji wa democrasia, Pandikizi wa CCM, na sababu lukuki.

Kwa mtazamo, Upinzani unapaswa kuwaondoa hawa wazee kwa uhalili mstari wa mbele.
Wachukuliwe vijana machachali mstari wa nyuma wachukue nafasi zao nao wabaki kama washauri au watazamaji. Vijana waliojaribiwa na kuonekana wanafaa, wenye ubunifu, wenye changamoto chanya wasimame mstari wa mbele .
Mbadiliko haya yanapaswa kufanyika sio zaidi ya mwaka 2018.
yawezekana ulikua na nia nzuri tu,lakini kwa haya uliyoeleza hapa huna concrete reason yaani umeandika bila kutafiti.pengine ungerudia kwa kutuwekea utafiti unaoonyesha upinzani umerudi nyuma katika mazingira gani,kivipi,na katika usimamizi wa namna gani kisheria unaosimamia usajili wa vyama vya siasa na shughuli zake.
 
Back
Top Bottom