Ni Mjazito Hataki Wazazi Wajue?

Ni Mjazito Hataki Wazazi Wajue?

Victor 20

Senior Member
Joined
Aug 14, 2013
Posts
146
Reaction score
15
Nina dada yangu mtoto wa baba mdogo aliyekuja mjini kureseat Necta ya form 4, alimaliza mwaka jana na kufeli sasa kabeba mimba. Tulizani kuwa ni malaria baba akanipa fedha nimpeleke akapime baada ya kupima hana malaria ni mimba, Sasa ananiambia nimfichie siri.

Naombeni ushauri wakuu.
 
msaada wakuu nifanyeje mie maana wale madoctor waliompima nahisi wanaweza wakamtoa kisirisiri nisipo sema
 
kama akijaribu kuitoa na akafa yeye na kitoto nitakuwa na dhambi kubwa sana duniani mpaka siku ya mwisho ya palapanda
 
Weka wazi wazazi waanze kujichanga hela ya pampas
 
Lazima ataitoa no way....Kama unataka asiitoe maana ndo kitakacho fuata bora uwaambie wazazi mapemaa...
 
Huyo mtoto aitwe UKAWA, Hivyo waambie wazazi mapema ili mimba asiitoe.
 
Lazima ataitoa no way....Kama unataka asiitoe maana ndo kitakacho fuata bora uwaambie wazazi mapemaa...

hata me nilkuwa nafkiria hivyo mkuu weekend hii nitafanya mpango huo
 
Kwanini unajiuliza kuwaambia wazee?? Au wewe ni sehemu ya tatizo- hiyo mimba ni yako mkuu?
 
Mwambie kuwa kama hatautoa huo ujauzito basi utamfichia siri lkn kama ana mpango wa kuitoa utasema. Hata hivyo ni veema kuwaambia wazazi wakati huo huo mtie moyo kuwa huo sio mwisho wa maisha na ikibidi mdadisi ili ujue mwenye huo mzigo hata ukiwaambia wazazi uwe na data zote. Mfanye rafiki akueze kwa kina ilikuaje.
 
Back
Top Bottom