Ni miaka 7 sasa ya mabomu ya Mbagala hakuna maazimisho

Jindal Singh

JF-Expert Member
Sep 9, 2015
1,857
1,538
Salaam...

Wakuu mnajua tukio la Mabomu Mbagala na matukio mengine yanayogharimu maisha ya watu wengi huwa serikali wanayafumbia macho katika kuandaa maazimisho yake.

Milipuko ya Mabomu - Mbagala ni tukio lililotokea mnamo saa 11:45 asubuhi ya tar. 29 Apili ya mwaka wa 2009 katika eneo la Mbagala jijini Dar es Salaam, Tanzania. Ni baada ya mabomu kulipuka katika ghala ya silaha ya kambi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)

Mabomu hayo yaliyokuwa yakilipuka kwa mfululizo yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 50, kujeruhi zaidi ya watu 200 na mamia kadhaa, wengi wao wakiwa ni watoto, kupotea. Athari nyingine ni uharibifu wa majumba na mali. Kati ya watu waliopoteza maisha katika mkasa huo ni mama mmoja ajulikanaye kwa jina la Sophia Shango, mkazi wa Mbagala kuu pamoja na mtoto wake. Wote walifyekwa vichwa na moja ya mabomu yaliyokuwa yakifyatuka kutoka kambi hiyo ya jeshi.

Japo watu watasema hakuna faida ya maazimisho, lakini hii husaidia kuwafariji wazalendo wafiwa.
 
Mijitu mingine bhana! maadhimisho kwani ni sherehe hiyo? umetumwa wewe.

Kwani Kila Maazimisho Sharti Iwe Sherehe? Mbona Taifa Linaazimisha Kumbukumbu Ya Kifo Cha Baba Wa TAIFA, Siku Ya Mtoto Wa Africa, Pia Bila Kusahau Sikukuu Ya MASHUJAA??.
Bila Shaka Wewe Utakua Kati Ya Watu Wanaopenda Kutoa Majibu Mepesi Kwenye Maswali Magumu.
 
Sana sana ni kuwakumbusha machungu ya kufiwa na fidia za shilingi elfu moja
 
Kwani Kila Maazimisho Sharti Iwe Sherehe? Mbona Taifa Linaazimisha Kumbukumbu Ya Kifo Cha Baba Wa TAIFA, Siku Ya Mtoto Wa Africa, Pia Bila Kusahau Sikukuu Ya MASHUJAA??.
Bila Shaka Wewe Utakua Kati Ya Watu Wanaopenda Kutoa Majibu Mepesi Kwenye Maswali Magumu.
Wewe wasema
 
Back
Top Bottom