666 chata
JF-Expert Member
- Mar 14, 2013
- 1,710
- 4,046
Nikiwa mdogo, nimeenda kuanza sekondari huko kwa mjomba, ndani ya miezi sita tu tangu nianze kuishi na familia hio, asubuhi yake tulisikia gari la matangazo limekuja pale nyumbani linatangaza kuwa nyumba yetu hiyo tunayoishi kesho yake itapigwa mnada, shangazi(mke wa mjomba) alichanganyikiwa.
Ni ukweli mjomba alikuwa ni mkimya sana, kumbe alikuwa kachukua mkopo kwenye hivi vitaasisi vya fedha kaweka rehani nyumba kashindwa kulipa na nyumba ndio ikawa sasa inapigwa mnada sisi tumo ndani, tulikuwa shocked familia nzima, ndani ya siku hiyo tulizungumzwa mtaa mzima, kila unakopita watu wanakushangaa kama tumeua.
Mjomba aliondoka tu kimya, kesho yake wakaja madalali na maspika yao wanatangaza ujinga tu pale eee nyumba hii kwa milioni 10 kwa mara ya kwanza, 10 kwa mara ya pili.
Sasa tukio lile la kukopa mpaka leo lipo kichwani, sijawai kukopa kitu nisichoweza kukilipa, siwezi kukopa na ninaogopa kukopa, nilishaathirika kisaikolojia kabisa, nikiona mtu anakopa anaweka dhamana nyumba huwa namsikitikia sana.
Nikiwa njiani natoka zangu sehemu sehemu usiku, nyuma yangu ikatokea bodaboda ikaja ikafika karibu na mimi kabisa wakaruka jamaa wawili wana mapanga mmoja anataka kunikata ili waniibie kile nilichonacho, nashukuru Mungu yule mwenye panga niliruka nae ki jet lee akaanguka chini nikakimbia mbio zisizo na idadi na wale wajinga wakaanza kunifukuza, bahati nzuri kwangu ulikuwa mtaa wa pili tu hapo.
Siku hizi usiku nikiona bodaboda inakuja usawa wangu na usiku najua ni wazee haoo naanza kujiandaa kabisa, na kuna muda nastuka sana bodaboda ikipita nyuma yangu kwa speed nawazia majizi jizi tu haya au linaweza kosea njia likanigonga.
Jioni moja nikiwa natembea na rafiki yangu barabarani huku tunapiga stori, niliishuhudia kitu cha ajabu sana njiani, pikipiki mbili ziligongana uso kwa uso, ubongo wa mmoja ulimwagika huku tunauona.
Njia ilikuwa ni nyembamba na hizi pikipiki zilikua zinatokea upande A na nyingine B zikiwa speed zote, mpaka leo mimi na rafiki yangu huwa tunashangaa kitu kile iliwezekanaje pikipiki zikagongana uso kwa uso hata kama njia ilikuwa nyembamba kiasi gani? Too bad njia ile wapita njia tulikuwa mimi na rafiki yangu tu, kabla ya wengine kuja, tulisimama kwa dakika kama tano hatujui tunafanya nini, tunasema hii ni kweli au ni ndoto.
Mpaka leo siwezi kupanda bodaboda kabisa, na sizipendi kabisa, nikiona mtu kapanda bodaboda tena hajavaa helmeti huwa natamani kumwambia mzee tubu kabisa dhambi yatakayokukuta huko.
Nimewahi kupanda mara kadhaa na penyewe yaani kwa kujilazimisha sana na kwa masharti kama visa ya UK.
Nikiwa nimeenda sehemu fulani kikazi, lodge niliyofikia usiku nimelala nasikia kabisa kuna mtu anatembea juu ya kitanda changu, niko macho nimezima taa ila ninaona kabisa hapa kitandani kuna jitu linatembea kabisa, linakaa, mara nasikia kama kuna kundi la watu linanong'ona chumbani. Nikasema huu ufala wanga hawamrogi wasiemjua, nikaamka nikarukia soketi ukutani halafu kwa matusi mazito, nawasha taa nasikia mtu anacheka dirishani kwa nje. Ebhana usiku ulikuwa mrefu, kwa mara ya kwanza nikaona umuhimu wa jua kuwaka tu masaa 24, mara bundi wanalilia dirishani kabisa, mara mtu anatembea juu ya but mpaka leo nikienda mikoani huko siwezi kulala lodge za kifala, bora nilale njaa ila nimefikia sehemu ya uhakika.
Nafikri haya ni matatizo ya kisaikolojia ambayo yamepatikana toka kwenye mazingira, yawezekana wenzangu mkawa na yenu ambayo ni makubwa na mazito zaidi au ya kawaida, lakini tukaona kumbe wenye hali hizi hatuko pekee yetu ni wengi hivi.
Basi tukaisukuma wikiendi yetu hii ndefu ya sikuku kwa mikasa ya hapa na pale na wataalam wa saikolojia wakasema mawili matatu.
Wasiwasi ndio akili.