Ni maswali tu, msinitukane!

MJENGA

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
883
Reaction score
852
Wanajamvi kuna jambo linanitatiza sana wakati juu ambapo siasa zimeshika kasi kuelekea uchaguzi mkuu. Ni kwamba chama cha mapinduzi kimeweka wazi kuhusu kutoridhishwa na mwenendo Wa Lowassa Wa kuanza kampeni mapema tena kwa kutumia nguvu kubwa ya pesa. Mbaya zaidi amebadili modality kwa kuanza kuwajaza mahela wanaccm njaa na eti kurudi kwake kumshawishi agombee kwa kumchangia fedha ambazo wamezitoa kwake. Inashangaza sana, kwa ufuatiliaji nilioufanya, wanaoogoza kumpigia debe Lowassa mitandaoni ni wanachadema. Aidha vyombo vya habari vinavyompamba Lowassa ni ITV na gazeti la Tanzania daima. Ninajiuliza maswali na pia kuwaulizeni wadau, je, ni kweli Tanzania daima linalomilikiwa na Mbowe halijui uovu Wa Lowassa?. Je, Reginald Mengi, mmiliki Wa ITV hajui uovu Wa Lowassa?. Kuna ni nyuma ya pazia?.

Msaada Wa majibu wadau. Matusi kama baadhi yenu mnaona yanafaa, jitusi kwanza wewe kabla hujanitukana. Karibuni.
 
Tuanzia hapa, uovu wa Lowassa ni nini ili tujadili kwa hekima,usilete Mwalimu kamkataa ni lini na kwa kosa gani. Uthibitisho tafadhali
 
Halafu pia sijawahi sikia hata siku moja viongozi Wa chadema wakiukemea ufisadi Wa Lowassa, kunani?
 
Acha kuwaalika watu wakutukane. Maswali yako yatajibiwa kwa kadiri ya ulivyouliza.
Sijui una uhakika gani kuwa CDM ndio wanaompigia debe au ITV inambeba, kumbuka Tanzania daima na ITV ni vyombo vya habari na moja ya kazi yao ni kuripoti yanayojiri katika jamii. Ukiacha Tanzania daima, gazeti ambalo linajulikana msimamo wake lakini ITV inajitahidi sana kuripoti habari bila ubaguzi, nasisitiza 'Inajitajidi'. Kuna Vituo vingine vya TV, habari hizi haziripotiwi kabisa. Je, ni ndogo kiasi hicho?
 
Tuanzia hapa, uovu wa Lowassa ni nini ili tujadili kwa hekima,usilete Mwalimu kamkataa ni lini na kwa kosa gani. Uthibitisho tafadhali

Hivi una elimu kiasi gani Rafiki?. Ulifaulu kwa kiasi gani maana naona kichwa chako ni kizito, hujauona uovu nilioueleza kwenye Uzi?
 
Hivi una elimu kiasi gani Rafiki?. Ulifaulu kwa kiasi gani maana naona kichwa chako ni kizito, hujauona uovu nilioueleza kwenye Uzi?
Ingekuwa vizuri kama "uovu" wa lowasa ulioutaja ungeuambatanisha na vielelezo, nadhani huyo bwana na wasomaji wengine wangeweza kuchangia mada yako bila ushabiki. Kwa jinsi ulivyomkashifu mwenzio huku ukiwa umeleta mada yenye uovu usio na ushahidi ni dhahiri mada yako ina lengo la kuzidi kumchafua ndugu lowasa. Usinitukane kama ulivyoomba usitukanwe
 
Hivi una elimu kiasi gani Rafiki?. Ulifaulu kwa kiasi gani maana naona kichwa chako ni kizito, hujauona uovu nilioueleza kwenye Uzi?

wew unatukana halafu hutaki kutukanwa! UmeuliZwa taja uovu wa el! Unamuita m2 hajaelimika! Ungumjibu tu kuwa kachota richmond etc! M.p.u.m.b.a,fu usiekuwa na kumbukumbu wew
 
"Mtu asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza kumpiga jiwe."
 
CHADEMA wanampigia debe EL ili akipitishwa na magamba wenzake owe rahisi kumgalagaza
 
wew unatukana halafu hutaki kutukanwa! UmeuliZwa taja uovu wa el! Unamuita m2 hajaelimika! Ungumjibu tu kuwa kachota richmond etc! M.p.u.m.b.a,fu usiekuwa na kumbukumbu wew

Umeshinda!
 
Janja ya chadema na ukawa ilishashtukiwa kitambo, mnatafuta pa kuiangushia CCM, mmenoa Lowassa hapitishwi ng'ooo!
 
Hivi una elimu kiasi gani Rafiki?. Ulifaulu kwa kiasi gani maana naona kichwa chako ni kizito, hujauona uovu nilioueleza kwenye Uzi?
Sasa kwa uliyoandika hapa ndo ya mtu mwenye elimu?....aliyefaulu vizuri?...mwenye kichwa chepesi?.....lol pole yako ndugu......Jamaa kakuhitaji KUDHIBITISHA unachodai ni uovu wa Lowassa......ulichoweza kufanya wewe 'mwenye elimu,uliyefaulu vizuri na mwenye kichwa chepesi' ni hicho?....ptuuuuuuu.....
 
Yes hii imekaa poa sana aliye mwema na aanze kumpiga lowasa mawe
 
Wengi wanaomuunga mkono Lowasa wanasema kashfa Richmond hahusiki ila alibeba mzigo wa kisiasa. Mie bado najiuliza kama mtu nimsafi kweli kama unawezaje kubeba mzigo wa mtu aliyewaibia Watanzania mabilioni yote? Kwa nini hakuwaacha wakabeba misalaba yao? Kuwakingia kifua wezi inamaanisha na wewe ni mwizi vilevile. Nchi yenye watu zaidi ya 40m hakuna mtu msafi kabisa tumkabidhi nchi yetu hii?
 
Mkuu wala usipate tabu! hapo kuna ukanda wote hao ni wa kaskazini.
 
Jaman Ripoti ya Leo iyosomwa kwa utafiti wa mikoa 13. Lowasa ameongoza. Watoto Vijana wazee wote wanaimba Lowasa Lowasa.
 
Janja ya chadema na ukawa ilishashtukiwa kitambo, mnatafuta pa kuiangushia CCM, mmenoa Lowassa hapitishwi ng'ooo!

MJENGA;
Kama weye ndo unampitisha basi utamkataa. Mngechelewa kidogo tu, Ikulu ingeenda kumshawishi. CCM hamna ubavu wa kumweka mwingine. Kumbuka mlisha anza kusema ati mtu yeyote atakayepitishwa na wengi ndiye mtamsimamisha kwenye ubunge.
Si mliona hasara yenu last tyme? Nasema EL atapita ccm bila kupingwa kwani nyiye hamna ubavu wa kumzuia
 
mkuu Mjenga usipate tabu na hawa jamaa. mbowe na lowasa ni walewale. WEZI.

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…