Ni masharti gani ulikua unapewa kuangalia tv kwa jirani enzi hizo

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,992
17,892
Haya maisha tunatoka mbali sana aisee.....

Miaka ya 2000 ndo tv zimeanza kushika kasi kijijin walokua na tv ni wachache sana

Basi nakumbuka kuna jirani yetu ndo alinunua tv

Kuna siku tumeenda kuangalia mpira akagoma kutufungulia halafu mvua ilikua inanyesha ilibidi tuangalie na dirishani nilinyeshewa na mvua hadi nikaugua homa

Kuona hivyo haikupita miezi 3 mzee wangu akanunua tv mambo ya kuangalia tv za kwa watu yakaisha ikawa na sisi watu wanakuja kwetu

Maisha haya nikikumbuka hili jambo nacheka sana.. Haya maisha haya

Tuambie ilishawahi kukutokea kuangalia tv za majirani enzi hizo, ni adha gani ilikukumba na ni masharti gani uliwahi kupewa?
 
Nilienda kumsalimia shangazi kutokana na ushamba wangu na kwetu hamna Tv nilivyofika pale kwa shangazi nikavizia shangazi yupo nje anaosha vyombo mimi nikajidai fundi wa kuwasha Tv na wakat ndo kwanza nimeionea kwake.

Nikaenda kwenye soket nikachomeka msumari nilitandikwa shoti nikapiga kelele.

Aunt akaja mbiombio akanikuta nimesharud kwenye kochi hata sijui nilifikaje kwa sekunde 1

Alivyo niuliza shida nini ? Nikaangalia angalia pembeni nikaona paka kajilaza alikua mpole sana yule paka nikasingizia paka ametaka kunikwangua ndo maana nmepiga kelele.

Kwanzia hapo nikawa naogopa Tv
 
Enzi za ze comedy

......kaeni chini,msikae kwa kochi.....chini,msiguse ukutani mnachafua rangi

Kabla hamjaingia mnakaguliwa weeeh, ze comedy ikiisha wanazima generator druuuuuuuuh..mnaambiwa mafuta yameisha,.....mkisepa wanawasha......

Ni vile tu utoto,makundi
 
Ze comedy hii ya juzi tu hapa mkuu? Au unazungumzia ipi?

Maana hapo hata mimi nilishaanza kimiliki
 
acha nicheke tu kiukweli nimekumbuka mbali sana
20211016_151459.jpg
 
Enzi za ze comedy

......kaeni chini,msikae kwa kochi.....chini,msiguse ukutani mnachafua rangi

Kabla hamjaingia mnakaguliwa weeeh, ze comedy ikiisha wanazima generator druuuuuuuuh..mnaambiwa mafuta yameisha,.....mkisepa wanawasha......

Ni vile tu utoto,makundi
Nimelipa sana 200 kuangalia ze comedy alhamisi
 
mimi kijiji nilichokulia jamaa mmoja mwaka flani ilibidi anunue generator na tv hitachi + deki ,akawa anaonyesha tv weekend mpaka weekend kiingilio 100 tu,kijiji kizima mpaka vitongoji vya jirani walikuwa wanajaa hapo,yeye kazi yake ni kwenda kuchukua cassete mpya mjini tu.

sasa sisi mzazi wetu roho yake alikuwa anaijua yeye mwenyewe faza yule,sijui alikuwa anaona noma kutoa 400 tukasafishe macho au alikuwa hapendi tu tukajichanganye,maana kiukweli kwa pale kijiji tulikuwa na life flani la ngazi mbili zaidi ya wengine.siku hiyo jpili night ndio anakomaa tusome usikuasubuhi shule kila mwanafunzi mwenzetu anasimulia mkanda wa jana,yaani alituvuruga kwakweli.

siku moja akaenda seminar,mkewe na wanae wawili wa kike wakaondoka kusalimia mjini na mama yao,ndani ya nyumba tukabaki wawili,yaani mimi na dogo wa kiume mwanae wa kwanza,tukakaa kikao na dogo wote tukakubaliana haiwezekani jpili hii tusiangalie movie,yaani zitumike mbinu zozote mpaka tukaingie kutizama picha.tumeshapewa tetesi kuna picha moja linaitwa red scorpio,amecheza bw dolf ni mauaji.asubuhi kukakucha,nikampanga dogo,oya kaa hapa acha nikamwone yule mwenye kibanda tujue tunayajenganje.
nikapanda baiskeri na madumu ya maji kama nakwenda mtoni,kijiji kile maji yalikuwa ya shida kiasi.
njia ni hiyo unapita kwa huyo jamaa mwenye banda la video.nikafika pale nikamkuta,nikamchana kila kitu,akanambia aaaaah mbona hamna noma wewe niletee dumu mbili za maji jioni mnaingia kiroho safi yaani,nikasema yees mambo si hayo bana!!fasta nikaenda nikabeba maji by saa tano nageuka,nikafika nikamiminia maji nikaguka tena mtoni,saa nane niko home,nampa dogo feedback ananipiga kifua,hakuna kama wewe ancle

imefika saa kumi na mbili watu wanapita pale home nasisi tunajiuliza tusepe au vipi,namwambia dogo inabidi tuvunge mpaka kuku ziingine bandani tufunge mlango tupaache safe,mara faza house huyu hapa,sijui kama uliishawahi kulia bila kutoa machozi na sauti mkuu kwa uchungu mkubwa!!!ndio ilikuwa hivyo yan.
akakuta baiskeri tumeifungia vitu tumepanga kuuliza vizuri tukamwabia ah unajua tuko peke yetu tunaogopa kufanya kazi na giza so tunafanya mapema tukiingia ndani hakuna kutoka,ni kusoma na kulala.akaguna kisha akasema,leo nataka mwende kwenye banda la video ila tunakwenda wote.

ikawa vibe ila sasa itakuwaje tumeshalipa kwa maji???vipi mjuba akikabidhiwa hela akagomakinaumana,basi tukatoka haooooo kufika pale nikamuwahi jamaa kwamba achukue tu hela ila hizo dumu za maji ipo siku tutakuja kuzitumia kuingilia.

tuliingia tukaangalia movie na kuinjoy sana,na kukiri kweli tulikuwa tunapitwa na vingi
 
Enzi za ze comedy

......kaeni chini,msikae kwa kochi.....chini,msiguse ukutani mnachafua rangi

Kabla hamjaingia mnakaguliwa weeeh, ze comedy ikiisha wanazima generator druuuuuuuuh..mnaambiwa mafuta yameisha,.....mkisepa wanawasha......

Ni vile tu utoto,makundi
Daaah aisee
 
mimi kijiji nilichokulia jamaa mmoja mwaka flani ilibidi anunue generator na tv hitachi + deki ,akawa anaonuesha tv weekend mpaka weekend kiingilio 100 tu,kijiji kizima mpaka vitongoji vya jirani walikuwa wanajaa hapo,yeye kazi yake ni kwenda kuchukua cassete mpya mjini tu.

sasa sisi mzazi wetu roho yake alikuwa anaijua yeye mwenyewe faza yule,sijui alikuwa anaona noma kutoa 400 tukasafishe macho au alikuwa hapendi tu tukajichanganye,maana kiukweli kwa pale kijiji tulikuwa na life flani la ngazi mbili zaidi ya wengine.siku hiyo jpili night ndio anakomaa tusome usikuasubuhi shule kila mwanafunzi mwenzetu anasimulia mkanda wa jana,yaani alituvuruga kwakweli.

siku moja akaenda seminar,mkewe na wanae wawili wa kike wakaondoka kusalimia mjini na mama yao,ndani ya nyumba tukabaki wawili,yaani mimi na dogo wa kiume mwanae wa kwanza,tukaaa kikao na dogo wote tukakubaliana haiwezekani jpili hii tusiangalie movie,yaani zitumike mbinu zozote mpaka tukaingie kutizama picha.tumeshapewa tetesi kuna picha moja linaitwa red scorpio,amecheza bw dolf ni mauaji.asubuhi kukakucha,nikampanga dogo,oya kaa hapa acha nikamwone yule mwenye kibanda tujue tunayajenganje.
nikapanda baiskeri na madumu ya maji kama nakwenda mtoni,kijiji kile maji yalikuwa ya shida kiasi.
njia ni hiyo unapita kwa huyo jamaa mwenye banda la video.nikafika pale nikamkuta,nikamchana kila kitu,akanambia aaaaah mbona hamna noma wewe niletee dumu mbili za maji jioni mnaingia kiroho safi yaani,nikasema yees mambo si hayo bana!!fasta nikaenda nikabeba maji by saa tano nageuka,nikafika nikamiminia maji nikaguka tena mtoni,saa nane niko home,nampa dogo feedback ananipiga kifua,hakuna kama wewe ancle

imefika saa kumi na mbili watu wanapita pale home nasisi tunajiuliza tusepe au vipi,namwambia dogo inabidi tuvunge mpaka kuku ziingine bandani tufunge mlango tupaache safe,mara faza house huyu hapa,sijui kama uliishawahi kulia bila kutoa machozi na sauti mkuu kwa uchungu mkubwa!!!ndio ilikuwa hivyo yan.
akakuta baiskeri tumeifungia vitu tumepanga kuuliza vizuri tukamwabia ah unajua tuko peke yetu tunaogopa kufanya kazi na giza so tunafanya mapema tukiingia ndani hakuna kutoka,ni kusoma na kulala.akaguna kisha akasema,leo nataka mwende kwenye banda la video ila tunakwenda wote.

ikawa vibe ila sasa itakuwaje tumeshalipa kwa maji???vipi mjuba akikabidhiwa hela akagomakinaumana,basi tukatoka haooooo kufika pale nikamiwahi jamaa kwamba achukue tu hela ila hizo dumu za maji ipo siku tutakuja kuzitumia kuingilia.

tuliingia tukaangalia movie na kuinjoy sana,na kukiri kweli tulikuwa tunapitwa na vingi
Daaah imenisisimua sana....watu wanatokaga mbali mno mwanang
 
...Kulikuwa na jirani familia ya kiarabu,mzee hana shida,mkewe sasa balaa,ana mjukuu wake sisi tulikuwa tunacheza nae mpira ndiye aliyekuwa anatuingiza.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom