Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni marehemu katika mwili mwingine!?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Mtambuzi, Aug 2, 2011.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Aug 2, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,609
  Likes Received: 788
  Trophy Points: 280

  Kuna wakati unakuwa mahali, halafu unahisi kwamba ulishakuwa mahali hapo kabla, na pengine ukiwa na watu wale wale. Lakini, kwa unavyojua, hujawahi kuwepo hapo, wala kuwa na watu hao.

  Hali ya uzoefu huu kufahamika kitaalamu kama Déjà vu. Kama nilivyosema awali kwamba, unakuwa katika sehemu ngeni unashangaa kuona kama kwamba, ulishawahi kwenda sehemu hiyo huko nyuma.

  Unaonana mtu kwa mara ya kwanza lakini unapata mawazo kama uliwahi kuonana naye huko nyuma. Hiyo ndiyo Déjà vu.

  Neno Déjà vu, asili yake ni lugha ya kifaransa ikiwa na maana kwamba, Tayari nilishawahi kumuona au mahali hapa niliwahi kupaona kabla, ikiwa na maana kwamba mtu anakutana na kitu kipya katika mazingira mapya na anagundua kwamba aliwahi kukumbana na hicho kitu kabla, pengine katika mazingira hayo hayo.

  Inasemekana kwamba, mambo haya ya Déjà vu ni ya kawaida. Kila watu saba katika kila kumi wanasema kwamba waliwahi kukumbana nayo angalau mara moja katika maisha yao.

  Neno hili Déjà vu lilitumiwa kwa mara ya kwanza na Emile Boirac (1851-1917), ambaye alikuwa mtafiti wa Kifaransa wa mambo ya akili za ziada za watu. Kuna maelezo mengi ya uzoefu huu, kama ifuatavyo: Unakutana na picha kwa mara ya kwanza lakini unagundua kwamba uliwahi kuiona zamani.

  Unafika mahali pageni na unagundua kwamba, mahali pale si pageni bali uliwahi kufika kabla. Lakini, kwa akili ya kawaida, unakumbuka kwamba hujawahi kufika hapo. Unaiona sinema mpya lakini unahisi kwamba uliwahi kuiona kabla. Na cha kushangaza ni kwamba unaweza hata kutabiri kitendo kitakachofuata na ikawa kweli, lakini hukumbuki na pengine hujawahi kuiona, kwani ni sinema mpya.

  Unakumbana na hali fulani au unafika mahali fulani pageni lakini unagundua kwamba hali ile au mahali pale uliwahi kupaona katika ndoto zako huko nyuma.
  Déjà vu pia inaweza ikaonekana katika unusaji, ladha ya chakula, mchanganyiko wa rangi, sauti ya juu au ya chini, kelele au kitu chochote ambacho kinafukua kumbukumbu ya mambo ya zamani.

  Mtu mgeni aliye mbele yako uvaaji wake na namna anavyoongea anaweza kukukumbusha mtu uliyekuwa umekutana naye kabla. Baadhi ya watu wanasema kwamba hali hii ya kufanana inaweza kusababishwa na hali ya ubongo kwa wakati huo.

  Watu wanaamini kwamba binadamu baada ya kufa roho yake inaingia katika mwili wa mwingine, wanasema kwamba kwa mujibu wa Déjà vu waliwahi kukumbana na hali kama hiyo zamani. Kunaweza kukawa na sababu na maelezo chungu nzima kuhusu Déjà vu.
   
Loading...