"ieleweke kuwa CCM peke yake bila ushirikiano toka kwa watu walio na itikadi ya vyama vingine haiwezi kuongoza nchi hii, vivyo kwa CDM, sasa sioni kwanini tusijenge ustaarabu katika kukosoana na kushauriana, badala yake tunajikita katika kudharirishana na kutiana maudhi, mbinu ambayo hutumika pale ambapo malengo ni kuangamizana na si kusaidiana na kurekebishana."
Lakini kitu ninachokiongea mimi hapa ni kifuatacho, tulikuwa na NCCR, waliokuwa NCCR waliongea waliyoyaongea wote tunaelewa kilichotokea. Tujiulize iko wapi NCCR ni nini kilitokea.
Japo ni vigumu lakini yatupasa tujifunze ustaarabu mpya, labda huo unaweza ukatusaidia.
Kama CCM imejaribu kufanya jambo ambalo linalenga kuleta muafaka wa kijamii, kwa nini isipongeze kwa hatua hiyo? Kama tutaamua kujivalisha unafiki na kujitia upofu wa kutoona jambo ambalo lipo dhahiri sidhani kama tutafika kule ambak tumekuwekea matamanio ya siku moja kukufikia.
Sidhani kama miongoni mwetu kuna mtu aliemsafi kwa kiwango kinachohitajika, na sielewi ni gauge ipi tunaitumia kupima na kuwapata watu wale tunaodhani kuwa ni wasafi.
Kuna watu wamejichagulia tabia ya kupinga kila kitu kifanywacho na watu walio upande wasio utaka wao, hapo tutakuwa hatujifunzi kitu wala hatujiandaa na mafanikio ya baadae, ieleweke kuwa CCM peke yake bila ushirikiano toka kwa watu walio na itikadi ya vyama vingine haiwezi kuongoza nchi hii, vivyo kwa CDM, sasa sioni kwanini tusijenge ustaarabu katika kukosoana na kushauriana, badala yake tunajikita katika kudharirishana na kutiana maudhi, mbinu ambayo hutumika pale ambapo malengo ni kuangamizana na si kusaidiana na kurekebishana.
Kuna njia ambazo ni za kisaokolijia zingeweza kutumika katika kurekebishana na hali na watu wangeelewana na maisha yangeendelea na maendeleo kupatikana, lakini kwa kuwa njia hizi za kisaikolojia ni tofauti na utashi wa kisiasa, acha na mimi niliongee katika mlolongo wa kisiasa.
Tuache tabia ya kubuni na kuunga unga taarifa ambazo mwisho wake ni kuchafuana kusiko na tija, kama wote lengo letu ni kusimama kama taifa moja imara katika nyanja zote za kijamii, yatupasa tushirikiane, tuwe wazi kiutambuzi kuwa pamoja na kelele zote CDM pia wana nafasi kubwa ya kushindwa kutimiza au kuyafanyia kazi yale wanayoyaahidi kwa wananchi kama vile ambavyo CCM inavyoshindwa.
Tuwe wakweli na kutambua mchango wa kila kundi katika kuijenga nchi yetu. Hakuna kundi la malaika miongoni mwetu, makundi yote yanaundwa na raia/binaadam dhaifu wenye mioyo na miili yenye asili na tabia za umimi, uchoyo, majivuno, tamaa, ubaguzzi,dharau,kukata tamaa, chuki,kuzaliwa, kuumwa kuishi na kufa.
Kama kuna watu wa kundi au chama fulani kinaundwa na watu wasio na tabia nilizozitaja hapo juu na wajitokeze.
Kwa hiyo unazungumzia maridhiano na ghafla unaweka vitisho, if I understand ur statement, unataka kutuambia kuwa CDM ni lazima ifanye some sort ya maridhiano na CCM otherwise iawatokea kama kilichotokea NCCR. Too low! mkuu jaribu nyingine.
Naona atleast tunasimama sehemu ambayo labda fikra zetu zikafikia muafaka, isipokuwa tu natofautiana na wewe unaposema kwamba vitu tunavyoongea huku "gizani" hatuwezi kuvisimamia kwenye jukwaa la hoja, hiyo sio kweli, hivi ni vitu ambavyo tunajadili mitaani kwetu, kwenye magazeti makini, kwenye midahalo mbalimbali ya wazi na kwa taarifa yako tu ni vitu hivi tu ambavyo vimekinyima ushindi chama "chako" huo wa kishindo wala sio eti hayo magamba mnayohangaika nayo sasa! Mi napendaga kusema kuwa hapa JF tunajadili TANZANIA MPYA (wengi wetu, sio wote).
Niende moja kwa moja kwenye hoja yangu. Nakubaliana na mawazo yako kwa kuyaweka kwenye hoja kwamba tunahitaji mjadala kitaifa kufikia muafaka wa Tanzania tunayoitamani badala ya kushikana uchawi...... kama sijakosea!
Mi naweza kusema kuwa, kwa fikra zangu, labda nipate ushauri au muongozo toka kwa wataalamu wa siasa sioni wala sijui ni namna gani mnaweza kufikia mabadiliko na mapinduzi matakatifu ya namna ya kujitawala na kusimamia rasilimali zetu na ustawi wote (wengine wanasema hii kuanza upya), kwa amani kama mnaserikali inayotawala ni kama hii yetu. Rejea baadhi niliyoyaandika hapo juu, pia mifano mingi tu kudhibitisha kuwa tunaserikali ya watu wa namna ninayoisema.
Natambua kwenye historia na mpaka sasa kuna baadhi ya nchi ambapo sarekali ndio kiongozi mkuu wa harakati za kupigania mustakabali wa watu wake (hata hapa kwetu ilipata kuwepo wakati wa mwalimu tu) lakini sio serikali zetu(kwanzia Mwinyi,Mkapa na huyu wa saiv)
Sipingi wazo lako, ndio maana nkasema naomba mtu anielekeze falsafa hapo kama hilo wazo lako linatekelezeka katika mazingira ya sasa? Mi binafsi naona hiyo ni nadharia tu, unazungumzia kuwa watu wanalalamika tu na kuwa malalamiko hayana tija..... narudi palepale pa saa zile kuwa katika mfumo ambapo hamna mkondo uliorahisi na wazi wa raia wa kuwasilisha matakwa yao ya jinsi wanavyotamani mambo yaende katika maisha yao ya kilasiku, wakati wamezungukwa na kero tupu toka mtu anapoamka hadi anapolala, pia kwa namna hiyo siju unataka watu wa kawaida wafanyaje.... ikumbukwe kuwa kuna asasi kadhaa za kiraia lakini nazo malalamiko yao juu ya serikali hii kila mtu anayasikia (tunaweza kulijadili kivyake hili) Sasa katika hilo wakulaumiwa sio watu kama mzee mkapa akakurupuka eti "....mitanzania mivivu" Mungu akamuumbua kupitia kwa Rais wa Botswana, watanzania wanaijenga Botswana huku... Ndugu yangu serikali ya Mkapa ambayo wengi wanaisifia saivi wanaisifia ndio hiyohiyo ya bwana JK (chama ni kilekile)
Sawa sisis ni watu wa kulalamika tu, ila ndio serikali zetu zimetujenga hvyo kwa manufaa yao kwamba wakati sisi tutaendelea kuwa walalamishi tu wao waendelee na zoezi la kubadili utajiri wa nchi kuwa wakwao na familia zao,
Ndugu yangu, mataifa yanajengwa na yanajengwa na watu wake lakini chini ya usimamizi wa wenzao miongoni mwao, Marekani ya leo ni zao la ndoto ya zaidi ya miaka mia nyuma na Obama anzungumzia Marekani ya miaka zaidi ya mia baada yake.
Na zaidi sana lazima tukubali kuwa uharibifu huu unaoendelea kwenye taifa hili utakuwa na athari kubwa sana kwenye kizazi kijacho, katika namna ambapo hamna namna yoyote ya kitaifa kuandaa vijana wake kuwajengea moyo wa kizarendo na uwezo wa kiutendaji na utaalamu (fuatilia mfumo wetu wa elimu kwanzia toka chekechea hadi chuo kikuuu, tutalijadili mda mwingine) juu ya nchi yao, hapo ni lazima bomu litalipuka tu marabaada ya utawala wa sasa, kwamba ni kweli nchi itayumba tu sio wakichukua upinzani bali hata wakibaki hao CCM,
Nimalizie, samahani kama nitakuwa nimekuelewa vibaya ila sauti ya maandikio yako ni kama mtu unaeamini katika "CCM MPYA", sitaki kukuhukumu pia ila kuendelea kuamini katika ccm tu ni kizingiti kingine cha kifikra...... kuna mambo ni kama "classical" kwa ccm tusipoteze mda kuaminisha kwenye ccm mpya, au msipoteze mda kujenga ccm, hizo rasirimali ni za thamani sana kwa nchi hii, ni bora watu makini kama nyie muache uoga wa kichama..... mje mjenge upinzani imara kwa manufaa ya taifa hili kwa vizazi vijavyo japo maana kizazi hichi chetu najua hatutaiapata hiyo TANZANIA MPYA, sababu ccm ishavunja misingi yote.
Sina hakika na vigezo unavyotumia kupata scrape value, kwa maoni yangu ni vya kibinafsi sana, labda utajiri na madaraka.
Kusema kila pesa inayopatikana inaishia kwenye mifuko ya mafisadi kunakutambulisha vizuri wewe ni nani na upo hapa kwa lengo gani, kwa sababu wizi upo lakini kuna barabara nyingi tu, madaraja yaani huduma za jamii japo siyo kwa kiwango ambacho tungependa. Sasa labda utuambie pengine ni wamarekani ndiyo wanatuletea mafanikio hayo kidogo au labda unatumia takwimu gani kupata hizo conclusions.
Sisemi Chadema hawawezi lakini kama mtanzania naamini kuwa siyo lazima Chadema ishike dola ili nchi iendelee kama wadau wengi wanavyoonekana kuamini hapa...
Nafurahi kuwa Wewe mwenyewe unakubali kuwa wizi upo, kipimo cha kuwa chama kimekuwa scrap au la si jambo la siri, achilia mbali ishara kama za ushindi finyu na uchakachuaji wa matokeo pia mpasuko ndani ya chama na kupoteza sifa (public image) zinatoa picha kamili.
Sisemi lazima CDM washike dola, ila CCM wasipofanya jitihada za dhati za kupiga vita ufisadi wao wenyewe bila presha lazima kitafika tamati. mbinu za danganya toto za kuondoa watu watatu halafu unaacha wengine unajifanya umepiga vita ufisadi hazikubaliki tena. Ukumbuke utajiri wa rasilimali iliyo nazo TZ ukilinganisha na hali ya maisha ya mtanzania kwa miaka 50 tangu uhuru havilingani. na tatizo hapa ni utawala bora, na ukizungumzia utawala bora maana yake unaitaja CCM moja kwa moja.
Ukweli ni kuwa wakati umefika wa kutaka mabadiliko, iwe CDM au CCm lakini mabadiliko ya kuweza kumkomboa mtanzania kutoka kwenye umaskini.