Consigliere
Platinum Member
- Sep 9, 2010
- 12,901
- 27,421
utumbo tuuuu,unataka tuwasifie CCM kwa lipi,nani asiyejua kuwa JK alipita kila kona ya nchi hii na kuwanadi EL,RA, na AC??leo hi Kikwete huyu huyu anasema eti hao marafiki zake wa zamani ni mafisadi ,,heee??alikuwa wapi wakati wa uchaguzi na alipowanyanyua mikono na kusema ni wasafi alikuwa anamdanganya nani??
KUWA WAZI KAMA NA WEWE UMEOLEWA KWA KIKWETE TUJUE SIO UNATULAZIMISHA KUSIFIA UTUMBO
Bora kupambana kupiga vita ufisadi, uchakachuaji wa CCM kwa Tanzania kuliko kusifia upuuzi na upotofu, uzandiki na ujambazi ili kuijenga Tanzania mpya na nzuri kwa vizazi vya baadae! UHUNI WA CCM WA UTAWALA WA HAUKUBALIKI! I WILL PERSONALLY FIGHT IT AT ANY COST!
HIZI SI ZAMA ZA WOGA!
Japo ni vigumu lakini yatupasa tujifunze ustaarabu mpya, labda huo unaweza ukatusaidia.
Kama CCM imejaribu kufanya jambo ambalo linalenga kuleta muafaka wa kijamii, kwa nini isipongeze kwa hatua hiyo? Kama tutaamua kujivalisha unafiki na kujitia upofu wa kutoona jambo ambalo lipo dhahiri sidhani kama tutafika kule ambak tumekuwekea matamanio ya siku moja kukufikia.
Sidhani kama miongoni mwetu kuna mtu aliemsafi kwa kiwango kinachohitajika, na sielewi ni gauge ipi tunaitumia kupima na kuwapata watu wale tunaodhani kuwa ni wasafi.
Kuna watu wamejichagulia tabia ya kupinga kila kitu kifanywacho na watu walio upande wasio utaka wao, hapo tutakuwa hatujifunzi kitu wala hatujiandaa na mafanikio ya baadae, ieleweke kuwa CCM peke yake bila ushirikiano toka kwa watu walio na itikadi ya vyama vingine haiwezi kuongoza nchi hii, vivyo kwa CDM, sasa sioni kwanini tusijenge ustaarabu katika kukosoana na kushauriana, badala yake tunajikita katika kudharirishana na kutiana maudhi, mbinu ambayo hutumika pale ambapo malengo ni kuangamizana na si kusaidiana na kurekebishana.
Kuna njia ambazo ni za kisaokolijia zingeweza kutumika katika kurekebishana na hali na watu wangeelewana na maisha yangeendelea na maendeleo kupatikana, lakini kwa kuwa njia hizi za kisaikolojia ni tofauti na utashi wa kisiasa, acha na mimi niliongee katika mlolongo wa kisiasa.
Tuache tabia ya kubuni na kuunga unga taarifa ambazo mwisho wake ni kuchafuana kusiko na tija, kama wote lengo letu ni kusimama kama taifa moja imara katika nyanja zote za kijamii, yatupasa tushirikiane, tuwe wazi kiutambuzi kuwa pamoja na kelele zote CDM pia wana nafasi kubwa ya kushindwa kutimiza au kuyafanyia kazi yale wanayoyaahidi kwa wananchi kama vile ambavyo CCM inavyoshindwa.
Tuwe wakweli na kutambua mchango wa kila kundi katika kuijenga nchi yetu. Hakuna kundi la malaika miongoni mwetu, makundi yote yanaundwa na raia/binaadam dhaifu wenye mioyo na miili yenye asili na tabia za umimi, uchoyo, majivuno, tamaa, ubaguzzi,dharau,kukata tamaa, chuki,kuzaliwa, kuumwa kuishi na kufa.
Kama kuna watu wa kundi au chama fulani kinaundwa na watu wasio na tabia nilizozitaja hapo juu na wajitokeze.
Japo ni vigumu lakini yatupasa tujifunze ustaarabu mpya, labda huo unaweza ukatusaidia.
Kama CCM imejaribu kufanya jambo ambalo linalenga kuleta muafaka wa kijamii, kwa nini isipongeze kwa hatua hiyo? Kama tutaamua kujivalisha unafiki na kujitia upofu wa kutoona jambo ambalo lipo dhahiri sidhani kama tutafika kule ambak tumekuwekea matamanio ya siku moja kukufikia.
Sidhani kama miongoni mwetu kuna mtu aliemsafi kwa kiwango kinachohitajika, na sielewi ni gauge ipi tunaitumia kupima na kuwapata watu wale tunaodhani kuwa ni wasafi.
Kuna watu wamejichagulia tabia ya kupinga kila kitu kifanywacho na watu walio upande wasio utaka wao, hapo tutakuwa hatujifunzi kitu wala hatujiandaa na mafanikio ya baadae, ieleweke kuwa CCM peke yake bila ushirikiano toka kwa watu walio na itikadi ya vyama vingine haiwezi kuongoza nchi hii, vivyo kwa CDM, sasa sioni kwanini tusijenge ustaarabu katika kukosoana na kushauriana, badala yake tunajikita katika kudharirishana na kutiana maudhi, mbinu ambayo hutumika pale ambapo malengo ni kuangamizana na si kusaidiana na kurekebishana.
Kuna njia ambazo ni za kisaokolijia zingeweza kutumika katika kurekebishana na hali na watu wangeelewana na maisha yangeendelea na maendeleo kupatikana, lakini kwa kuwa njia hizi za kisaikolojia ni tofauti na utashi wa kisiasa, acha na mimi niliongee katika mlolongo wa kisiasa.
Tuache tabia ya kubuni na kuunga unga taarifa ambazo mwisho wake ni kuchafuana kusiko na tija, kama wote lengo letu ni kusimama kama taifa moja imara katika nyanja zote za kijamii, yatupasa tushirikiane, tuwe wazi kiutambuzi kuwa pamoja na kelele zote CDM pia wana nafasi kubwa ya kushindwa kutimiza au kuyafanyia kazi yale wanayoyaahidi kwa wananchi kama vile ambavyo CCM inavyoshindwa.
Tuwe wakweli na kutambua mchango wa kila kundi katika kuijenga nchi yetu. Hakuna kundi la malaika miongoni mwetu, makundi yote yanaundwa na raia/binaadam dhaifu wenye mioyo na miili yenye asili na tabia za umimi, uchoyo, majivuno, tamaa, ubaguzzi,dharau,kukata tamaa, chuki,kuzaliwa, kuumwa kuishi na kufa.
Kama kuna watu wa kundi au chama fulani kinaundwa na watu wasio na tabia nilizozitaja hapo juu na wajitokeze.
Mkuu elewa kuwa sifundishi kusifia wala kutukana, ninachokifanya ni tujiangalia na kujitambua sisi ni wakina nani na mahitaji yetu ni yapi, tukosoane sawa, tushambuliane sawa, lakini CCM si ya kulaumiwa katika ujumla wake, na wala hatukatai kuwa ndani ya CCM hakuna aina ya watu wanaotuhumiwa kwa kiwango hicho, wapo na wamechangia sana kudhoofisha hali ya nchi na kutuacha hapa tulipo.
Ninachojaribu kuonyesha hapa ni kuwa munaposhambulia CCM ieleweke kuwa ndani ya chama hicho kuna kundi lingine ambalo nalo linapambana kama wafanyavyo wafanyavyo watu wa vyama vingine dhidi ya watu au kundi lile lile.
Ndiyo maana nimesema matusi ya jumla ni kujenga ufa tu kitu ambacho hata baada ya vita kulishinda kundi kundi linalolalamikiwa hatutaweza kukaa pamoja na kuwajibika kwa maslahi ya taifa, kwasababu tayari tutakuwa tumejijengea picha kwamba kitendo mtu kuwemo ndani ya chama fulani ni tayari huyo ni mdhambi. Kila upande unahitaji changamoto ili kuwza kujijenga na kuwa imara.
Hapo ndipo tunapofika mahali tujihoji je dhamira yetu ni ipi?
CHADEMA ilijipanga vizuri sana, kwa kiwango ambacho kama ingeshinda uchaguzi wa mwaka jana ingepata ushirikiano mkubwa na wa hali ya juu kutoka kwa watu mashuhuri waliopo ndani ya CCM, hii inatokana na ukweli kuwa katika uchaguzi wa mwaka jana walikuwa na uungwana mkubwa kwa kuweza kuwatenganisha watu dhai na watuhumiwa waliomo ndani ya CCM na CCM yenyewe.
Lakini sasa hivi inaonekana kuwajumuisha wote kuwa ni sehemu ya tatizo....hebu tufikiri kwa pamoja, nini kitarajiwe hapo mkuu?
Naona Musembi unavuta shuka asubuhi. Huu ushauri kawape akina makamba kule Lushoto hapa jf tunajadili jinsi ya kuizika ccm maana ilishakufa
Naona unatafuta Comfort zone Mkuu, hapa sio zenji kutaka muafaka baada ya kuona mambo yanaenda doro. CCM and its bureaucratic machinery will never bring the change we want in Tz. Na hatutaki Suluhu katika hili. Tumeshatafakari tafakuri zote, hadi unazohisi hatujatafakari. Hatutaki muafaka wala kisingizio chenu cha oooh mnahatarisha amani, oooh mnakua wachochezi. CCM ni nyoka mbaya sana, mnatuchekea majukwaani na kwenye hotuba huku mwatutafuna sisi na nchi yetu, wazi wazi na nyodo mnatuletea!
Kwa nidhamu ya woga na ufisadi wenu mtachakachua hadi nguo zetu za ndani!
WE WANT CCM OUT, (WABAYA NA WAZURI WAKE WAKIWEMO) CCM OUT CCM OUT CCM OUT CCM OUT!
Mheshimiwa nadhani kuandika kila mtu anayo uwezo ya kuandika, ila kutoa hoja za msingi ni kipaji sio kila mtu anacho.
kabla sijaenda kwenye hoja ya msingi naomba nianze na hili: kama viongozi na wana CDM wataacha kupiga kelele kuhusu ufisadi na kurukia kwenye HIV/AIDS,MARALIA,MAGONJWA MBALIMBALI,MAMBO YA KILIMO,UFUGAJI Hivi vitafanyikaje wakati vinahitaji pesa na kila shilingi inaopatikana mafisadi wanakusanya wanaweka mfukoni mwao? au itabaki na wao kuwa wahubiri wa sera na ahadi hewa maana hela zote zimeshaliwa na MAFISADI huku wao wakiwahubiria wananchi mambo ambayo ni ndoto za alinacha?
Kimsingi CCM imeshayahubiri haya yote chini ya mwamvuli wa maisha bora kwa kila mtanzania, lakini hakuna lililofanyika na sababu kubwa wamesingizia uwezo mdogo. ila kuna mabilioni yameibiwa kwa hiyo jibu unalo kuwa cha kuongelea ni ufisadi kwa sababu ndio unaokomba pesa za kutekeleza hayo mambo ndiyo maana yameshindikana.
Nikirudi kwenye hoja ya msingi ni kuwa siasa duniani kote zimesimama katika msingi wa kukosoana na kurekebishana, isipokuwa kurekebisha au kukosoa kitu lazima kuwe na kiwango. ikizidi hapo lazima kufuta/kutupilia mbali na kuanza upya. hata gari kuna kiwango cha uharibifu kikishafikiwa linakuwa scrap, haliwezi kurekebishwa tena, linatupwa. Mahali walipofika CCM ni pa kutupilia mbali na kuanza upya. na kwa hapa hatuwezi kukubali vitu vidogovidogo vya kisanisanii tunaunga mkono ati kuwa wamerekebisha.
sikatai kuwa ni vizuri walivyofanya, mfano hatua za JK za kuvunja kamati kuu kwa nia ya kuondoa ufisadi. ila hili ni jambo dogo sana ambalo haliwezi kubadilisha mwelekeo wa wengi ambao wameshaichoka CCM, kwanza ni watu watatu tu walioguswa wakati mafisadi CCM hawako watatu tu wako wengi. Lakini muda ambao hatua hizi zimechukuliwa ukilinganisha na kipindi ambacho wananchi wamelalamikia ufisadi inaonekana kuna usanii wa hali ya juu.
Vitendo kama vya kuwasafisha mafisadi wakati wa uchaguzi halafu wameshachaguliwa leo unasimama hadharani kusema waachie ngazi ktk chama kwa kuwa ni mafisadi ni ukanganyifu wa mabo na kuonyesha kuwa ama watz hawana akili au yeye JK hana mwelekeo.
Kwa kumalizia tu ni kuwa CDM hawapingi kila jambo yapo mambo ya msingi wanaunga mkono. Mfano katika kikao kilichopita cha bunge waliunga mkono hoja ya kuanzishwa kwa mfuko wa mahakama. ila walipinga hoja ya mchakato wa kuunda katiba mpya na hili lilipingwa na kila aliye na mapenzi meme na TZ. yapo pia mengine mengi. sasa msingi wa hoja yako kuwa tunapinga kila kitu uko wapi wakati umeona wazi ya msingi yameungwa mkono?
Wewe elewa tu kuwa CCM kinakufa kwa sababu ya kukumbatia UFISADI na wacha kife usijifanye msamaria mwema wa kumwagia maji na kukipepea wakati na wewe unateseka kama waTZ wengine shauri ya ufisadi
we mbumbumbu unaongea matapishi tuu kama sio takataka,CDM will never take control of this country with politics of kutaja taja majina na kukosoa kila kitu kinachofanywa na serikali,jifunzeni nchi zingine zilizokomaa kisiasa maana ya upinzani sio kukosoa kila kitu hata kama baadhi ya mambo yanafanywa kwa lengo la kuwasaidia wananchi! i though baada ya CDM kugaragazwa katika uchaguzi mkuu wangetumia nafasi hii kuwaeleza wananchi sera zao,mikakati yao na labda kutoa mipango mbadala itakoyosaidia kuijenga nchi yetu,sasa mmekalia kelele za ufisadi? ni kweli ufisadi hatuutaki lakini kuna mambo mengi ya kuwaambia wananchi kama vile mambo ya HIV/AIDS,MARALIA,MAGONJWA MBALIMBALI,MAMBO YA KILIMO,UFUGAJI mi nafikiri ili lingewajenga zaidi au mnataka tuamini nyie hamna sera kabisa za kuwaambia wananchi wa Tanzania zaidi ya nyimbo ya ufisadi ambayo sasa imekuwa mdomoni mwenu kila siku??
Bado tuna tatizo katika uelewa, japo hoja zinazotolewa ni nzito na uzito wake unatokana na ukweli uliomo ndani ya hoja hizo.
Lakini kitu ninachokiongea mimi hapa ni kifuatacho, tulikuwa na NCCR, waliokuwa NCCR waliongea waliyoyaongea wote tunaelewa kilichotokea. Tujiulize iko wapi NCCR ni nini kilitokea. Ninachokiongea hapa ni kwa ajili ya afya ya siasa zetu.
Tunapojadili na kuchangia katika siasa ni vizuri tuongee katika hali ya kwamba wakati wowote tunaweza sisi tukapewa majukumu ndani ya vyama vyetu, je mara muda huo utakapofika tutaendelea kuongea mambo haya tunayoyaongea tukiwa ndani ya majina ya bandia? Hatuoni kuwa kwa kutumia muda mrefu kujiamini tukiwa gizani kunatuondolea fursa ya kujizoeza kuongea hadharani na hivyo kukomaza udhaifu wetu wa kutokuwa na ujasiri wa kuwakibili wale tunaodhani ni tatizo kwetu? Pia tunajiondoa binafsi katika nafasi ya kuwa viongozi itakapobidi hivyo kuishia kudhani kuwa kuna watu maalum wapo kwa ajili ya kutuongoza?
Binafsi sijawahi kusita kuongea kile ninachokiamini, ninasikia faraja kama mtaniokosoa na kunihukumu kwa hoja na mtazamo wangu, na nipo tayari kubadilika kama nitathibitisha kuwa hoja yako ni sahihi. Ila jambo baya kuliko yote katika maisha yangu ni kuwa mtu mwenye kauli mbili katika maisha, yaani mchana niongee hivi na usiku niongee vingine, kwa kuzingatia hilo hapo ndiyo msingi wa hoja yangu unapotokea kuwa je kauli na matendo yetu yanaweza kuleta mchango wowote ili kupata mageuzi? Kuna mtu amesema hatuhitaji malaika wala watu wasafi kwa kiwango hicho bali wanaotambua kuwa kuna usafi katika maisha na watu na wanaotamani kuwa wasafi, hilo ni kweli kabisa, tatizo ni kuwa hoja nyingi zinazotolewa ni za mkato sana na zinazohitimisha kuwa kuwa anaehitajika ni mtu mwenye vigezo vya malaika.
Tunahitaji viongozi wanaowajibika kwa wananchi, ambao watatutengenezea miundo mbinu itakayoharakisha maendeleo yetu na aina hiyo ya viongozi inapatikana na ndani ya jamii ya watanzania sisi ambao tumegawanyika katika misingi ya kiitikadi tofauti, je ni sahihi tofauti hizi za kiitikadi zitunyime fursa ya kutumia uwezo wa watanzania wengine waliopo katika vyama vingine. Ndani ya CCM kuna tupo tunaoshauri kuwa katiba ya chama ibadilishwe ili kuruhusu wapinzani kuingia katika baraza la mawaziri kwasababu kuna rasilimali watu ya nzuri sana kule, ndani ya CCM tupo wanachama ambao tunathamani mchango wa upinzani nchini na na wengine wanavipa msaada, tupo wengi ndani ya CCM ambao tunaamini kuwa maslahi ya chama si jambo la kupangiwa mkakati na kuingia gharama, bali ni suala la chama kuwajibika kwa wananchi kwa kadiri ilivyotarajiwa.
Hapo ndipo ninapokuja kuhoji usahihi wa lawama za jumla, aina ya lawama ambazo kwa hakika hazitasaidia bali zitalizorotesha na kudumaza maendeleo ya taifa. Lawama na mashambulizi ambayo tuna ujasiri wa kuyafanya tukiwa gizani lakini hadharani hatupo tayari.
Ndiyo maana nasema tusimame pamoja na tuongee kama taifa lugha itakayomfanya mtu kujitambua na tuungane pamoja kumpiga vita kwa namna yoyote ile mtu ambaye anahatarisha maslahi ya taifa na anayejaribu kufuja mali za nchi, na kudhani kuwa anstahili zaidi hayo kuliko wengine.
Sijui kama kuna mwana-CCManayeweza akasimama hadharani na kuongelea uzuri wa CCM, pamoja na kuwa na mambo mazuri iliyoyafanya katika utawala wake, lakini haya mabaya yaliyofanywa ya kuweka kigingi katika guruduma na kukwamisha maendeleo ya taifa hakika yametuchafua wote ndani na nje kama wanachama na kama watanzania, watu hawa hatuna haja ya kuwaonea huruma wala kubembelezana nao.
Lakini swali langu lina baki pale pale kuwa je lawama za jumla zina tija yoyote kwetu kama taifa??
Pia muelewe kuwa kama mimi na ninyi hatutajiandaa na kuwa tayari kuwa viongozi kwa kuishi, kutenda na kuongea vile inavyompaswa kiongozi aliyepo madarakani basi tuelewe kuwa tunatengeneza kundi la walalamikaji daima dawamu.